MAREFA NI MAADUI ILA MAKOCHA NI MALAIKA

MAREFA NI MADUI MAKOCHA NI MALAIKA!

Hivi ulishawahi kujiuliza Man utd na Chelsea zikifungwa nani analaumiwa? Utasikia Ferguson akimtukana Mike Dean, utasikia Mourinho akisema Howard webb ametunyima penati..... Ile ilikuwa sio offside n.k... Hata refa achezeshe vizuri huwezi sikia akisifiwa hata siku moja.... Heshima hii anayo muitaliano colina tu....


Wachezaji wanawaheshimu makocha kuliko marefari wa michezo... Wachezaji wanawafanya waamuzi kama watoto wa shule..... Kuwatolea kauli chafu n.k...unakuta timu ni mbooooooovuuu.... Ila watamkimbilia refa kama timu fulani hivii pale london...watamkoromea mwamuzi.. Watatoa maneno machafu utadhani wamehukumiwa kufaa.... Kwa upande wa mchezo wa rugby refa anakuwa mfalme kuliko hata mwalimu.... waamuzi wa Rugby hata wafanye maamuzi machafu vipi lakin huwezi ona amenyooshewa kidole...tena refa wa Rugby anaitwa Sir... Kwenye Rugby ukimfokea Refa ni adhabu kubwa kwa timu nzima......


wachezaji wa Brazil na Crotia wakimzonga mwamuzi

Timu ikifungwa huwezi kusikia kwenye mahojiano kocha akizungumzia uzuri wa refa hata kidogo....kilichopo tusiwafanye Marefa kama wapumbavu.... Tusiwaone kama watu ambao hawakosei... Inabidi tuwakoromee akina Giroud ambao wanabaki na goli wanakosa na sio refa aliyewanyima Penati... Mara ngap wachezaji wanakosea lakini hatuwazongi??? Juzi kadi nyekundu ya Collocine imefutwa... Sijui FA wamemaanisha nini...collocine alitolewa kwenye mechi dhidi ya Sunderland na huyu refa aliyemtoa ameonekana kama refa aliyefanya maamuzi ya kipuuzi... Huyu refa anajulikana kama Madley wengi wamepinga maamuzi hayo... Binafsi nasema ya ngoswe mwachie ngoswe....


refa phil dowdy..... Mashabiki wa Spurs wanasema huyu anatoa kadi kama nyanya

Nadhani FA wanapaswa washughulikie suala kubwa sio hili la juzi kati.... Kumtoa Gibbs badala ya chamberlain hayo ndo mambo FA wanapaswa washughulike nayo.... Maana wakiamua kufuatilia kila kitu itabidi basi marefa wapewe jicho la tatu... Unapaswa ushangae inakuwaje goli la Collocine la uwazi linakataliwa na FA wanafanya kama wao hawahusiki....ni ajabu sana... FA wanaamini maamuzi ya watu watatu ambao wanakaa katika ile kamati ya INDEPENDENT PANEL ni ya muhimu zaidi kuliko marefa wanne wanaokuwa uwanjan....


kiboko ya kadi Mark Clunterburg huyu hana utani uwanjani

Je refa ana uwezo wa kukata rufa juu ya INDEPENDENT PANEL?? Je mwisho wake nini? Shirikisho kubwa kama FA linapoanza kuangaika na kasoro ndogo uwanjan basi wanataka kufanya mchezo wa soka kama amri 10 za Mungu... Kufuta kadi nyekundu ovyo kama vile ni kumaanisha Refa sio chochote sio mwamuzi ila ni mpiga filimbi tu... FA ni sawa wanajamba halafu wanauliza harufu mbaya imetokana na nini.... Walichofanya kwa Bobby Madley ni kuwanyima marefa haki na nguvu....


No comments

Powered by Blogger.