HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO

USIKUBALI KUPITWA NA HIZI ZA KIMICHEZO LEO
4.3.2017
Baadhi zinazohusu michezo
1. Chelsea yaitoa  Manchester United baada ya kuifunga 1-0 na kutinga nusu fainali ya FA. goli hilo pekee kafunga Ngolo Kante dk ya 51. Hata hivyo United walilazimika kucheza pungufu tangu dk ya 35 kufuatia kadi nyekundu kwa Ander Herrera.

2. Nusu fainali ya kwanza Chelsea na Tottenham April 22

3. Nusu fainali ya pili Arsenal na man City, April 23

4. Nani kakudanganya Yanga wanaenda Zambia kwa treni? Wanaondoka kwa ndege alhamis hii.

5. Wadau waipongeza Azam kwa ushindi dhidi ya Mbabane, wengi waitaka ikapambane zaidi, inaondoka kesho

6. Kocha Salum Mayanga aanika kikosi cha Taifa stars. Wamo Manula, Dida, Nduda, Kapombe, Kessy, Zimbwe Jr, Gadiel Michael, Salim Mbonde, Nyoni, Dante, Banda, Mkude, Muzamiru, Ndemla, Kichuya, Msuva, Ajib, sure boy, Himid Mao, Kabunda, Samata, Ulimwengu, Farid, Mbaraka Yusuph na Abdulahman Musa.


7. Blagnon adaiwa kukosa hati ya uamisho wa kimataifa (ITC). sasa atarejea Simba

8. Simba yatua Arusha. Inajiaandaa na madini FC jumapili kunako  robo fainali ya FA jumapili.

9. Kiafrika
-Durban  yapokwa uenyeji wa jumuiya ya madola 2022. Chanzo chatajwa kutothibitisha usalama wakati wa michuano hiyo lakin pia maandalizi duni

-Mohammed Diame wa Sénégal na Newcastle atangaza kustaafu kuitumikia timu ya Taifa. Asema kwasasa kuna nyota 23 zaidi yake Sénégal. Washabiki wamjia juu. Ana miaka 29

-Mali hatarini kufungiwa na FIFA, ni baada ya serikali kuingilia michezo kwa kuwatimua maofisa wa shirikisho la soka la nchi hiyo.

-Zanzibar kupigiwa kura ya kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la soka barani África, Caf, alhamis hii. Inahitajika 2/3 ya kura

-Siku hiyo pia kutafanyika Uchaguzi wa kumpata Raisi wa Shirikisho hilo. Raisi wa Shirikisho hilo tangu 1992 Issa Hayatou anachuana na Ahmad Ahmad wa Madagascar.

10. Kona ya Vijineno
- Raisi wa TFF Jamal Malinz asema atapiga kura ya kumchagua raisi wa shirikisho la oka Afrika si kwa maslahi yake bali kwa maslahi ya taifa.

-Ngoma aitamân Simba. Sio Ngoma Donald, ni Ngoma kiungo wa Zanaco 😃😃

-Mourinho asema mpk watapopata meneja atayewapa mataji manne ya EPL ndipo takuwa namba  2, kaongeza kwa sasa atabaki namb moja ni baada ya kuzomewa na washabiki wa Chelsea


11. Nyinginezo
-Fernando Torres arejea mazoezini huenda akaivaa Bayer Leverkusen kesho
-Donald Ngoma kuikosa Zanaco
-UEFA kuendelea leo na kesho
-Leo kuna Juventus na Porto, lakin pia kuna Leicester na sevilla
-kesho Monaco na man city, lakin pua Atlético madrid na Bayer Leverkusen
-UEROPA wiki hii si jumatano ni alhamis baadhi ya mechi ni man utd na Rostov, Genk na Gent

Ni hayo kwasasa SOURCE whatsapp by pallangyo


No comments

Powered by Blogger.