ALIYESABABISHA BARCELONA KUFUNGIWA NAE ATUPEA MIAKA MINNE

ALIYESABABISHA BARCELONA KUFUNGIWA NAE ATUPWA NJE MIAKA MINNE.


Juzi Juzi nilizungumzia kuhusu Gabriel Jesus na Gabigol Barbosa kuwa moja kati ya vipaji murua kabisa siku za usoni. Mmoja tayari nyota yake ishaonekana bado kung'aa na amesajiliwa Man City. Miaka kadhaa nyuma Arsen wenger alikiinua kipaji cha Cesc fabregas na kumfanya moja ya viungo bora na tegemezi pale arsenal, ila Giovan Dos Santos alienda kupoteza kipaji chake galatasaray kabla ya kuja tottenham. Miaka ya 2000-2005 pale La masia palikuwa kipindi kizuri sana cha akina Messi, Pique, fabregas na dos Santos. Wote walifanikiwa isipokuwa tu huyu Dos santos ambaye uchaguzi wa klabu ya kwenda ulimponza. Alionekana kuwa moja ya wachezaji bora kabisa katika wakati ule na alitabiriwa kuwa Ronaldinho mpya.
*******************************


Allen akipasua msitu

Miaka takribani 10 imeisha hakuna anaeumuulizia Dos Santos.Biashara yake imeisha, lakini hivi majuzi Arsen Wenger amesafiri mpaka Japan kumwangalia Asano takuma. Nia yake ni kufanya kile alichofa ya kwa fabregas, Nadhani amepatikana kwa ada ya E9.  Lakin Wenger huyu huyu alimkataa messi kwa kigezo kuwa alikuwa na umbo dogo. Leo kamfata takuma. Ila Wakati anamfuata takuma, kule spaini kuna bwana mdogo anaitwa Alen Halilovic. Dogo wa kutoka Crotia. Huyu bwana mdogo ni fundi aibu. Kuna wakati nasema Luiz Enrique hakuna kocha pale watu wanakataa. Enrique amekubali kuweka kipaji cha huyu bwana mdogo katika wakati mgumh kama Frank Rijkaard alivyoweka matatizon kipaji cha Giovan Dos Santos kwa kumpeleka Galatasaray, kwa kumpeleka huyu Halilovic Humberg SV. Niseme ya rohoni kama huyu dogo angekuwa Mspain leo hii wangekubali akaharibu maisha yake huko ujeruman? Leo hii Munir anapata namba Barca Halilovic anaachwa kwa E5. Unajua kwanini wenger hahaingiki tena na hawa watoto la masia? Tutaona mbele
*******************************

Najua wengi hatumfahamu Halilovic.


Huyu kijana alipiga sana mpira mwingi pale la liga. Ni zao la la dynamo zagreb  ingawa hajacheza mchezo hata mmoja mmoja wa ligi na Barcelona. Wakati akiwa Sporting Gijon kwa mkopo, huyu Messi mdogo aliwaokoa hawa Asturian wasishuke daraja. Huyu dogo aliongoza kwa kukokota mpira kwa mara 81 ukiacha neymar 143 na Mess 117 la liga nzima. Alitengeneza nafasi za magoli 26 alitengeneza magoli matano na kufunga magoli matatu akiwa na miaka yake 20 huku akiwa kwenye timu iliyokuwa ikipambana kutokushuka daraja.
****************************


Akiwa na zlatan

Lakini bado naona Barca wanamtega maana wameweka kipengele cha kumsajili tena kwa kiwango kisichozid E12. Huenda Wenger ambaye anapenda vipaji changa alimwona lakini hivi vipengele vya barca vya kinafiki vimemkumubusha kuhusu Cesc fabregas. Amini naawaambia huyu ndiye atakaekuja kuivaa jezi namba kumi kama ataweza kujitoa kwenye hii kesi aliyobambikiziwa ya kwenda Humberg ili kukuza makali yake zaid. Barca wanatabia moja ya kijinga kweli. Yaani wakikuona wewe ni mzuri na huwezi kupata namba kwa wakati huo wanakupeleka gerezani kwa muda. Kumbuka Pique kumbuka Jord alba kumbuka fabregas, kisha kama utafanikiwa basi wanakurudisha kambini. Wanachofanya wanaweka mkataba wa kununua tena kwa bei fulani. Hii inawapa ahueni na nakuondoa fedheha kubwa kama waliyoipata Man utd kwa Paul Pogba
*****************************!


Hapo juu nimemwita Messi mdogo, mtu anaweza kuniona chizi, ila ndio hivo. Huyu bwana mdogo akiwa na miaka 16 na siku 100 kabla hajaja catalan alikuwa kule Dynamo Zagreb ambako ndiko alikoanzia, katika umri huo alikuwa mchezaji wa kwanza kucheza mechi akiwa na Umri mdogo katika historia ya Zagreb na Istoshe alifunga goli katika umri huo tena goli alilofunga kwa dakika 10 za mwisho alizoingia  tu na kuwa mchezaji mdogo kuwahi kufunga katika historia ya ligi hiyo. Alivunja rekodi ya Bwana mdogo Matteo kovacic ambaye kwa sasa anakipigia Real Madrid. Istoshe mwezi wa 11 mwaka 2012 alifunga goli lake la pili ambalo pasi alipewa na matteo kovacic goli zuri kabisa alipiga shuti nje ya box. Kwenye mechi ya Uefa alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya PSG akiingia kumpokea Kovacic na kuwa mchezaji mdogo kabisa wa pili kucheza michuano ya UEFA. Barcelona walimnunua kwa mkataba wa miaka mitano kwa ada ya E2.2 akiwa na miaka 17.
****************************


Akiwa na Lionel Messi

Barcelona wa walifungiwa kusajili kwa kitendo cha kumsajili halilovic ambaye alikuwa hajafikisha miaka 18. Na alicheza mchezo mmoja tu kwenye mchezo wa copa de la rey. Aliichezea crotia katika umri wa miaka 16 na kuwa mchezaji mdogo kuwahi kuichezea Crotia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ureno. Baba yake mzee sejad aliwahi pia kuichezea Dynamo Dynamo Zagreb, ila kuna tetesi kuwa baada ya kuhamia barcelona  familia yake yote ilihamia maeneo ya mjini wa barcelona sasa sijui alipoenda humberg na familia.imefuata nyuma ama lah lakini mdogo wake yupo timu ya watoto ya la masia kwa sasa. Katika michezo 106 aliyocheza amaefunga magoli 26. Sizungumzii umri ila naangalia uwezo wake wa kukimbia na mpira , mwepesi , anapiga mashuti yani ukimwangalia ni kama unamwangalia Modric mwenye umessi ndani yake.. kila la kheri allen.


Akiwa na wachezaji kikos cha kwanza cha Barcelona


No comments

Powered by Blogger.