MOURINHO KUBURUZWA MAHAKAMANI.

MOURINHO KUBURUZWA MAHAKAMANI.

Unaambiwa hujafa hujaumbika, mbali na majanga yaliyomkuta  mourinho, lakini Bado Eva Carneiro ameamua kumbwaga Mourinho mahakamani. Ni baada ya kutibuana kwenye mazungumzo yaliyodumu kwa saa 2 hivi majuzi.
*******************************

Eva analalamikia  Constructive Dismissal na sex Discrimination. Yaani kutimuliwa bila kufuata taaratabu za kisheria na unyanyasaji wa kijinsia. Kesi hii ipo kwa Jaji Wa mahakama ya South Employment Tribunal kule Croydon london, hizi ni mahakama maalamu za ajira!
*****************************

Chelsea hivi majuzi walipewa muda wa kujibu tuhuma za Eva ambayo ndio siku hiyo hiyo Mourinho alipotimuliwa! Kumbe chini ya kapeti  huyu dokta hakulipwa fidia yake yote. Mkasa ulianza mwezi wa 8 tarehe 8 pale Mganga mkuu wa timu bwana John Fearn na mwanadada huyu kutumia muda mwingi kumuuguza Hazard ambaye alionekana hajapata majeraha makubwa huku timu ikiwa inahitaji ushindi.
************************

Mimi nmesoma kidogo kuhusu sheria za ajira/kazi, kwanza kuna kitu kinaitwa utu wa mwajiriwa, mwajiri ana jukumu la kulinda utu wako na siokumdhalilishaji, kwa hapa kwa Mourinho alikosea sana hasa yeye kama mwajiri wa Eva. kwa sababu pale mwajiriwa wako anapokosea lazima unamfata yeye mwenyewe na kumweleza kuhusu alichokifanya mkishindwana ndipo unakuja kwenye umati na kulielezea hilo.
*******************************

Kosa la Mourinho ni kuja kwenye mkutano wa waandishi wa habari na kumsema vibaya yule mwanadada. Mwanamama Hearther Rabbats ndiye anaongoza uchunguzi huu chini ya FA na amekiri kumtetea Eva kwa udhalilishaji wa namna ile.
****************************

Chini ya Kapeti pia kuna taarifa kuwa klabu ya Charlton ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili dokta huyu.
*****************************

Mbali na hayo Nachoshangaa kwanini timu ilipobeba ubingwa hiki kitu hakikuwepo? Lakini mara baada ya kuanza kupoteana kelele zilimwendea Eva? Maana uchunguzi wa FA unaonesha mara kwa mara mourinho amekuwa akitumia lugha chafu na ya matusi kwa mwanadada huyu.
*****************************

Taarifa pia zinasema Mourinho anapaswa kupeleka vielelezo vya ushahidii mbele ya mahakama hiyo akishindwa basi atalipa ada ya E1000 na atabidi amlipe Eva maelfu ya pesa kama atashindwa kesi hiyo kwa mantiki hiyo chelsea haitahusika hapo. Lakini kwa upande mwingine chelsea itapaswa kumlipa malipo kama Posho kwa kuwa nae alichangia mafanikio ya chelsea akiwa ajirani.

No comments

Powered by Blogger.