GUARDIOLA HATA LISSU AWE WAKILI WAKO HII KESI ITAKUSHINDA
Kijiweni Kwetu
GUARDIOLA HATA LISSU AWE WAKILI WAKO HII KESI HUWEZI SHINDA
Na Priva Abiud
Naam.. msimu wa EPL unakaribia kuanza matumbo yaliyowengi hasa hasa majirani zangu yamejaa joto. Wapo wanapagawa na ujio wa Pep Guardiola wapo wanaotokwa mapovu na usajili wa Pogba na wengine wanahaha kutokana na klabu zao kutosajili majina makubwa. Msimu huu kutataliwa na Uzoefu, uwezo na umakini. Msimu wa mwaka jana palitaliwa na Bahati, uzembe na udhaifu wa timu kubwa
××××××××**×*×*×*×*×*×*×*×*×*×*
Nafasi nne za juu zipo wazi kwa timu tatu tu kwa mtazamo wangu. Arsenal, Man United na chelsea.. nafasi moja nazipa timu tatu liverpool Tottenham na Man city. Huwa nachokiamin mimi ni kuwa kusajili wachezaji wengi sio kupata mafanikio kirahisi. Pep amesajili wachezaji wakawaida sana woteee afadhali hata Ilkay Gundogan ingawa nae alikaa msimu mmoja benchi. Pep guardiola anakuja kujaribu ligi England anakuja kujaribu mfumo n.k,,,, nataka nimpe salamu kuwa babu yake alipita asubuhi pakiwa hapana jua na pakamchosha je yeye ataliweza jua hili la mchana kweli? Hapa namzungumzia Loius Van Gaal alikuja ligi ikiwa imepoa, ligi ilikuwa inatawaliwa na Potchettino, Ranieri hadi West ham nao walikuwa timu ya kuogopeka.. LVG alikuja msimu chelsea ni wabovu n.k...
*×*×*×*×*×*×*×*×*×!×!×*×*×*×*×*
Wengi tunamdharau Wenger, lakini huwa mimi nikitaka kuisoma ligi naiangalia sura ya Wenger Pale anapoulizwa maswal kuhusu usajili.. ukiona pua ya wenger ni nyekundu akihaha kununua wachezaji jua huo msimu sio wa kubet. Msimu huu wenger amerelax sana. Sio kwamba hana hela,, kwa taarifa yako Arsenal ndiyo inaongoza kwa kuwa na hazina kubwa msimu huu. Wenger atabak nafasi tatu za juu tena ikiwezekana ya Pili. Ana uzoefu mkubwa na majira ya ligi na anajivijua viwanja vingi zaidi. Rahisi kwake kupata matokeo mazuri. Klopp tayari nae ashajua njia ya bar tayari nae ni mlevi hawez kupotea njia maana tayari ashakuwa mzoefu anajua ni kiwanja kipi nisiende kichwa kichwa na wapi nitumie akili. Conte anakuja na mfumo pendwa na wenye mafanikio zaid EPL defencive oriented, hakuna mabadiliko makubwa chelsea. Wachezaji woteee wana uzoefu na EPL na wamekwisha iviana tayari Conte yupo hatua mbili mbele ya Guardiola.
*×*×*×*×*×*×*×*×*×*×*×*×*×*×*×*
Jose mourinho siwezi kumzungumzia sana maana kila kitu kipo wazi kuhusiana na uwezo wake na uzoefu wa ligi alionao. Tayari ameshajeng hofu kwa majirani. Alichobakiza ni kubeba ubingwa tu. Hana cha kujitetea hata kidogo. Arsenal mpaka sasa namhakikishia nafasi ya pili, ndiye mtu sahihi wa kupambana na Mourinho. Klopp ana kazi ndogo tu ya kupambana na Guardiola maana wote wamesajili wachezaji wengi ambao sio wachezaji wakubwa na hawana uzoefu mkubwa na ligi ngumu hasa wakiwa kwenye klabu kubwa. Guardiola amemsajili Gabriel Jesus mchezaji mdogo kabisa ambaye ndo kwanza anachipukia nadhan ana msimu mmoja ndani ya Palmeiras, kamsajili Nolito nae ndo kwanza amepata namba timu ya taifa, kaja na Moreno achana na huyu Stones ambaye waingereza wamepata lulu, sina shida nae ila hawa wengine bado wanahitaji vichapo vingi ili wajue wapo EPL. Pep Guardiola ni kocha mkubwa na mwenye mafanikio na klabu kubwa. Alifanikiwa na.Barcelona kwa kuwa alikuwa pale pale barcelona na alikuwa anaifaham vizuri zaid la liga, tupilia mbali zawadi kubwa aliyopewa (messi) alipolekea Bundasliga pale ndipo tulipojua ukweli kuhusu Pep, kuwa Pep ni mwalimu mzuri ambaye wanafunzi wanamuelewa kwa urahisi zaid, tatizo ni kuwa mwalimu kama anafundisha vizuri lakini mtihani hatungi yeye wala hasahihishi yeye basi kazi ipo kwa wanafunzi. Wanafunzi wa Guardiola Pale Buyern walimuelewa vizuri lakini Mitihan ya UEFA walifeli. Buyern kufaulu mtihani wa Bundasliga kwao sio sifa, sifa ni kutwa UEFA. mwalimu Guardiola naamini ana mbinu nyingi kufundishia, lakini hizi mbinu haziwezi kufanya kazi ndani ya msimu Mmoja. Kama anabisha basi akamchukue Tundu Lissu aje amsaidie kwenye hii kesi akishinda naomba Wenger apigwe Risasi hadharani
Kwa Mantiki hiyo, nyie wapinzani (kwa sauti ya Mrema) arsenal sio timu ya kuibeza, guardiola ana kazi ya ziada klopp hana cha kujitetea msimu huu. Na pia leicester City atajitahidi kwa kiasi chake
UTABIRI WANGU
2.Arsenal
4.Man city/liverpool/tottenham
1.Man united
3.chelsea
5.Man city/liverpool/Leicester city
6. Leicester City/west ham/ tottenham
Kwanini nimeweka timu tatu katika hizi nafasi. Binafsi yangu nafasi ya 4, 5, 6 nmeziacha wazi kwa mtu yoyote yule.
Leave a Comment