GUARDIOLA NI KAMA VAN GAAL NA SI KAMA VAN GAAL
GUARDIOLA NI KAMA VAN GAAL NA SIO KAMA VAN GAAL...
Kichwa cha habari kinaweza kuwa kigumu kidogo kueleweka!.... Kuna jamaa mmoja hivi aitwaye Xavier sala-i-martin ambaye alikuwa mhazini wa Barcelona na ambaye pia ni Proffesor wa Uchumi aliwahi kusema mfumo wa Guardiola ni sawa na brand ya Zara! Unaweza ukauliza Zara ni nini? Na mimi lazima nikuulize swali kwanza? Unamjua Louis Vuitton? Huyo sasa ndo aliyeanzisha hii brand miaka ya 1975. Hii ndo brand ya nguo iliyotikisa zaidi Spain na Duniani kwa ujumla.....
****************************
Alimaanisha nini bwana Xavier, alimaanisha Guardiola haishiwi mbinu.. Alimaanisha Guardiola ni brand iliyotikisa zaidi kwa mifumo (style mbalimbali). Huyu Guardiola sio muoga wa kubadili mfumo hasa pale anapohitaji matokeo fulani...amekuwa akitumia zaidi mfumo wa pasi nyingi, na hasa pale mfumo unapogoma basi utaona Beki wa kati akicheza pasi ndefu zaidi (kumbuka ushindi wa goli 3-0 dhidi ya BVB november mwaka jana) si unamjua Martinez? Huyu sasa mara nyingi alikuwa anamchezesha kama Team Ball winner hasa kipindi anacheza nyuma ya Mandzukic....
@@@@@@@@@@@@@@
Nadhani bado sijazungumzia kichwa cha makala hii... Ila twende taraatibuu utaelewa namaanisha nini... Jamaa ana kitu kina false 9.... Yaan ni sawa na kusema namba 9 kisheti.... Au namba 9 hewa! Mara nyingi mpira ulipokuwa ukimkataa David Villa basi utashangaa Messi anasimama kama namba 9... Jamaa alipoichukua Barca alimtimua Eto'o na dinho... Akaanza na mfumo huo false 9 akimtumia zaidi Messi... Wapo watu wataniuliza katumia vipi huu mfumo Buyern, ikiwa alikuwa na namba 9 wengi tu kama lewa, mandzukic na Muller! Huu mfumo huwa anautumia zaidi katikati ya mchezo hasa pale anapomtumia Gotze kumpokea namba 9.
++++++++++++
Nasema Guardiola ni kama Van gaal na is kama yeye kwa sababu kwanza wote sio waoga, wagumu kusikiliza watu.. Ukibishana nao huwa ni wepesi wa kufanya maamuzi mengine mabaya!.... Guardiola Ni mtu mwenye maamuzi ya ajabu! Kuna wakati aliwahi kumtumia Gustavo kama kiungo wa pili mkabaji halafu akampandisha Schwensteiger kama namba 10 ingawa hii teknik ilikubal na ilizaa matunda. Van gaal nae amekuwa na tabia hizi hizi za kubadilisha wachezaji nafasi zao mara kwa mara bila kujali maneno ya mashabiki! Van Gaal na Pep ni moja kati ya waalimu wanaobadilisha nafasi za wachezaji au mifumo katikati ya Mchezo hasa pale wanapodhani kuwa kuna uhitaji wa hilo.
@@@@@@@@@@@@@@@
Ukirudi nyuma tena kidogo kuna mchezo kati ya Buyern na Mainz iliyoisha 4-1 msimu uliopita... Unaambiwa Lahm alicheza zaidi ya nafasi 4. Kuna mchezo mmoja ya liverpool na man utd ambapo rooney alicheza kama namba , 9,10, 8..
Guardiola vs Van Gaal (ushambuliaji)
Kuna aina fulani ya washambuliaji wanaitwa Withdrawn striker... Hawa n viungo wenye uwezo mkubwa wa kuingia kwenye box na kuleta madhara.... Guardiola amekuwa mgonjwa wa hawa watu na ndio maana alitumia gharama kubwa kumpata Mario Gotze kwa ada ya Paund 32... Van gaal amemtoa Javier Hernandez, na Robin Van Parsie maana hawa ni Orthodox Striker... Amemleta Mephis Depay na Martial hawa ni Withdrawn Strikers! Ukijaribu kuwaangalia utagundua hawa n watu wawili ambao wapo sawa kiasi fulani... Rooney alikuwa mshambuliaji mzururaji ila kwa sasa amekuwa Neutral haeleweki jukum lake lipi.. Muda mwingi Amekuwa akisubiria mipira... Amechukua jukumu la muller aliyekuwa akicheza chini ya Hiyckens... Kwa sasa muller wa Guardiola amekuwa mshambuliaji mzururaji yAan jukumu la Rooney zaman... Anacheza mpaka wingi ya kulia... Kuna vitu van gaal na Guardiola wanatofautiana ndipo nasema van gaal is Guardiola ila Guardiola ni kama Van gaal kwa wakati fulani....
#################
Mabeki..........
Van Gaal anatumia 3-4...... Naamaanisha mabeki watatu tu sawia na Guardiola... Labda niseme tu kwa ufupi... Nadhan unamjua alaba.... Austria anacheza kiungo... Buyern anacheza kama wing back.... Wakati fulani anacheza hata kiungo... Young, blind, valencia na shaw pia wametumika hivi hivi na Gaal.... Achilia mbali lahm ambae nae ametumika hivi... Makocha wote mpira wao upo katikati... Ukishika kiungo chao basi.... Kiufupi Kama United watamleta Guardiola basi watakuwa wamebadili majina tu lakin aina ya mfumo utabaki ule ule ila tu kitakachobadilika n attitude za wachezaji.... Itategemea watampokea vip? Je atawatreat vip maana suala la mfumo wote ni mpira wa pasi nyingi, mfumo ni 3-4-2-1.... Wote wana falsafa za ubishi na ukolon..... Tutaendelea
Leave a Comment