TUNABAGULIWA HATA KWENYE BARA LETU

aliyekuwa kocha wa raga afrika kusin bwana Meyer

TUNABAGULIWA HATA KWENYE BARA LETU??

Na Priva ABIUD

Ushawahi kufuatilia mchezo wa Raga? Kwanza unajua maana ya Mchezo wa raga? Haya labda kama hujui.... Basi ni ule mchezo watu wanapigania mpira kwa nguvu na kukimbia nao..... Hapa afrika nchi kama kenya na afrika kusini ndio wakali wa huu mchezo..... Tanzania mhhh labda tuache kula chips ovyo....

Afrika kusini wamepatwa na Pigo, binafsi mimi sijajua kama ni pigo kwa wote ama lah.... Heyneke Meyer ndio kocha springbok yaan timu ya taifa nchi hiyo kwa jina la utani.... Inasemekana kuwa kocha huyo aliongeza mkataba lakini siku ya tarehe 3 mwezi huu kocha huyo ametangaza kuacha kuendelea kuifundisha timu hiyo! Ila nmesikia tatizo ilikuwa ni kuhusu wachezaji weupe na weusi kwenye timu hiyo ya taifa..

Cosatu shirika moja ya biashara nchi humo lililamikia kitendo cha kocha huyo kuwa na ubaguzi wa wazi kwa kuwaacha wachezaji weusi watano makusudi kwenye kikosi chake. Msemaji wa Shirikisho la Raga  ajulikane kama Nyaniso Sam alisema malalamiko ya Cosatu sio ya kweli na ni uchochezi tu.. Shirika hilo la Cosatu lilisema linahitaji kocha atakaewakilisha taifa hilo kwa ujumla na sio rangi fulani....


Mbali na kuingoza springbok mpaka nafasi ya tatu kwenye kombe la dunia mashabiki wengi wamesema hawawezi kusamehe kitendo cha timu yao kupoteza kwa timu dhaifu kama Japan na Argentina. Raisi wa shirikisho la mchezo huo nchini afrika kusini bwana Oregen Hoskins amemshukuru sana kocha huyo aliyepata mafanikio kuliko kocha yoyote..


Swali linakuja hivi waziri wa Michezo Bwana Fikile mbalula hakuliona hilo tokea mwanzo? Kwanini ifike mahali mpaka watu wanaingilia? Kwanini watu weusi tunanyanyasika hata kwenye bara letu? Maana nilisikia huyu waziri baada ya kusikia tuhuma hizo alikataa kuongea chochote... Maana kuna watu walilalamika kuwa kati ya wachezaji walikua fom ni wachezaji weusi ambapo walipochanganywa na hao makaburu kwenye michezo ya super 15 timu ilifanya vizuri... Lakin kwenye kombe la dunia kuna watu kama Jean De Villiers ambaye hata kukimbia ilikuwa tabu nae aliitwa kwenye timu ya taifa....kwanza alimweka nje winga Cornal Hendricks na lwazi mvovo na kumweka chalii fulan mwenye miaka 21 Rookie Jesse Kriel kwenye nafasi ambayo hata hajawahi kucheza....


No comments

Powered by Blogger.