MOURINHO KUIKABILI ARSENAL AKIWA NA MAN UTD

Na Priva ABIUD

Baada ya kichapo dhidi ya sunderland basi huend Louis Van Gaal akakabidhi mifuko kwa Jose Mourinho. Taarifa za ndani za Man United zinadai kuwa Mourinho atateuliwa kuwa kocha mkuu wa Man utd kabla ya mchezo wa ligi kuu unaofuata!


Mara baada ya mchezo dhidi ya Paka weusi hao Kocha mkuu wa Man united amedai kuwa kwa sasa Man utd ina nfsi ndogo kumaliza kwenye nafasi nne za juu. Zikiwa zimebaki mechi 12 ligi kuisha Mashetan wekundu wapo chini pointi 6 dhidi ya aliyeko namba 4.


Bodi ya Man utd haina cha kupoteza kumkabidhi Mourinho timu kabla hat ya mchezo wa tarehe 28 mwezi huu dhidi ya Arsenal. Kwenye mchezo wa Uropa Man utd itakutana na Midtjylland ya kutoka Denmark kisha Shrewsbury kwenye michuano ya FA.


No comments

Powered by Blogger.