FIFA NA TFF KAZI YENU NINI? JE NYIE NI VIBARAKA?

FIFA NA TFF KAZI YENU NI NINI?

Naombeni kidogo leo, nizungumzie kila ninachokiamini, hivi kuna mahusiano gani kati ya TFF na TAKUKURU? FBI na KAMATI YA MAADILLI YA FIFA? Je hizi zote ni taasisi za Kiserikali? Zinaongozwa na aina gani ya sheria? Je sheria za binafsi (Private laws)? Au Public Laws (sheria za kiserikali)?  TAKUKURU wanafanya kazi kwa asasi zipi? Za kiserikali au za binafs? Je TFF inafanya kazi kwa niaba ya FIFA au serikali? Je viongozi wa TFF ni waajiriwa wa serikali au wapo chini ya muundo wa FIFA.
***************************************





Napata mkanganyiko kidogo! Naomba nitumie elimu ndogo tu ya kisiasa na elimu ya kiuwekezaji, kama mnakumbuka vizuri, mwaka jana kama sikosei, kuliletwa hati maalumu ya makubaliano ya kimkataba baina ya PPTL na TANESCO kwenye Bunge letu, kuhusu suala la kutokupelekana kwenye Mahakama ispokuwa tu mahakama za usuluhishi za kibiashara pekee yake! Juzi Juzi mnamo mwaka 2014 tarehe 8 mwezi wa 10, blatter sepp na plattin Michael walipewa adhabu ya siku 90 na kamati ya maadili ya fifa. Mnamo 1/9/2016 blatter na wenzake walifungiwa miaka 8 na kamati ya maadili ya FIFA kujihusisha na soka kwa vitendo vya rushwa na uhujumu.
*****************************************

Huko ujeruman, waziri wa Haki, Bwana Heiko Maas aliomba wale wote waliohusika na Rushwa wakamatwe mara moja, kisha akaongeza kuwa FIFA haipo juu ya sheria, hivyo serikali itawakamata wahusika na kuwatia nguvuni. Hapa sasa napata mkanganyiko, juu ya nguvu ya FIFA na sheria za nchi, na juu ya nani mwenye mamlaka katika ofisi za fifa na tff. David cameroon mwenyewe waziri mkuu wa England alimtuhumu sana blatter na alimwambia aachie ngazi mara moja kwa tuhumu za Rushwa.
**************************************

Marekani amekuwa mstari wa mbele kuchunguza masuala ya RUSHWA kuzidi hata FIFA yenyewe! Wametumia FBI na baadhi ya mawakala wao kukamlisha chunguzi zao. Kitendo hiki nacho kimehamia Tanzania. Juzi Raisi wa Simba kakamatwa na TAKUKURU kwa kile kilichodaiwa ni rushwa. Swali ni Je, TFF walishachunguza hilo? Je TfF si ina kamati yake ya maadili? Je kamati ya maadili ilifanya uchunguzi? Kwa serikali inaingia taasisi binafsi ghafla bila kuzipa muda taasisi husika muda wa kutafakuri hilo jambo?
****************************************


Mwisho wa haya ni nini? Nini kazi ya TfF? Nini kazi ya FIFA, ? Zipo mahakama za michezo kama Court of arbitration for Sports (usuluhishi wa kimichezo) kwanini wasipelekwe kwanza huko? Nafahamu sana umihumu wa serikali kupambana na Rushwa na nafahamu, jukumu kubwa la serikali, lakini pia serikali inapaswa kuwa na mipaka na viwango vyake vya kiutendaji. Hizi zote ni taasisi huru, zinapaswa zifanye kazi kwa uhuru wao, serikali inapaswa kuingilia tu, hasa pale patakapoonekana kana kwamba kuna uvunjivu wa haki za binadamu, au ukiukwaji wa sheria za nchi. wapeni TFF uwezo wa kuamua mambo yao, wape TFF mahakama zao za kimichezo, serikali ikiingilia kila kitu kutaondoa uhuru wa hizi taasisi. FIFA imebaki kama mbwa mbwekaji tu. Kila kitu marekani ameingilia kuanzia ngazi ya taifa, kimataifa na hata nje ya mipaka yao....ni mtazamo wangu tu.


No comments

Powered by Blogger.