CONTE, OSCAR HAJAVAA NDALA YUPO PEKU USIMTUME VICHAKANI
CONTE, OSCAR HAJAVAA NDALA YUPO PEKU USIMTUME VICHAKANI.
Antonio Conte naweza kumuita mpenda matokeo. Yaani yeye anayatamani zaid matokeo kuliko kuwaza zaid plan zamatokeo. Wakati wa mechi yake dhidi ya West ham, dakika za mwisho alionekana kucheza mfumo wa mwaka 1958 kipindi brazil wana zagallo, Pele , vava na Garincha mbele wote wakiwa washambuliaji, pale kati kulikuwako na vipande viwili vya wanyakyusa Didi na Zito. Dakika kama kumi za mwisho Conte alijaribu huu mfumo baada ya kumtoa Hazard, willian na Oscar kisha akawaleta Mosses, Batshuayi na Pedro! Kwa mantiki hiyo alitumia 4 2 4. Kimsingi ni kama alicheza kamari na alishinda maana pasi ilitoka kwa Batshuayi kisha kwa Costa na akamkimbiza Conte aliyeshangilia kama amejibiwa meseji na mtoto wa Obama.
******************************************
Oscar ni kiungo mzuri mchezeshaji zaidi kuliko kutengeneza. Au wengine wanapenda kuwatumia watu kama (Of the shoulder) kama unawakumbuka watu kama akina Davor Suker, yaani washambuliaji nusu, kazi yao ni kumsaidia Poacher kama akin dvid trezeguet n.k, ila sasa Oscar alisimama nyuma ya Costa haku akiwa na jukumu la kukabia timu juu na dimba la kati, hivyo hakuwa na jukumu la kushmbulia zaidi. Oscar sio Poacher wala mshambuliaji. Kila mtu alimwona Oscar kama amepotea, ila shida oscar alicheza jukumu gumu. Unaweza ukashangaa kwanini nasema hivi lakini Oscar alicheza jukum alilopaswa kucheza namba 8 ambaye ni matic, kiuhalisia ni kama Matic hakuwa uwanjani kwa sababu shughuli yote Oscar alishaimaliza.
******************************************
Mfumo wa 5 3 2 1 ambayo ni sawa na 3 1 4 3 unaonekana haumfai pale EpL. Ila huu mfumo unatumiika kwenye baadhi tu ya nafasi za huu mfumo, kwa mfano, Akiwa Italy alikuwa na wanamieleka watatu Chielin Bonucci na Bazargli, ila kwa bahati mbaya chelsea ana waendesha boda boda wawili ( aplicueta na Ivanovic) na wakata mkaa wawili Terry na Cahil. Hivyo ameonelea hawa waendesha boda boda watumike zaidi kupeleka mkaa na toyo zao (spidi/kupanda na kushuka) kwa sababu wanapumzi na kasi. Kweli azpilicueta aliwapa penati chelsea alipoangushwa kwenye box! Kumbe mfumo wa kutumia mabeki kama mawinga bado umemfaa! Kwa upande mwingine, Wakati Italy akitumia traquatista mmoja ambaye ni De rossi hapa chelsea kaweka wawili badala ya mmoja Kante na Matic ili kuziba nafasi wanazoacha hawa waendesha boda boda pindi wakipanda! Kwa hapa nampa tano!
***************************************
Shida ipo kwa Oscar na Fabregas! Mchezo wa juzi Oscar ametumika sehemu ambayo alipaswa atumike Hazard lakini kwa jukumu tofauti. Kwanza Oscar sio kiungo wa Kati (CM) ila ni kiungo wa kati mshambuliaji (CAM). Amemtumia Oscar kama alivyokuwa amemtumia Eder kwenye michuano ya Yuro! Shida ya hili eneo ni kuwa mchezaji lazima aendane na mfumo wa gegen (mfumo wa klopp) yaani dakika 90 mchezaji unakimbia tu muda wote! Hii aina ya mfumo ulimkiimbiza Arda turan pale atletico. Madhara yake ni kuwa inamfanya mchezaji acheze au aonekane kama amevaa ndala kama huyo mchezaji hana nguvu, pumzi na kasi ya kutosha! Huyu mchezaji wengine wanamuita Box to Box! Yaani wewe sio namba 10 sio namba 8 na wala sio 6 ila wewe unaitwa Mad Dog uwanjani yaani mbwa chizi. Unapokuwa na kiungo wa aina hii basi sio lazima uweke tena viungo wakabaji wawili, haina maana yoyote maana mshambuliaji wa mwisho atakosa patna. Chelsea naweza kusema walipata ushindi finyu kwenye iliyocheza ovyo kabisa. West ham walidefend sana, Conte dakika za mwisho ndipo anashtuka hilo anaamua kuondoa viungo na kuweka washambuliaji. Kama angeenza hivi tokea mwanzo basi magoli yangekuwa mengi tu, HIVYO ASIMPE OSCAR JUKUMU HILO AMPE HAZARD AU FABREGAS, oscar mpeleke pemben au mwache akae dimba la kati awe mchezeshaji tu hayo mengine utamchoma miiba tu.
*****************************************
Binafsi sikuona sababu ya kumtumia oscar vile kwa sababu tayari Matic, na kante walikuwepo ndani. Nafasi aliyocheza Oscar ingemfaa zaidi Fabregas ili kumlisha Costa na kupress timu pinzani iwaze zaidi kuclear mipira, au angeenda eneo husika hazard ili aendeshe timu, atengeneze nafasi zaid na kufunga pia. Kwasababu tayari alishamweka Kante ndani tayari timu ilishatulia kilichobaki ni kutengeneza nafasi kuliko kusubiri zaidi matokeo kwa kufosi washambuliaji wanne dakika za lala salama. Labda ametumia mfumo huu kwa sababu alicheza na timu dhaifu au alitaka kujenga imani na hazard anayetokea pembeni kuliko hazard huru. Ila kwa muonekano tu Conte atakuwa tishio zaid kama atampa uhuru Hazard kuliko kumtegemea Costa. Naiona chelsea tishio kubwa sana hasa kwa mfumo huu huu wa 4 2 3 1, endapo viungo wa kati watacheza diamond style yaani kiungo mshambuliaji yaani namba kumi acheze nyuma au hatua kadhaa kutoka langoni ili kuleta upinzani mkubwa kwa Libero na Namba 5 na kumpa nguvu namba 9 yao. Mimi sio mtaalamu wa soka lakini soka ni mchezo wa macho! Makosa na mipango vinaonekana kwa macho ya kawaida. Kila la kheri Conte

Leave a Comment