MATUSI NI SIFA PALE OLD TRAFORD, MWAMBIENI FELLAIN

MIWANI YANGU.

Juzi wakati wa mchezo wa Man utd dhidi ya Hully City Maroune Fellain alionekana kumsaidia mwanamama mmoja aliyekwama miguu wakati mashabiki wa Man utd wakishangilia goli la usiku kabisa la Rashford. Fellain huyu misimu mitatu iliyopita hakuna shabiki wa united aliyekuwa tayari kumshika mkono? Fellain misimu mitatu iliyopita alikuwa mchezaji wa kuzomewa sana uwanjani. Hakuonekana kama fellain yule wa Everton. Maisha yanabadilika sana, wakati fella akizomewa Martial alikuwa Mussa wa wana wa israel ndani ya Old trafford. Leo nilisikiliza wimbo wa mwanamama mmoja anaitwa Mwaipopo unaimbwa anayekudharau atakusalimia kwa heshima..hii ni tofauti kwa Martial, Msimu huu martial amebakiza skendo na kutolewa kila dakika za 70 anapoonekana hana faida tena kwenye dakika zilizosalia, anaonekana kama ganda la ndizi, akiendelea kubakia uwanjan basi watakanyaga na kuanguka. kwenye soka kama hutumii nyakati zako vyema hakuna atakae kukumbuka labda ukishaondoka uwanjan au dunian. Juzi nilimsoma jamaa mmoja anaitwa ally mkame, anakwambia tunakosea heshima  messi ronaldo na bolt. Tunasifia waliokwisha ondoka uwanjan ambao hawajafanya haya waliofanya hawa watu, Yaan mtu anakwambia maradona ni bora muda wote lakini anajifanya haoni anayofanya messi na ronaldo. Tuna tabia ya kusifia kisichopo, tena kwa kujipiga kifua, mbaya zaid wengine hata hao pele na maradona hatukuwahi kuwaona.




Tuachane na hayo. Everton ilikuwa klabu ya kipekee na yenye mafanikio kwa fella. Klabu ambayo nilimsikia dr leakey akisema "moyes alikuwa anakabidhiwa E5 za usajili na anaambiwa, sitoke nafasi 7 za juu. Unajiuliza hiyo pesa atamnunua nayo nan? Mmoja wa wafalme waliomkomboa Moyes pale Godson Park ni Marouane  fellain. Msimu wa 2012 jamaa alimaliza msimu na magoli 13. Fellain aliweka rekodi ya mchezaji ghali kununuliwa Everton ya E15 nadhan huo msimu hakuna mwingine aliyesajiliwa? Ila hapa naona kama dr leakey alitudanganya.... na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka ubelgiji kununuliwa ghali kwa wakati huo. Ni mchezaji ambaye alitengeneza ufalme wake Everton. Huwa kuna wakati namkumbuka sana tony hibbert aliyecheza zaid ya mechi 260 bila kufunga goli lolote ndan ya everton. Yaani yeye hajawahi kabisa kufunga goli katika maisha yake ispokuwa tu mchezo wa kumbukumbu yake alipocheza dhidi ya AEk athens. Mbali na kutokufunga jamaa alikuwa ndiye mchezaji pendwa sana pale Everton na palikuwepo nA jukwaa lililokuwa limejaa mashabiki wake tu.

H


Fellain akiwa everton

ibbet hayupo tena uwanjan, lakini fellain ambaye alikuwa kipenzi cha wanaeverton bado yupo uwanjani, ila yupo kwenye ardhi ya laana, ardhi isiyokuthamini ukiwa chini. Old trafford ni kiwanda cha mashujaa, ni ngumu kwao kukutukuza ukiwa uwanjan kwa kipindi kirefu, pogba aliitwa na fergie mpuuzi leo zaid ya mashabiki million 500 wanaimba pogback, ukiondoka tu utasikia kejeli zao, eti tulikuwaga na Ronaldo na aliondoka sembuse di maria,? Tena watakwambia tuna pesa za kumtengeneza star mwingine kama wewe. Thamani ya fella imeonekana ndani ya mechi tatu. Ona wanavyomsifia? Fella alitukanwa miaka mitatu? Ona wamesahau kuwa walimwita mzigo? Mzembe? Mzitto? Manywele mengi hana akili? Hii ndio ardhi ya lawama na sifa! Ndani ya old trafford kupewa sifa hata kwa kucheza dakika kumi ni kawaida. Unaweza kucheza dakika saba na wakakuita pele mpya. Alikuja macheda... unamkumbuka? Aliyedanganywa na fergie kuwa atasomeshwa bure na familia yake kuhamishiwa England? Mchezo wa Aston villa ulimfanya aonekana dwight york ama andy cole mpya. Yuko wapi macheda? Yupo wapi falcao aliyevunja rekodi ya headlines kwenye google hata bila kutua ardhi ya England?


Van parsie kushoto kulia chicharito

Alikuja chicharito wakamwita Ruud Van mpya alipewa sifa zote leo chicha kapita kama upepo alikuja rvp dunia nzima ilisimama kwa miez nane pale rvp alivyoibeba united na kuipa ubingwa, ameondoka nan anamkumbuka? Ukumbukwe kisa magoli 20? Kisa kombe moja? Hapana aameondoka giggs juzi kwa kugoma ajira united, kila mtu anamnyooshea kidole kama msaliti. Hizi ni salam zangu kwa fella. Leo watakutuza kama wayahudi walivyompokea Yesu kule Yerusalemu. Jana tulimwita Martial mkombozi leo tunamwona Yuda. Maisha yakibadilika ndani ya Old trafford uwe na uhakika wa njia mbadala. Naombeni mumwambien fellain kuwa ahakikishe anakamia hivo hivo hadi msimu unaisha, afahamu fika benchi yupo herrera carrick na morgan. Juzi mourinho kasema Bastian kurudi uwanjan ni ngumu, hajasema kama haiwezekan inawezekana lakini ni ngumu. Aliyeonekana kuwa mzgo anamweka benchi mchezaji bora kabisa wa kizazi cha wajerumani kwa sasa. Hizi ni salamu ila ninae msalimia hanisikii sio mbaya mashabiki wake wamezisikia salam

No comments

Powered by Blogger.