WACHEZAJI WA MANCHESTER UTD BADO HAWAELEWI ANACHOKIHITAJI MOURINHO

WACHEZAJI WA MAN UTD BADO HAWAELEWI ANACHOKIHITAJI MOURINHO

Na Admila Patrick
Wakati natazama pambano kati ya man utd na Liverpool jumatatu iliyopita katika uwanja wa anfield kuna kitu nilikiona na hata baada ya mechi kumalizika binafsi matokeo hayakunishangaza,,Jose alienda anfield huku amewambia wachezaji wake wacheze kwa kujilinda zaid na sio kushambulia na wasicheze kama liverpool,,Mourinho alifanikiwa kuondoka na point pale anfield na ndicho alichokiamin kwamba kitatokea,Unajua kwanin matokeo yalikuwa vile,, Jibu ni rahisi tu kwamba liverpool  ya kloop haina wachezaji ambao wanatumia nguvu nyingi,Can,henderson,lallana,firmino,coutinho,Sturridge, ni wepes sana na wanawaza kushambulia na hata kocha wao anaamin hivyo,hivyo ukiwatibulia mara nying na kutumia nguvu bas unawakatisha tamaa.


Nikirudi kwenye mchezo wa jana kati ya Chelsea na Man utd,Mourinho hakuelewa ni opponent au mpinzani gani anaenda kukutana nae,Wachezaji wa man utd walio wengi hawana akili ya kujinda,Herrera sio kiungo mkabaji halisia,,Pogba sio kiungo mkabaji,Fellain sio kiungo mchezeshaji na wala sio mkabaji ,Mourinho analazimisha wachezaji wake wamuelewe haraka kitu ambacho hakiwezekan kwa haraka yan itachukua muda mrefu, Felllain hana speed ya kumzuia ngolo kante wala matic, Ngolo kante na matic wote wanakaba na wana nguvu, na pia wana speed,,Hawa ndio waliharibu kila kitu, Mourinho hana wachezaji wa aina hii,Man utd haina kiungo mkabaji halisia kama morgan schneiderlin,Herrera analazimishwa tu ila sio nafasi yake, hata carrick sio kiungo mkabaji maana hana speed, Carrick unampenda akiwa na mpira anajua wapi aupeleke tofaut na fellain,Sifa  kubwa ya kiungo mkabaji lazma awe na nguvu na speed,,

Angalia chelsea wana hazard,mozes, willian,Pedro,, Man utd wana mata,martial,rashford,lingard,depay,mkhtaryan,hawa wachezaji  wa man utd hawawez kushambulia halafu warudi kukaba kwa haraka,unakuwa unawatesa tu,kwanza hawana nguvu wao wanatumia akili,Sio kama hazard,willian na mozes,ndio maana mfumo wa Conte wa 3-4-3 umewaingia haraka akilini wachezaji wa chelsea na wameuzoea kwa haraka kwa sababu wachezaji waliopo,Unahitaji wachezaji wa pembeni wenye nguvu na speed, Ni wachezaji wachache ambao mourinho anategemea walinde na kushambulia,Ndiomaana huwez kuwalaumu wachezaji wa manchester utd, Tatzo ni falsafa za kocha Jose mourinho,Mourinho hana aina ya wachezaji anaoamin wanaweza kuzielewa falsafa zake kwa haraka,

Kuibadilisha akili ya mtu sio rahisi lazma ichukue muda mrefu, Martial,mkhtaryan,mata,rashford,depay wote wanawaza wakipata mpira bas ni kushambulia tu,na huwez kuwalaumu ndivyo walivyo,Mchezaji anayeonekana anazielewa haraka falsafa za mourinho ni Antonio Valencia na Baily,hawa wote. Wana nguvu na wana speed, Herrera ameonekana anaweza kuzielewa falsafa za mourinho lakin bado akikutana na viungo kama wa tottenham na Chelsea bado atachemka tu kwasababu hana nguvu, Angalau ukimchezesha yy pamoja na Carrick au Schneiderlin team inaonekana ina balance na iko imara,Bado mourinho ana kazi kubwa ya kufanya, Kazi aliyonayo ni kuwafanya wachezaji wake wazielewe falsafa zake kwa haraka vingnevyo anaweza kuwa na maisha mafupi sana Old trafford,


No comments

Powered by Blogger.