…ETI ARSENAL NA MAN CITY AU LIVERPOOL HAZITASHIRIKI UEFA MWAKANI…
Priva ABIUD
kijiweni kwetu
Kuna watu
wameamua kuwa maafisa wa UEFA ghafla na wameanzisha sheria zao binafsi katika
kupanga timu ipi iende au isiende. Wametokea baadhi ya wachambuzi ambao wao
wanadai kuwa wanaijua sheria ya UEFA kuliko ilivyoandikwa kwenye sheria hizo. Huwa
najiuliza vigezo vipi hutumika ili mtu kuatafsiri maneno ya kiingereza na
kuyafanya ya Kiswahili? Yaani unahitaji nini ili uwe mtafsiri mzuri? Maana hawa
wachambuzi wamekuwa wakitafsiri makala za kiingereza huku wengi wao wakiwa
hawana ueledi mzuri wa lugha hivyo na wengi wao huishia kupotosha jamii. Samahan
kama nitakuwa nimekukwaza ila kama huna elimu yoyote kubwa ya lugha achana na
utafsiri na tafuta mhusika akusaidie ili kulinda uweledi wako katika kuchambua
kwako soka.
Ni kweli
kumekuwa na mabadiliko mbalimbali katika sheria mbalimbali za UEFA. Watu wanapaswa
kuelewa kuwa idadi ya timu zinazoshiriki UEFA huwa zinatofautina kila mwaka
kutokana na maendeleo ya kiuchumi katika kuendesha ligi mbalimbali, mabadiliko
ya washindi wa ligi ya mabingwa na ligi Uropa, pia baadhi ya mataifa kujiondoa
kwenye shirkisho la UEFA au baadhi ya nchi kujiunga katika shirkisho hilo. Kwa mfano
mwaka 2012 zilishiriki timu 75 kutoka mataifa 52, mwaka 2014-15 zilishiriki
timu 77 kutoka mataifa 53, ila kwa mwaka 2016-17 zilishiriki timu 78. Ingawa shirikisho
la UEFA linajumuisha mataifa 55, kwa mfano mwaka 2016 mataifa kama Kosovo na Liechtenstein
hayakushirki katika michuano hayo licha ya kuwa wanachama kutokana na kukosa
baadhi ya sifa zinatambulika na UEFA. Ili kushiriki michuano ya UEFa kuna
leseni huwa zinatolewa kwa kila taifa kulingana na hadhi ya ligi hiyo, pia
waangalia vitu kama viwanja na masuala yay a bajeti ya ligi hiyo n.k.

******************************************************************************
Sasa nataka
niwaeleze baadhi wachambuzi wakubwa ambao wamekuwa wakipotosha habari kuwa
nafasi ya 4 ligi England msimu huu hatoshiriki michuano ya UEFA kwa kigezo kuwa
endapo Man Utd itatwaa ubingwa wa UROPA watachukua nafasi ya mshindi wanne. Kwanza
hawa wachambuzi wanapaswa wajue kuna makundi makuu yaliyotengwa na UEFA
kulingana na alama mbalimbali, kuna kundi la kwanza ambalo linajumuisha nchi 3
{Uhispania, ujeruman na Uingereza} kundi hili linapeleka timu tatu moja kwa
moja katika makundi ya UEFA na mshindi wanne anaenda kucheza mtoano. Kuna kundi
la pili linajumuisha mataifa ambayo yanepeleka timu mbili moja kwa moja na
mshindi wa 3 ataingia kwa kucheza mtoano, kundi la tatu linajumuisha mataifa
ambayo yanapeleka timu moja huku mshindi wa pili ataenda cheza mtoano,na kundi
la mwisho ni lile linalopoleka timu mmoja tu. Mbali na hayo makundi sheria ya
UEFA pia imeweka nafasi za upendeleo kwa Bingwa wa UEFA na Bingwa wa UROPA
kuingia kwenye makundi moja kwa moja bila kucheza mtoano wala kuathiri idadi ya
timu zinazoingia UEFA kwa makundi tajwa hapo juu ispokuwa kuna baadhi ya
mazingira yatamfanya bingwa wa UROPA kucheza hatua ya mtoano na ntaelezea hapo
mbele.

KUFIKIA MWAKA 2013 KAMATI YA UEFA ILIKAA
RASMI NA KUFANYA MABADILIKO YAFUATAYO
1.
Iliongeza idadi ya mwisho kabisa ya timu kuingia
kwenye UEFA na kufikia idadi ya timu tano {maximum qualifications teams]. Hapo awali
ilikuwa timu . mabadiliko haya yalifanyika mwaka 2013 lakini yalianza kutumika
ramsi 2015-16.
2. Sheria pia iliweka vigezo kuwa bingwa UROPA atacheza
michuano ya mtoano endapo tu bingwa wa UEFA atatoka ligi moja sawa na bingwa wa
UROPA na mabingwa hao wote kushindwa kuingia UEFA kwa kumaliza nafasi ambazo
zinawaruhusu kupita kwa msimamo wa za ligi kulingana na makundi tajwa hapo juu
kwa mfano [kumaliza nje ya top four]. Mfano mwaka 2015, Barcelona alitwaa
ubingwa wa UEFA na sevilla kutwaa ubingwa wa UROPA, lakini Valencia alimaliza
nafasi ya 4 huku sevilla akimaliza nafasi ya 5, Valencia alingiaa uefa kwa
kucheza michezo ya mtoano lakini sevilla alipita moja kwa moja kwa kuwa alikuwa
mshindi wa UROPA na hakuathiri nafasi ya aliyekuwa mshindi wanne katika ligi.
3.
Idadi ya timu kuingia UEFA kwa kila ligi haiwezi
kuathiriwa hata kama Bingwa wa UEFA au UROPA watatoka nje ya nafasi za 4 za
juu. Sheria hii ni kwa mataifa yanayopeleka timu 4 tu ndiyo yenye sifa hiyo
yakupeleka timu tano UEFA na sio kwa mataifa mengine. Watu wengi wamechanganya
sheria hii na kipindi kile Chelsea alipotwaa ubingwa wa UEFA kisha akamaliza wa
6 na akashiriki UEFA na kumnyang’anya Tottenham Hotspur iliyomaliza ya 4 kwenye
msimamo wa ligi na kusukumwa UROPA. Baada ya malalamiko mengi dhidi ya sheria
ile iliyonekana kuzionena timu zinazomalzia nafasi ya 4, basi kamati kuu ya
UEFA ilikuja na sheria hii mpya ambayo ilikuwa lengo lake ni kuwabeba mabingwa
wa UEFA na UROPA bila kujali nafsi waliopo na pia bila kuathiri idadi ya timu
ambazo zinapaswa kushiriki UEFA ispokuwa kuwa tu zisizidi timu 5.
UTATA UMEKUJAJE?
Wachambuzi wengi wa soka najua wamesoma ile sheria ambayo inasomeka hivi
[winner of UEFA and UROPA each given additional entry if they do not qualify
for UEFA through their domestic league. “Because a maximum of 5 teams from one association
can enter to the champions league, if both the winner of UEFA and UROPA are
from the same top three ranked association and finish out of top four of their
domestic league the fourth placed team will be moved to Europa league” ]
Kwa akili ya haraka haraka wachambuzi wengi wamekimbilia kwenye neno “BOTH”
kwa uelewa wao wanadhani kuwa eti ili timu ziende tano lazima mabingwa hao
watoke ligi moja, hivyo wasipotoka ligi moja nafasi ya timu tano haipo. Naomba niwasaidie
kidogo na kiingereza changu cha shule ya kata chenye cheti original ni kwamba,
hapo walipoweka neno “BOTH” hawakumaanisha kuwa lazima mabingwa hao watoke ligi
moja la hasha, neno hilo limetumika kumaanisha kuwa kuwa ni lazima mabingwa hao
watoke kwenye {top three ranked association} yaani lazima watoke kwenye kundi
namba moja ambalo linapeleka timu 4 UEFA ili huyo wa UROPA apewe nafasi hiyo ziweze
kutimia timu 5.

Kama hamjaniliewa naomba mrudi tena kwenye makubaliano ya kamati ya UEFA ya mwaka 2013 juu ya sheria hii ambayo yanasema hivi “The previous limit of a maximum of four teams per association will be increased to five, meaning that if the Champions League title holders or the Europa League title holders are from the top three ranked associations (but not both from the same one) and finish outside the top four of their domestic league, the fourth-placed team of their association will not be prevented from participating in the tournament”

Leave a Comment