SWALI NI JE NGASSA YUPO SAHIHI

NGASSA YUPO SAHIHI KUUVUNJA MKATABA WAKE NA FREE STATE STARS...

Akiwa katika ile timu ni vyombo vichache sana vya habari vilikuwa vikifatilia habari zake . Ripoti nyingi zilikuwa sikisikika wakati akiwa likizo nyumbani.

Toka ametua kwenye timu ile hajawa na wakati mzuri kwa sababu mbalimbali ambazo ndizo zimemfanya juzi kabla ya dirisha la usajili kufungwa kuamua kuvunja mkataba na timu hiyo.

Kiasilia Ngassa ni kiungo mshambuliaji kati au pembeni. Ana uwezo mkubwa sana kuzitendea haki nafasi hizo na kuifanya safu ya ushambuliaji kuwa moto muda wote au kumsimamisha kama kiungo wa juu lakini asiye na majukumu ya kukaba zaidi ya kutawanya mipira . Hili huwezekana akiwa na back up nzuri ya compact defensive midfielder.

Free State Stars walikuwa wakimpanga kama kiungo mkabaji . Yaani anarudi chini kama mkabaji . Nilishituka sana nilipoliona hili . Nikajisemea moyoni maisha ya msukuma huyu yanahesabika pale Bondeni.

Ngassa si kiraka kukupa nafasi ya kumtumia nafasi zote za kiungo . Kwanza kwa kimo chake ni ngumu kusimama pale kati kwa ligi yenye viungo na wachezaji mahili kama ile.

Ngassa anahitaji nafasi ili azipange hesabu zake vyema kufunga au kutoa pasi nzuri za mwisho.

Kupambana na msitu wa kati kulimfanya kiungo huyo kuumia goti na kabla ya hapo alionekana floppy sana na kukosa nafasi ya kuichezea timu hiyo.


Hapa ukitazama si kwamba Ngassa amekwisha bali mbinu za mwalimu, mifumo na falsafa zake zimekinzana na uwezo binafsi wa mchezaji huyu aliyepata kuwika na Young Africans , Simba SC na Azam FC bila kusahau kudumu na kikosi cha Taifa Stars kwa muda mrefu.

Bila kufanya utafiti tunaanza kumhukumu Ngassa kwamba hawezi kucheza nje na akili yake yote ipo Young Africans . Si kweli mambo mengine ni bahati na kudra za Mungu.

Wapo wachezaji mahiri waliwahi kutokea nchi hii lakini hata mkataba wa miezi miwili nje hawajawahi kuupata. Unaweza kuamini Lunyamila au kipa Mohamedi Mwameja walishindwa vipi kuwika na timu nje?!

Kulinda kipaji chake , heshima yake na kiu yake ya kucheza mpira Ngassa imemlazimu kufikia maamuzi hayo. Lakini pia nahisi kuna msukumo mkubwa wa kocha wa timu hiyo kumtaka mchezaji huyo kuvunja mkataba maana hakuwa kuvutiwa na kiwango cha mchezaji huyo.

Nimewaza tu...

Mmmm🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄👆🏾

Chanzo whatsapp


No comments

Powered by Blogger.