TFF ANDAENI KITU KAMA VILE NI CHA KESHO
TFF ANDAENI KITU KAMA VILE NI CHA KESHO
Kiu yangu
Na Patrick Admila
Mambo mazuri huwa hayataki haraka,hiki ndo kitu ambacho TFF wanashindwa kukielewa na kama wanashindwa kukielewa bas hata vilabu vyetu haviwez kuwa na mabadiliko.Unatakiwa uandae kitu kama vile ni cha kesho kumbe ni cha baada ya miaka kumi au kuminatano mpaka 20,Wenzetu wanajua namna ya kuwekeza na wanajali sana muda,wanaandaa kitu ambacho hawategemei kupata manufaa kesho,TFF wanatakiwa kuwekeza kwenye soka,na kabla ya kuwekeza lazma uwe na watu ambao wana wivu na maendeleo,Kama vilabu vikubwa vya simba na Yanga havina hata uwanja wa mazoez unategemea nini?
Labda niwaulize TFF hapa nchini Tanzania kuna shule ngapi za soka? kila mkoa una shule hata ya kulea vipaji vya soka?Au kuna watoto hata 1000 ambao wanalelewa kwa kufuata misingi ya soka? Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo au samaki mkunje angali mbichi ukimkunja akishakua atakusumbua vitu vingi hataelewa na hata wachezaji wetu ndivyo walivyo.Mtoto anaelewa zaid akiwa tangu mdogo ndomaana wenzetu wazungu wanawaandaa watoto wakiwa bado wadogo baada ya miaka 8 au 10 wanakuwa wameiva na hata wakiingia kwenye team za wakubwa wanakuwa wanaelewa vitu vingi labda mambo madogomadogo ndo wanarekebishwa maana hawawez kukumbuka kila kitu.Kitu hiki hakipo hapa nchini,Soka letu halina mipango ambayo ni Progressive yan Endelevu,
Kama Ndani ya TFF kuna uozo mkubwa je kwenye vilabu kuna nini? Vilabu viko chini ya TFF ambao ndo shirikisho la mpira Tanzania,
Kama team ya Taifa inakosa mwelekeo basi hata vilabu haviwez kuwa na mwelekeo,Kama Team ya taifa inashindwa kufuzu hata kombe la Afrika au inafuzu halafu mapema inatolewa bas hata vilabu vitaishia kushiriki tu na team yetu ya taifa itakuwa inafanya kaz ya kushiriki tu sio kushindana.Usipojiandaa mapema na kuwa na mikakati basi kila siku ni malumbano,majungu na mambo mengne mengi na bila kupata viongoz ambao wanaweza kufikiria Tanzania imekwama wapi kisoka na kufikikiria nni kifanyike hatutapiga hatua,wakati nikifikiria haya yafanyike huwa najiuliza nin zaid ambacho Tanzania imefanikiwa ukiachana na soka?
Leave a Comment