CHELSEA YAWEKEWA DAU NA MUUZA MADAWA YA KULEVYA

MUUZA MADAWA YA KULEVYA AWEKA DAU CHELSEA

Hii sio taarifa ya usajili wala sio taarifa ya kisoka zaid, muuza madawa ya kulevya bwana El chapo jina halisi Joaquin Guzman kutoka mexico aliyekamatwa hivi majuzi amekuwa kivutio kikubwa mwezi huu baada ya kugundulika amekuwa akiwalipa baadhi ya wachezaji mishahara.

Mwanaume huyu aliyetoroka gerezani kwa mara yaa pili miezi 6 iliyopita alipotoroka kwa kutumia bomba la chini ya ardhi inasemekana kuwa alikuwa tayari kuinunua klabu chelsea. El chapo ambaye ni mshabiki mkubwa wa soka alidai kuwa atainunua chelsea na kuibadili icheze soka safi kabisa. Guzman anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilion moja sawa na trilion 3 za madafu hapa Bongo.

Ni mshabiki mkubwa ligi ya MX akishabikia Puebla. Taarifa pia zinadai Kuwa mwanaume huyo alikuwa tayari kuinunua klabu hiyo ambayo Roman Abramovich alinunua E140 mnamo mwaka 2003. Huyu mtu anasemekana kuwa muuza madawa mwenye nguvu zaidi dunian kwa sasa

No comments

Powered by Blogger.