WENGER ATAADHIMISHA MIAKA YAKE 20 KWA FURAHA?
WENGER ATAADHIMISHA MIAKA YAKE 20 KWA FURAHA?
Na Admila Patrick
Ndilo swali ambalo sio mashabiki tu ambao wanajiuliza au wachambuzi wa soka ila hata mzee wenger ndo linamhusu hasa maana kufundisha klabu kwa miaka 20 sio rahisi ukilinganisha na maisha ya soka yalivyo sasa ni wachache sana waliofanikiwa kufika na kuandika historia katika klabu.Manager wa zaman wa Manchester united amefanikiwa tena amepita hiyo miaka anayoadhimisha wenger hapo kesho, haijalishi umefanikiwa kiasi gani ila ni namna ulivyoweza kuiongoza klabu na kuipa mafanikio japo sio kila msimu, ni heshima kubwa kwa namna moja ama nyingne na hata ukiondoka unaacha historia ya aina yake ambayo sio rahisi kuvunjwa na mtu mwingne,Unaweza kuona mfano tangu Sir Alex Ferguson alipoamua kustaafu na tangu apo ni unaweza kuona ni makocha wangapi waliokuja na kuondoka tena wengne wameondoka hata mkataba hawajamaliza.Sio tu kwamba wenger hajashinda mataji mengi kama Sir Alex ila wenger amehakikisha ameiwekea guarrante Arsenal kumaliza katika nafasi za juu yani top four na huwa wenger hatumii pesa nying kusajili ila uzoefu wake na uwezo wa kuibua vipaji unamsaidia sana wenger,
Wenger alianza kuiongoza Arsenal tangu mwaka 1996 na kesho ataingia katika uwanja wa Emirates kuivaa chelsea na moja ya kitu kitakachompa wenger nguvu ni the fact kwamba yupo emirates mbele ya mashabiki wake, Ni mechi ya Inayozikutanisha team kutoka mji mmoja wa London,ni London derby itakayochezwa kesho majira ya saa 1:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.Japokuwa rekod inaibeba sana chelsea kumharibia wenger adhimisho lake ila huwa kuna wakati tunasema rekord haichez uwanjan,mpira ndo unachezwa na mpira ni mchezo wa makosa ukikosea kidogo unafungwa,Binafsi nngependa wenger aadhimishe kwa furaha yan awafunge chelsea asiwe mnyonge kwa chelsea tena,Kingne kitakachompa wenger nguvu ni kukosekana kwa Jose mourinho,Jose mourinho na Wenger ni mahasimu ambao wamekuwa wakionyesha hisia zao kila wanapokutana na mourinho amekuwa akiibuka mbabe mara nying.Chelsea ina manager mpya Antonio Conte ambaye ndo kwanza anakutana na wenger na anachotakiwa kufanya yy ni kuendelea kuweka rekord yani aifunge Arsenal.
Kukosekana kwa mourinho katika hiyo derby kunapoteza radha ya mchezo wenyewe ila tutarajie mchezo wenye kusisimua hisia za mashabiki ulimwenguni kote,
Leave a Comment