DORMUND BILA MKHTARYAN,GUNDOGAN NA HUMMELS HAKUNA TATIZO
DORTMUND BILA MIKH,IKAY NA HUMMELS HAKUNA TATIZO
Kiu yangu
Na Patrick Admila
Ni rahisi kusema kwamba dormund hata wakiondokewa na wachezaji muhimu(key players) bado wanaweza kukabiliana bila shida, BvB09 wanajua namna ya kuziba pengo la mchezaji yeyote anayeondoka klabuni kwao na hasa mahasimu wao wakubwa Bayern munich ndo wamekuwa kama wanategemea kizaz cha BvB.
Wakat naona henrikh mkhtayan,gundogan na mats Hummel's wanaondoka nilijua BVB watapata shida sana kufanya replacement za hao wachezaji,,wakwanza ni mkhtaryan alifunga magoli 23 na kutoa pass za mabao 32 katika msimu wa 2015/2016, Unapoondokewa na mchezaji kama mikh lazma uumize kichwa, Pia ameondoka mshindi wa kombe la dunia 2014 mats Hummel's tena kwa mahasimu wao wakubwa the bavarian na pia ameondoka kiungo Ikay gundogan na kujiunga na Manchester city inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza,Ikay ni Bonge la midfielder anajua kupiga pass ni aina ya viungo kama kiungo wa zaman wa Fcb Xavi Hernandez tatzo la Ikay ni mchezaji wa majeruhi sana na unaweza kuona city imepata kiungo mzuri sana lakn tatzo majeruh ya mara kwa mara,hakuwa muhimu sana msimu uliopita katka kikosi cha kocha Tomas tuchel wa BvB kutokana na kukumbwa na majeruhi.
Dortmund baada ya kuwapoteza wachezaji wao muhimu walichofanya ni kumrudisha tena Mario Gotze amabaye awali alisajiliwa na Bayern munich misimu mitatu ya nyuma,,Gotze kabla hajasajiliwa na Bayern alikuwa amefunga magoli 22 na kuhusika katika magoli 24 katika misimu yake mitatu iliyokuwa imepita,,Pia wamemsajili kiungo mshambuliaji Andrei Schurrle kutoka Wolfsburg ya ujeruman,,Lengo la Tomas tuchel ilikuwa kujaribu kuziba pengo la Henrikh mkhtayan aliyejiunga na Manchester utd,,Aliamini kwamba Gotze pekee yake hawez kuleta pass nying za mabao pia kuna majeruhi ambayo yanaweza kutokea na kuigharimu team, na pia Gotze na Schurrle wana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi nyingi uwanjani maana wote ni viungo washambuliaji na wana kasi ya kushambulia,,Pia Thomas Tuchel alihitaj depth yan awe na kikos kipana,kumbuka wakat anawaleta schurrle na Gotze walikuwepo wengne wakali kama Marco Reus na Shinji kagawa na bila kumsahau Pierre Aubermeyang,,
Nafas ya Gundogan amesajiliwa Sebastian rode kutoka Bayern na pia nafas ya Hummel's akasajiliwa Mare batra na Tuchel hakuishia hapo Alimuongeza mshindi wa Uefa Euro 2016 ambaye beki wa kushoto anaitwa Rafael Guarreiro na pia wakamleta kinda mwingne Osmane Dembele na Emre mor ili kuhakikisha akina gundogan na mkhtaryan wanasahaulika haraka sana,Mpaka hapo unaweza kuona kweli BvB wana team ya kushindana,na hasa kwa upande wa safu ya ushambuliaji kocha Tom tuchel anaumiza kichwa kutokana na kuwa na aina ya wachezaji wanaofanana yan style ya kucheza
Lakin pamoja na hayo nawapongeza BvB kwa kufanya usajili wa maana baada ya kuondokewa na wachezaji muhimu maana misimu ya nyuma walikuwa wakiuza wanabaki hivyo hivyo mwisho wa siku soka la bundesliga likatawaliwa na Bayern munich ambayo kila msimu inachukua ubingwa na huwa inatangaza zikiwa zimebaki mechi nying za kucheza,inaonyesha kuwa ligi haina ushindani na Bayern wao siku hizi wananunua hawategemei makinda kama ilivyokuwa kwa BVB,, Mpira wa sasa ni biashara,usiponunua unaishia kusindikiza tu,, Nawapongeza Bvb kwa kuliona hilo na wamesajili na wao,Sio kila msimu wao wanakuwa wanyonge kwa Bayern, Nataka kuona Borrussia Dortmund inatwaa ubingwa wa Bundesliga maana inachosha kuona kila msimu team moja ndo inatetea ubingwa wake, hata hivyo sio Bvb tu ndo iwape changamoto Bayern hata team zingne zilete changamoto,wawekezaji wakiongezeka katika ligi kuu ya Ujeruman bas tutaona ushindani mkubwa sana,, hatutaki kuona ligi inayotabilika kila msimu,watu washindane
Mtazamo tu
Leave a Comment