ORODHA YA WANACHEZAJI WANAONGOZA KWA MISHAHARA MIKUBWA TANZANIA
Wachezaji 10 wanaolipwa mishahara mikubwa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017
10 . Vicent – Simba SC (milioni 2.1 za Kitanzania )
Vincent Atchouailou de Paul Angban , Kipa wa simba raia wa Ivory Coast ambaye aliwahi kudakia timu ya vijana ya Chelsea chini ya umri wa mika 21 kama mchezaji asiye na mkataba ambaye amepita miaka 21 anakula dola 1000 za kimarekani sawa na milioni 2.1 za kitanzania
9 . Juuko Murshid – Simba SC (milioni 3.2 za Kitanzania )
Juuko Murshid , Beki wa kimataifa wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda , The Cranes aliyeisaidia taifa lake la Uganda kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani nchini Gabon baada ya miaka 38 anakula milioni 3.2 kila mwezi akiwa na wekundu wa msimbazi
8 . Laudit Mavugo – Simba SC (milioni 4.3 za Kitanzania )
Baada ya Mohamed Dewji kuichangia Simba milioni 100 , klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi haikufikiria matumizi ya pesa hiyo na moja kwa moojakuamua kumshusha mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo. Mavugo anakula mshahara wa Dola za kimarekani 2000 sawa na milioni 4.3 za kitanzania
7.
John Bocco adebayor
John Bocco – Azam FC (milioni 5 za Kitanzania )
John Bocco ‘Adebayor’ , mchezaji aliyeipandisha Azam FC ligi kuu Tanzania bara Julai 27, 2008 anakila sababu ya kuvuta milioni 5 za kitanzania kila mwisho wa mwezi .
6. Vicent Bossou – Yanga (milioni 7.6 za Kitanzania )
Beki wa Yanga, Vicent Bossou alijiunga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara akitokea Goyang Hi FC ya Korea Kusini ambapo hivi sasa kila mwisho wa mwezi anakula milioni 7.6 .
5. Haruna Niyonzima – Yanga (milioni 7.6 za Kitanzania )
Kiungo huyu wa kimataifa wa Rwanda anaekipa katika klabu ya Dar Es Salaam Young African (Yanga) Haruna Niyonzima naye anavuta takribani milioni 7.6 kwa mwezi.
Haruna Niyonzima
4. Amissi Tambwe – Yanga (milioni 7.6 za Tanzania)
Mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita , Amissi Tambwe alitua Yanga akitokea simba majira ya saa sita usiku wakati dirisha la usajili likielekewa kufunngwa . Tambwe , raia wa Burundi naye anaingiza milioni 7.6 za kitanzania kwa mwezi .
3. Donald Ngoma – Yanga (milioni 7.6 za Tanzania)
Aliyekua mshambuliaji tegemeo wa FC Platinum, Donald Ngoma alitua kwa vigogo wa Tanzania, Yanga SC kwa usajili wa Dola za kimarekani 50,000. Ngoma anaingiza milioni 7.6 mwisho wa mwezi
2. Obrey Chirwa – Yanga (milioni 10 za Tanzania)
mshambuliaji wa zamani wa FC Platinum , raia wa Zambia , Obrey Chirwa alitua Yanga kwa dau la dola 100000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 za kitanzania . Chirwa anaingiza milioni 10 kila mwezi .
Serge wawa wa azam
1 . Serge Wawa (Milioni 15 Za Tanzania)
Beki wa kati wa Azam FC, Muivory Coast , akiwa na umri wa miaka 30Serge Wawa anakama mpunga mrefu kuliko mshahara anaopata rais wa sasa wa Tanzania , John Pombe Magufuri anayeingiza milioni 9 . 5 kwa mwezi . Wawa anakamatia dola za kimarekani elfu 7 sawa na milioni 15 za kitanzania .
Source bongosoka.com
Leave a Comment