ROONEY NI KITABU CHA KICHINA WATU HAWAKIELEWI
ROONEY
NI KITABU CHA KICHINA WATU HAWAKIELEWI
Mashabiki
wa Man Utd wakati msimu unaanza zlatan alionekana kama shujaa mpya aliyetokea
kuokoa kizazi cha historia kilichobakia akilini mwa kila mshabiki wa Man Utd.
Baadae kidogo zlatan huyu huyu alianza kutukanwa na kuonekana hafai, kidogo
wakahamia kwa Rooney, wakasema kachoka, kidogo faraja ikarudi kwa goli
alilofunga Paul Pogba hivi majuzi. Walio weng nadhani hawajajua hasa ni kitu
gani kinaisibu Man Utd. Wapo ambao tayari wameshakata tamaa na Jose Mourinho,
wengine wanasema mpira wake ni mbovu n.k

****************************************************************************
Binafsi
natamani kuona Wayne Rooney akiongezea mkataba wa miaka mingine kama mitano na
mshahara mnono. Najua unaweza ukashangaa kwamba rooney huyu huyu ambaye hata
kurusha mpira hawezi. Ndio rooney Huyu huyu wanaemnyooshea kidole. Man utd ya
sasa sio kama ya zamani, hii ni Man Utd ambayo mchezaji anaelipiwa zaidi ya
170,000 yupo benchi, man utd ambayo
wachezaji wenye thamani zaid ya milion 100 wapo benchi, morgan E32, mikhitaryan
E30, Memphis E28 na luke shaw E30. Haikuwahi kutokea katika historia ya Man Utd
wachezaji wenye thaman kubwa kias hicho kukaa benchi wakisubiri mchezaji
anaelipwa 70,000 kwa wiki Lingaard, na 37,000 rashford wachoke, tena wengine
wakisubiri mchezaji wa Bure zlatani atoke ili wao wapate nafasi.
******************************************************************************
Wakati
huo huo Mchezaji aliyeonesha kiwango bora sana msimu uliopita ndugu Martial
msimu huu akiwa katika msimu mbovu kabisa kumzidi hata oliver Giroud
tunaemdharau kila kukicha. Unapoizungumzia Man Utd huzungumzii, mchezaji wa
ghali duniani, huzungumzii mchezaji mwenye maudambwidambwi, huzungumzii, kikosi
cha gharama, huzungumzii matumizi makubwa ya fedha, kama huamini nitajie kikosi
Ferguson alichobeba nacho ubingwa msimu wake wa mwisho 2012? Katikati alikuwa
na Daren fletcher, alikuwepo cleverly Tom, alikuwa hadi na akina Darren Gibson,
pembeni butner alikuwa anampokea Evra, kule Evansi, hapa Oshea, mbele
walimtegemea welbeck achana na Van Parsie, alikuja hadi bwana mdogo macheda.
Yaani ukilinganisha kikosi ch sasa na cha nyuma ni aibu kubwa na fedheha kwa
Jose Mourinho.
******************************************************************************
Leo
hii Old Trafford sio machinjio tena, bali pamegeuka pango la wahuni, United
imekuwa na Mastaa wengi waakubwa na wenye viwango vya hali ya juu lakini hadi
Burnley nae kajipatia point old Trafford. Asilimia 80 ya wachezaji wa Man utd
kwa sasa hawajui nini maana ya wimbo wa GGMU (glory glory Man Utd. Wapo
waliokuja kukuza majina (depay) wapo waliokuja kwa sababu waliwekea mishahara
mikubwa (shaw, pogba, mikhitaryan} na pia wapo waliokuja kupokea penshen
(zlatan na Bastian)
*******************************************************************
Utagundua ile hari ya upamabanaji wa man utd
imepungua. Shida kubwa mashabiki wa Man utd wanadhani ni kana kwamba Mourinho
hafai sijui anapaki basi n.k sio kweli, fergie alikuwa anacheza soka gani la
kutisha? Cha ajabu kwa Fergie ilikuwa nini zaidi ya spirit? Wachezaji wa United
wamuige rooney watajua kwa nini katika umri wa miaka 30 rooney hawezi tena
kutoa pasi, watu wamesahau taulo la Vidic.
Akina
fletcher walikuwa kama vichaa uwanjan, muulize wenger alikuwa hawapendi akina
nani pale united kama sio Carrick na Fletcher, je carrick na fletcher mbali na
kuwa hawana ufundi lakini fabregas Rosicky na Nasri walikuwa hawapumui. Achana
na hao turudi miaka ya akina Roy kean? Roy kean alikuwa anaachiwa timu na
Fergie aongoze zoezi na kumpeleka majina ya kila anayefanya vizuri mazoezin, je
leo Mourinho atamwachia nani kama sio rooney?
Leave a Comment