SUAREZ KWA RONALDO? ACHENI MATUSI
Kijiwe chetu
KWANINI RONALDO NA SIO SUAREZ
Nmetembelea mitandao mingi nmegundeua kuwa watu wanalalamika Ronaldo kuwekwa tuzo ya ballon D or huku suarez akiachwa! Lakini kuna mtu kanambia kwani ile ni Barcelona D or ndo kila mchezaji wa barca aingie? Kuna kitu kinaitwa balance! Ndio maana utashangaa kill music walimpa Ali kiba tuzo ambazo hata hakustahili...
*******************************************************************
Ukijaribu kuangalia msimu wa 2010 iniesta na Sneijder walistahili kuchukua zile tuzo kwa mafanikio ya klabu zao! Hapa nataka kuwakumbusha kitu... Dwight York alitwaa zaid ya makombe manne makubwa lakini hakuna aliyemwangalia na Rivaldo akabeba tuzo ile, Drogba nae aliwahi kufanya maajabu na chelsea ila nani aliyemzungumzia?.. Mmesahau kuhusu Canavaro??
*******************************************************************
Ballon D or sio tuzo ya mwenye magoli mengi au vikombe vingi!!! Ile sio Golden shoe award.... Ile ni individual award! Tuzo ya mtu binafsi.... Tupilia mbali maneno ya kishabiki ya mtaani... Ronaldo anapaswa kusindikiza kwenye hii tuzo na sio suarez! Mafanikio ya barca, au assist au hata magoli aliyofunga hayatoshi tu kumweka kwenye kundi la wale watakaopaswa kukaa kiti cha mbele kumpigia makofi Messi akibeba tuzo yake ila ronaldo ambaye kiwango chake ni kikubwa na hakiwezi kuathiriwa na alichofanya suarez!
******************************************************************
Suarez alifanya vizuri lakini kwenye uwezo binafsi mbele ya Ronaldo ni matusi... Watu wataniuliza mbona hata diarby ana uwezo binafsi basi nae awekwe! Uwezo wa Ronaldo upo wazi kwamba ni nani wakulinganishwa nae! Amefanya vizuri... Amejitahidi kwa kadiri alivyojitoa lakin jitihada hizo zimemuhakikishia kiti cha mbele tu.. Nadhani hizi ni shukran tu za FiFa kwa Ronaldo kwa ufalme wake wa takriban miaka 7 ndani ya tuzo hizi... Ni rekod nzuri ya aina yake
Leave a Comment