NAJUA HATUELEWI KIARABU,
XAVI ALITUTUKANA LAKINI ANAWAELEWA WAARABU, TUMPE NAFASI TUMSIKILIZE
Na Priva, ABIUD
“………..huyu bwana mdogo
kimuonekano ana manywele kama ya fellain kwa mbali, anapenda kutumia mguu wa
kushoto, ana uwezo mkubwa wa kupiga mipira ya (curve) wabongo tunaitwa ndizi,
anajua kutengeneza sana magoli kwa utaalamu wake wa kupiga pasi za kukata na
kuchopu na pasi ya kupitilizisha katikati ya mabeki au mipira ya kuzungusha.
Kwa mfano mwaka 2013 aliweka rekodi ya kutengeneza magoli 23 kwenye michuano
yote ikiwa ni pamoja na kutengeneza magoli 17 kwenye ligi kuu Saudia, pia
alitajwa kuwa mtengenzaji magoli bora kwa mismu miwili mfululizo 2013 na 2014……….”
“……….Huwa najiuza sana,
sisi waafrika tupo busy na nini? Kwasababu mchezaji chipukizi kwetu ni Yule
mwenye miaka 25. Waraabu inajulikana wazi kuwa wapo bize na mambo mengi,
wachimbe mafuta, wauze, starehe na mengineyo, sisi kazi yetu kubwa ni kilimo tu
sasa tunakosa vipi muda wakuwainua vijana wadogo tunasubiri mpaka tuje tuwaone
umiseta? Kwanini tusiwachukue wakiwa UMITASHUMTA?...........”
*********************************************************************
Unapoangalia maisha ya
Lionel Messi nyuma yake palikuwa na kikundi kikubwa cha watu. Messi
hajafanikiwa tu kwa juhudi zake binafsi, ingawa Ronaldinho aliwahi kutamka
kuwa, hajawahi kumfundisha lionel messi kitu chochote ila lionel messi
alijifunza mwenyewe baadhi ya vitu kutoka kwa watu mbalimbali na yeye akiwepo.
Nyuma ya messi palikuwepo na Bwana Rondell aliyekuwa mwalimu wa la Masia
kuanzia miaka ya 1990s mpaka 2000, wakati messi anijiunga pale akiwa na miaka
13, pia alikuwepo mtu ayeitwa Juan Laporta ambaye ndiye alikuwa raisi wa
Barcelona kwa wakati ule ambaye alionekana kuipenda zaid la masia kuliko
kununua wachezaji kutoka nje, kama vile Pique, Iniesta, fabregas, xavi na
Messi.
**************************************************************
Kule Riyadh Saud Arabia
mwaka 1999 kuna mtu anaitwa Abdulrahman Eissa, huyu wakati waarabu wenzie
wakichimba mafuta na kwenda maduka makubwa kuulizia Buggat Veyron 4, na Range
Rover sport, yeye alikuwa akipitapita kwenye mitaa ya familia za kati, siku
moja alipita kwenye viunga vya familia ya Hadhrami ambayo ni jamii ya
hadhramaut huko huko saud Arabia na alikutana na kijana Mmoja anaeitwa Omar
Abdulrahman (Ommy) ambaye ni kaka yake na akina ahmad, khaled na Mohamed. Bwana Eissa alimchukua dogo Ommy na kumpeleka
klabu ya El Malaz karibu na uwanja wa mtoto wa mfalme Faisal Bin Fahd ambapo
mtoto wa mfalme alishangaa sana kipaji cha mtoto huyo na kuuliza kuwa ancheza
klabu gani? Baadae alipata nafasi ya kuijunga na klabu ya Al hilal. Ingawa
hakuwa na utaifa kamili wa Saud Arab, yeye peke yake alipewa uraia wa nchi hiyo
na familia yake kutoswa kupewa uraia lakini baba yake mzazi mzee abdul alikataa
katakata akidai kuwa ni ubaguzi wa wazi na uonezi dhidi ya familia yake. Hapa
katikati wakati wa mzozo wa uraia kuna mtu mwingine alikuja akaongezeka katika
harakati za kumsaidia Ommy, nae anaitwa Al Garoon, ambaye ni rafiki wa Eisa nae
alipigiwa simu na Jamaa mmoja aliyekuwa akisaka vipaji vya soka, nae anaitwa
Nasser Bin Thaloub ambaye alitokea klabu ya al Ain, bwana esia alimpa habari
kuhusu Ommy kuwa ni kijana mzuri na mwenye uwezo wa kipekee. Hapo ilikuwa mnamo
mwaka 2000 na Kipindi hiki Messi alikuwa na Umri wa miaka 13, lakini kaka Ommy
alikuwa na Miaka 9 tu.
************************************************************************
Huwa najiuza sana, sisi
waafrika tupo busy na nini? Kwasababu mchezaji chipukizi kwetu ni Yule mwenye
miaka 25. Waraabu inajulikana wazi kuwa wapo bize na mambo mengi, wachimbe
mafuta, wauze, starehe na mengineyo, sisi kazi yetu kubwa ni kilimo tu sasa
tunakosa vipi muda wakuwainua vijana wadogo tunasubiri mpaka tuje tuwaone
umiseta? Kwanini tusiwachukue wakiwa UMITASHUMTA? Yaani unangoja mpaka anafikia
TUSA (michuano ya Vyuo Vikuu) ndo mnaanza kusema Yule kijana anakipaji. Kwenye
Maisha ya Ommy hapo tumekwisha ona zaid ya watu watatu wanajaribu kuinua kipaji
chake akiwa na miaka 9 tu. Mtoto wa kitanzania akiwa na miaka mitano wazazi
wanamnunulia mpira mlaini, akifikisha miaka 7 akionekana anacheza mpira, huo
mpira unatupwa mabatini au kuchomwa na wazazi wake wazazi hapa wanasahau kama
waliwahi kuwanunulia mpira, akiwa na miaka 11 kuendelea akionekana anacheza
mpira mzazi atamwita tu makusudi ampe kazi nyingine ilimradi tu asicheze mpira.
Huyu huyu kijana mwenye dhamira ya kweli na soka akifikisha miaka 18 bado
anakomaa na mpira wazazi wataanza kumlaumu kumpa maonyo kuwa asichezee elimu, yaani lawama kibao kuhakikisha tu
anasoma na sivinginevyo. Basi asipofaulu elimu zaid ya hapo akicheza mpira wa
mitaani ataonekana mvivu, mhuni n.k. huyu huyu kijana mpaka aje afikie malengo
yake ni miaka 25, hapo ndipo figisu inaanza, anabadili mwaka wa kuzaliwa ilia
apate nafasi ya kushiriki michuano ya madaraja ya chini, cocacola n.k ndiposa
apate nafasi ya kujiunga samba na yanga.
******************************************************************************
Wakati Rijkaard
anaongezeka kwenye listi ya watu waliomsaidia Lionel Messi anaamua kumpa nafasi
baada ya kushauriwa na mwalimu wake bwana Rondell, upande wa pili kule Uarabuni
nako tunaona mtu wa tano akiongezeka kwenye listi ya watu wanaomsaidia Ommy
kufikia mafanikio yake, nae ni kocha Winfred Schafer alipoamua kumpa ommy
nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza akiwa na miaka 16 tu. Messi huyu wa Asia
alifunga magoli 6 kwenye michezo 10 na kutengeneza mengine matatu. Kwenye
mchezo wake wa kwanza kwenye mechi za wakubwa alitengeneza goli pekee tena
aliingia uwanjan mnamo dakika ya 77 tu na kutengeneza goli hilo la pekee baada
ya kupiga shuti liliogonga mtambaa wa panya kabla ya Dias kuwapa Al ain
ushindi. Msimu wa 2009 aliweka kimyani magoli matano kwenye michezo saba, msimu
wa 2010 alifunga magoli 11 kwenye michezo 29 na kutengeneza magoli 8 ikiwa ni
msimu wake wa pili.
****************************************************************************
Baadae klabu ya Man
city walimchukua kwa majaribio, mtu wa 6 aliyeongezeka hapa ni mwalimu wa
kikosi cha watoto Man city bwana Brian Marwood aliyemfuata ommy mpaka falme za
kiarabu. Alipomkuta aliiomba klabu ya Al ain kumruhusu waondoke nae kwa
majaribio ya wiki mbili kwa makubaliano ya kumsajili kabla ya dirisha kufungwa.
Alifanya majaribio ambapo klabu ya Man city ilikubali kumpa mkataba. Lakini
shida ya vibali ya kazi pamoja na viwango vya FIFA vya taifa lake havikukidhi
kwa yeye kucheza ligi kuu England.
********************************************************************

Kwanini wanamwita
messi, huyu bwana mdogo kimuonekano ana manywele kama ya fellain kwa mbali,
anapenda kutumia mguu wa kushoto, ana uwezo mkubwa wa kupiga mipira ya (curve)
wabongo tunaitwa ndizi, anajua kutengeneza sana magoli kwa utaalamu wake wa
kupiga pasi za kukata na kuchopu na pasi ya kupitilizisha katikati ya mabeki au
mipira ya kuzungusha. Kwa mfano mwaka 2013 aliweka rekodi ya kutengeneza magoli
23 kwenye michuano yote ikiwa ni pamoja na kutengeneza magoli 17 kwenye ligi
kuu Saudia, pia alitajwa kuwa mtengenzaji magoli bora kwa misimu miwili
mfululizo 2013 na 2014. Anacheza kama kiungo wa pembeni anaetokea kushoto, pia
anaweza kucheza kama kiungo wa kati mshambuliaji. Ana uwezo mkubwa wa chenga,
mwepesi, anakasi, na mmoja wa wachezaji bora kutoka Asia kwa sasa. Tayari umri
wake umeenda kidogo sawa, akiwa na miaka 25 tayari ana mafanikio makubwa ndani
ya bara la Asia, lakini bado kwa aina yake ya uchezaji binafsi bado namwona ni
mchezaji bora ndani ya bara la Asia kwa wazawa.
Tayari ameisaidia klabu ya Al Ain kubebwa ubingwa wa ligi za kiarabu,
ubingwa wa ligi, super cup, kombe la Rais, na ubingwa wa AFC. Ametajwa kama mchezaji bora wa klabu mwaka
2008, na 2009, alitajwa pia kuwa mchezaji bora chipukizi 2009, 2010, mchezaji
bora wa mwaka kupitia Al Ahram 2010, mchezaji wa thamani kwenye michuano ya
ubingwa wa ligi za kiarabu mwaka 2010, mchezaji bora wa mashabiki kupitia AGL 2012, pia aliwahi kuwa mchezaji bora chipukizi
kupitia Al Hadath 2013, na mchezaji bora wa Emirate 2013. Mchezaji bora wa bara
ya Asia 2016, mchezaji bora wa ABA ligi kuu zote za Asia 2015,mchezaj bora
kupitia GSA, AFC 2016, al haram
mchezaji bora 2015/6 mchezaji bora wa Emirate kupitia AGL
kwa msimu wa 2014/15/16. Yaani ukiangalia vizuri hizi tuzo anatosha kabisa kuwa
mchezaji bora wa kiarabu kwa miaka ya hivi karibuni.
Huyu ndiye Messi wa Asia
na ndiye mshindi wa Mars D Or mchezaji bora wa kiarabu mwaka 2015. Ukitaka
kumjua tu wala usijipe tabu nenda youtube andika tu Omary Abdulrahman utamwona
na naamini utaamini yale niliyosema kwa Gabriel Jesus miaka miwilli iliyopita
hakika huyu nae akipata nafasi nyingine ndani ya ligi kuu Hispania kati ya
Barcelona au Madrid, au hata England ndani ya klabu kama Arsenal Na Liverpool
ambazo naona zinanendana na mfumo wake basi nae atamulikwa kama wanavyomuikwa
wengine.
*****************************************************************************
Makumpuni
kama AGL. AGC, AFC,
al harham, al hadaath, OSN, zimembeba sana kijana huyu kufikia hapo
alipofika,
lengo la makampuni haya ni kutanagaza lulu ambayo waarabu wanajivunia.
Je sisi
Tanzania ni makampuni mangapi yametoa nafasi kuwatangaza wachezaji wetu
kushinda tuzo mbalimbali ili kuwapa moyo wale wadogo kufikia malengo?
Kwa ufupi
tu huyu ndo Ommy wa kiarabu ambaye yeye ameona hakuna umuhim wa
kutojiunga na ISIS na kuamua kufurahisha watu kwenye tv. Lakini binafsi
naona Xavi amekuwa kama anatoa kashfa kwa Ronaldo kila kukicha, lakini
mnamo
mwaka 2015 alimsifia bwana mdogo Ommy na kusema anastahili kuja ulaya.
Ni wazi
kuwa aliona kipaji chake.
Neymar, luiz david, pamoja na zidane walimsifia sana
kijana huyu. Naweza pia kusema tunaweza kumweka kundi la akina Adnad Al
Taylani, na akina Ismail Matar. Xavi anasema hajawahi ona lulu kama ile, xavi
amekuwa akiimba sana kuhusu huyu mtu, lakini naona ni wakati wa xavi
kusikilizwa na yeye, juzijuzi nilibahatika kumsikia Leandro mshambualiaji
kibrazili anayekipiga Hyundai ya china, alisema, sijawahi kuona mwarabu kama
huyu, ni zaidi ya jini, huenda wazungu hawawaelewi watangazaji wa kiarabu, laiti
wangekuwa wanawaelewa wanavyomtangaza kumpamban ommy anapokuwa na mpira leo hii
asingekuwa uarabauni. Xavi amekaa uarabuni, hajui iarabu lakini anayoyaona huko
yana umuhimu mkubwa kwa soka la kiarabu hasa kwa ommy mwenyewe
Leave a Comment