MATCHDAY

Mechi kali ya Leo..
Manchester United vs Liverpool

Waswahili wanamsemo wao mmoja " baraza hukolea siku ya pili ikiwa mazungumzo yatarejelewa" na mimi ninaweza kusema utamu wa game ya Liverpool na Man United msimu huu ni game ya leo ..hii mechi ipo to tofauti na ile ya Kwanza(17 October ) ambayo ilionekena kuwa ni ya upande mmoja, kutokana na Liverpool kuwa kwenye kiwango bora ..
  kila mtu aliipa Liverpool asilimia nyingi za kushinda mchezo huo, Man utd walikuwa hawajakaa vizuri, kwani ilikuwa imetoka kufungwa na Watford pamoja na kutoa sare  nyumbani na stoke city..

Kwasasa unaweza kusema baraza limekolea wanaenda kukutana kwa mara ya pili tena ikiwa wote viwango vyao vipo vizuri...si rahisi kutoa utabiri wa haraka nani ataibuka mshindi..

#Muundo_wa_timu_zilivyo
Unapozungumzia United ya sasa..  Unazungumzia timu iliyokamilisha michezo 15 mashindano yote bila kufungwa, inaonekana Mourinho ametibu kiasi tatizo lililokuwa linaisumbua Manchester United, na hii ni baada ya kuanza kumchezesha #Mkhy.
United ilikuwa na tatizo la finishing tu.. mpira walikuwa wanaucheza vizuri sana na nafasi za mabao walikuwa wanatengeneza nyingi sana tatizo lilikuwa ni hilo tu!!!..
Japo saivi United inaonekana kukaa vizuri lakini tatizo la finishing bado lipo... Nafasi wanazozipata ni tofauti na wanazofunga..
Leo wanaenda kukutana na Liverpool ambayo washambuliaji wake ni  hatari sana .. Liverpool huwa inakasi kuanzia eneo la kati yaani kwa Henderson kisha timu huwa ikifanyiwa mipango zaidi mpira  unapopelekwa kwa Coutinho,felmino na lalana..
Hawa ni watu ambao kwenye nafasi tano wanakufunga 3 ni tofauti na united inayoonekana kukosa huduma hiyo..

Tatizo la Liverpool ni moja tu hawana beki Imara pamoja na kipa bora, yaani kwa ufupi eneo la Liverpool la nyuma sio zuri ... hili ni tatizo kubwa kwenye Ligi na mechi ya leo kwa ujumla... huwezi kufanya mashabulizi matatu ya nguvu kwa beki hizi za Liverpool ukakosa kupata bao mbili.. 
Hii ni hatari kubwa sana kwa Liverpool inayokutana na Man United yenye washambuliaji wenye nguvu na kasi kisha ni mafundi..

#Eneo_la_kati
Msingi wa timu zote hizi mbili  kwasasa unaonekana kupewa uhai mkubwa eneo la kati .. japo United inaonekana muda mwingine kumtumia zaidi vallencia kufanya mashabulizi kwa kupitia pembeni..
Nadhani eneo la kati ni kama wachezaji wa timu zote mbili wanafanana ...Manchester United wana Pogba,Herrera na Carrick kisha Liverpool wana Henderson,Lallana na wajnadum, Nadhani hili eneo ndio litakalo fanya mshindi apatikane...
Kwaupande wa man United hili eneo ndilo litakalo push mashabulizi na kusaidi kiasi eneo la nyuma ambalo kimsingi linaonekana kuimalika sana kwasasa.
Ili Liverpool isiruhusu mashambulizi mengi kwa beki zake hili eneo ndio  litakuwa na kazi hiyo  aidha kukaa sana na mpira muda mwingi au kucheza wakiwa deep zaidi ..Ili Man United wasipate nafasi kubwa ya kushambulia muda mwingi..

Nadhani mechi ya leo itaamuliwa na  makocha yaani Klopp na Mourinho

Tusubili..

#by Nasri Van Man Utd


No comments

Powered by Blogger.