Priva ABIUD.
kijiweni kwetu.
Hivi majuzi nimemsikia David
Trazeguet akimsihi sana Kylian Mbappe kuhusu uhamisho wake wa wapi pakwenda.
Man Utd imeonekana kutaka kumchukua kinda huyu wa Monaco aliyeanzia Maisha pale
yake pale AS Bondy ambako baba yake mzee Wilfred alikuwa kocha. Huyu kijana
alizaliwa mwaka 1998, lakini miaka 7 nyuma yake alizaliwa Antonio Griezmann. Wakati
luis Nan akijiunga Man Utd mwaka 2007 Mbappe alikuwa na 10 tu. Mbappe na Griezmann
wamezaliwa katika maisha mazuri ya kisoka maana wazazi wao wote walikuwa
makocha na walikuwa watu ambao walikuwa na uwezo wa kulisha familia yao. Wakati
Griezmann, Mbappe na Anthony Martial wakiwa na mazingira mazuri kimaisha
hii ilikuwa tofauti na Luis Nani.

Kwa kifupi kuna vitu vingi hawa vijana
wanapaswa kujifunza kwa luis Nani kwanza kabla ya wao kufanya maamuzi magumu
katika hatma yao ya kesho. Nmetangulia kumzungumzia David Trazeguet,
naamini wengi tunamkumbuka David hasa kwenye kombe la dunia la mwaka 2006 pale
alipokosa penati ya mwisho na Italia kutwaa kombe la dunia. David anasema kuwa mbappe
kwanza ni mdogo sana, hajafikia kiwango cha kuuzwa million 70. Amesema biashara
hizi huenda zikaharibu kiwango chake na kikapoteza maisha yake kwa ujumla. Amemsihi
sana kutokujiunga Man utd kwa sasa hata kidogo. trazeguet anadai kuwa, mbappe bado hana misuli ya kwenda kubeba mawe pale Old trafford, trazeguet anaamini Old trafford ni shamba ambalo ni gumu kwa Mbappe kuvuna kirahisi ikiwa ndo kwanza maisha yake yanaanza. Mbappe ameanzia maisha yake Monaco akiwa
na miaka 16 na siku 347 tu alicheza
mechi ya wakubwa akitokea benchi.

Wakati magazeti yakimtangaza
Mbappe na Martial wakiwa na miaka 15 tu, luis Nani katika umri huo yeye alikuwa
akipigana na Umasikini na maradhi. tumekuwa tunahisi kuwa kila mtu anayeishi ulaya basi wanatoka maisha mazuri. lakini amini usiamini kuna watu wanatoka maisha magumu ambayo wanakosa hata maji ya kunywa. kwenye umri wa miaka 18 Luis nani alikuwa akipokea kitita cha dola 10000 kwa mwezi. ukitazama kiwango hicho ni kidogo sana kwa Mbappe kwa sasa. kwa umri wa mbappe anahitajika kwa kiasi kikubwa cha hela kama million 70 maana yake mshahara wake hautakuwa chini ya dola laki 2 kwa wiki. ni tofauti sana ukifananisha na mshahara wa Luis Nani akiwa Lisbon.

Katika kijiji cha Santa Filomena kuliko
Lisbon huko ndiko alikokulia luis Nani. Katika mitaa ile kijana yoyote
aliyekuwa na umri wa miaka 15 alikuwa chokoraa au mwizi. Vijana wengi wa maneno
yale walikuwa na hati ya uhalifu wakiatafutwa na polisi kwa makosa mbalimbali ya
uhalifu. Nyumba ya akina luis Nani alikuwa na mlango wenye viraka na matundu
mengi huku baadhi ya maeneo ya nyumba yakifunikwa kwa Nyasi.
Katika umri huo wa
Luis Nani, mdogo wake Kylian Mbappe tayari Monaco washaanza kumnyemelea na
magazeti kibao yalishaanza kumpamba kwenye kurasa za mwanzo tu.

Baada ya Loius Nan kuhamia santa
filomena akitokea Cape Verde, shirika moja lililokuwa likisaidia watoto
waliokuwa wakiishi mazingira magumu walimchukua na kumpeleka shrikan kwao. Bwana
Alcides Mendes ndiye mtu wa kwanza kuona kipaji cha kijana huyu. Alimchukua Louis
Nani na kumpeleka shirikian hapo ili kumkwepusha na makundi ya kiuhalifu
yalikuwa yamekithiri mtaani kwao. Louis Nani anasema mara ya mwisho baba yake
mzee Domingos alirudi nyumban wakati wa sikukuu akiwa na miaka saba na hakuwahi
kurudi tena. Anaongeza pia mama yake Mama Maria do Ceu alikimbilia nchini uholanzi
luis akiwa na miaka 12. Maana yake luis nani aliishi kwa kipindi kirefu bila
wazazi. Louis Nani anakwambia nyumbani kwao walikuwa watoto 10, hivyo hakuweza
kukimbia familia baada ya wazazi wake kukimbia hivyo alibidi abaki santa
Filomena kwa shangazi yao huku akisema kuwa chumba kimoja walilala watoto 6. Akiwa
mdogo anakwambia kuwa alikuwa anadandia treni kwa nyuma ambayo ilikuwa inakwenda
kwa umbali wa maili 6 ambako ndipo alipokuwa akifanya mazoezi ya mpira katika
klabu ya Real Massama. katika klabu ya Massana anasema mara nyingi alichezea klabu ile kwa sababu alikuwa akipata chakula na baadhi ya mahitaji yake madogo madogo

Mendes anasema katika kipindi
chote hicho akiwa na kijana Yule, alisema kuwa ni mmoja kati ya vijana
waliokuwa hawakati tamaa.
Anasema kuwa
wakati Fulani alikuwa akipenda kucheza kwenye timu yenye wachezaji dhaifu ili
kila saa awe na mpira yeye na hata wakati mwingine ili ajipe majukumu makubwa
zaidi uwanjani.
Mendes anaongeza kuwa
ilikuwa ngumu sana kwa kijana kutoka kijiji kile na kwenda duniani akimaanisha ni
ngumu sana kwa kijana mdogo katika mazingira yale kufanikiwa kwa kiwango
alichofanikiwa Luis Nani.
Anasema alipigania
maisha yake pale ureno kwa sababu alikuwa Muafrika na alikuwa akibaguliwa sana
mpaka pale alipofikisha miaka 18 alipopata uraia wa Ureno. Mbali na soka Luis
Nan alikuwa nakwenda na kaka yake kwenye shughuli za ujenzi ili kujipatia kitu
kidogo cha kula na kulisha wadogo zao. tukiachana kidogo na Luis Nani, Mimi binafsi sina tatizo na Kylian Mbappe kwenda Man utd. Mimi pia naamini ndoto za mbappe ni kucheza klabu kubwa duniani kama Man Utd. Shida kubwa iliyopo katika timu kubwa kama hizo unaposajiliwa kwenye ile klabu ukibweteka kidogo unapotezwa. Klabu kubwa haziangalii maisha uliyotokea, haziangalii historia yako zinaangalia jitihada zako. Luis Nani hakwenda United kwa sababu alionewa huruma, ila alikwenda pale kwa sababu alionesha jitihada kubwa. anthony martail amekuwa na maisha magumu Old trafford. maisha magumu yalimfanya Luis Nani kujiamini na kujipa moyo kuwa ipo siku atakwenda duniani. aliamin kuwa ugumu wa maisha ungempeleka dunia. mbali na hapo bado alaimini kuwa Old Trafford itakuwa shamba lake na atapata yale alikuwa akihitaji wakati akiwa sanata filomena.

kwa Upande fulan ni kama vile Martial hajapata somo kutoka kwa Luis Nani kuwa na kiwango bora kabisa alipobweteka hakuna aliyemgeukia. martial amekuwa si na msimu mbaya tu pia amekuwa na migogoro ya chini kwa chini kama ule wa Luis Nani na Kocha wake mkuu bwana Alex ferguson. ila kwa mbali nmeanza kuielewa kauli ya Trazeguet, ni kama anamwambia Mbappe kuwa Martial ameonja kikombe alichoacha Nani. Mbappe huenda Martial nae akatoa somo kwake, na kama hatolielewa somo hili mapema basi atalielewa akiwa anaondoka Old trafford kama Depay. Umri wa mbappe ni mdogo sana kwa kiwango kile cha pesa, hastahili hata nusu ya pesa zile kwa umri wake. Old trafford ni uwanja wa vita, ni uwanja ambao ulimzawadia Nemanja Vidic mataulo mengi ya kufutia damu ilimradi tu kabati la timu likose vikombe. Vijana wengi hawajui Historia ya klabu ile hivyo wanaendeshwa na hisia za kwamba ipo siku watajengewa sanamu. kufanya waliyofanya akina Japp stam na akina Bobby Robbson huwezi ukawa unashinda saluni hata siku moja. Mbappe kama ataenda Man utd ajue fika kuwa anakwenda kwenye vita wala hakuna majaribio pale. ni uwanja ambao kila wikiendi unajaza wambea zaid ya 70,000 waliobeba mabango yenye historia za babu zake na baba zake wakiimbia GGMU. tuachane na Mbappe tuendelee na Luis Nani....

Ansema staili yake ya kushangilia kwa
sarakasi alijifunzia kwa wabrazili Fulani waliokuwa wakija shirikani wakijulikana
kama kundi Capoera. Loius nan anasema akiwa anashangilia vile huwa anakumbuka
sana maisha aliyotokea na anapenda kumkubuka dada yake wa kike aliyekuwa
akiipenda sana staili ile na aliyempa jina la utani. Maisha yake yalikuwa ya furaha
sana licha ya kuwa na njaa na umasikini uliokithiri mno. Anakumbuka
kuwa katika kipindi kile kazi yake nyingine kubwa ilikuwa wizi wa matunda
katika mashamba ya watu. Alikuwa akienda kwenye matukio mabaya na magumu lakini
aliukuwa akipata matokeo mazuri kwa familia yake. Anaongeza kuwa kaka
yake anayeitwa Paulo ndiye aliyekuwa nguzo muhimu katika maisha yake. Anaongeza kuwa kuna matukio
mabaya yaliyomfanya baba yake asirudi nyumbani. Anasema kuwa mwaka 2006
alikutana na baba yake, kisha baba yake alimweleza kuwa kwanini alikimbia Ureno. Wakati baba yake akimweleza hayo, Luis Nani uchungu ulimpata na
akamsihi baba yake kuwa hahitaji baba yake amuombe yeye msamaha kwa kuwa yeye ni mtoto wake na alimweleza
kuwa hana tatizo naye. Alikuwa na furaha kubwa kukutana na baba yake. Ni wanaume
wachache waliofanikiwa kwenye
maisha
wenye moyo kama Luis Nan hasa kwa kitendo cha baba yake kuitenga faimilia. Lakini yeye alimwelewa na alichukulia ni sehemu ya maisha na ni changanmoto tu
za kawaida. Mbappe
na martial wanapaswa kujifunza kuhusiana na ugumu wa maisha ya Nani
katika kuhakikisha kuwa wanafika mbali. Wao wamelelewa maisha
mazuri yasiyo na vikwazo na ikiwa walipata bahati ya kucheza klabu kubwa
mapema kabisa. wana nafasi kubwa ya kufanya makubwa, wanapaswa waone Old Trafford ni kama Santa Filomena. wanapaswa watafute mafanikio sio kwa kupenda pesa na sifa bali kwa kuweka jitihada nyingi na kwa kujiamini, kujituma na unyenyekevu mkubwa.

Wakati magazeti leo hii yanamtangaza Mbappe kuwa ndiye
Thiery Henry Mpya miaka yake luis Nan alikuwa akipambana na wahuni
mitaani. kwa
mtazamo wa haraka haraka utagundua utofauti wa maisha ya Santa Filomena
na kijiji cha Macon alichozaliwa Griezmann. kwanza wakati Luis Nani
akizaliwa katika adha zote hizo kule Cape Verde, Griezmann yeye
alizaliwa Hospitalini tena alizaliwa na meya wa mjini na mama yake
alikuwa mfanyakazi wa Hospitali. maisha yao ni tofauti kabisa. huenda hata Griezman akija Man Utd nae akabweteka, hivyo anapaswa ajifunze ugumu wa maisha ya Old trafford. leo hii mchezaji bora wa Ujeruman Henrik Mikhitaryan anateseka ndani ya ukumbi ule. vwanjan vya Old trafford au Santiago vipo mjini lakini maisha yake ni kama kijiji cha santa Filemona. sio sehemu ya Maonesho na pia sio sehemu ya kujifunza bali ni sehemu za vita.
Maisha ni kwenda mbele na kurudi ulipotoka, Baaada ya mafanikio makubwa luis
Nan anarudi kijijin Massama alikoanzia soka na kuwapa nguo pamoja na vyakula
mara kwa mara. Anakumbuka fadhila alizopewa wakati wa utoto wake hasa kwa
vyakula na nguo ikiwa ni kama fadhila. Luis nani anasema kipindi cha nyuma,
hakuwa na uwezo wa kununua nguo za mazoezini hakuwa na uwezo wa kununua nguo
nzuri, hivyo marafiki zake walikuwa wakimpa nguo zilizochakaa au nguo ambazo
zilikuwa hazitumiki. Wakati fulan marafiki zake walikuwa wakimwita nyumban kwao
ili wapumzike nae angalau wakati wa chakula aweze kushiriki nao msosi
kibongobongo hii tunaita kudoea msosi kwa jirani.

Mnamo mwezi wa 5 mwaka 2007,
Aurelio Perrera alipokea simu kutoka kwa Carlos Queiroz ambaye alikuwa rafiki
mkubwa wa Sir alex Ferguson na kocha msaidizi ndani ya Man utd. Queiroz alipata
taarifa kuhusu huyu kijana, hivyo walimbeba David Gill mpaka Lisbon. David Gill
alikuwa na wasiwasi kuhusu kijana Yule hasa suala la ada ya uhamisho. Carlos
alikuwa Hotelini huko Lisbon, na ni mzee mwenye miaka 64 ambaye kazi yake kubwa ni
kuibua viwango vya wachezaji wadogo huko huko Ureno. Huyu Carlos ndiye aliyeibua
vipaji vya Cristiano Ronaldo, Luis Figo, Paulo Futre, na Ricardo Quaresma.
Carlos alipoulizwa kama huyo kijana {luis Nani} ataweza kwenda Old Trafford
alishikwa na kigugumizi maana ilikuwa ni dili la takribani million 25. hapo juu nilisema kuwa kiwango cha pesa ambacho mbappe anahitajika nacho ni kikubwa mno, kiasi kwamba ukijaribu kuangalia kiwango alichonunuliwa nacho luis Nani pia kwa wakati ule ni kikubwa mno. Yapo mengi ya Mbappe kuulizwa kama alivyoulizwa Luis Nani kabla ya kusajiliwa. Nani aliulizwa je utaweza kuhimilia makelele na presha ya Old trafford? jibu lilikuwa ndiyo kwakuwa tayari alishajiamini. Luis Nani alitambua kuwa mlango wa Maisha yake umeonekana hakujalish kama akishapita ataufunga au atauacha wazi. Kuna mawili kwa Mbappe, kumsikiliza Trazeguet au kufumba macho kama Luis Nani kufungua mlango bila kujali atakachokutana nacho huko Duniani. Maisha ya luis nani Man utd hayakuwa maraisi hata kidogo, yalikuwa ni
maisha magumu yaliyojawa kelele za kila aina, sio kelele za wahuni, ni
kelele za wadau wa soka, mashabiki na waandishi wa habari. Baadae Carlos
alimhahakikishia david Gill kuwa ni kijana mzuri na mwenye uchu wa mafanikio.

Baadae luis Nani alifumba macho na akafungua mlango ambao aliamini ndiyo sehemu ya kuanzia maisha yake. David Gill alikamilisha dili la kijana huyo mwenye miaka 20. Hapo ndipo safari
ya duniani kwa Luis Nani ilipoanzia. tukirudi nyuma kidogo katika Maisha ya luis Nani pale Real
Massama, yalikuwa ya tabu sana, anasema moja ya vitu ambayo hawezi kusahau ni
kwamba siku moja walialikwa na klabu ya Benfica kwenye mechi ya kirafiki, kabla
hawajaingia uwanjan unajua
nini
kilichottokea?
Basi ungana nasi kwenye sehemu ya pili ya makala hii
Leave a Comment