HABARI MOTOMOTO ZA MICHEZO, USAJILI MAJUU


16.5.2017


Kitaifa
1. Serengeti boys yaanza na sare Afcon. Yaibana Mali 0-0. Mali ndiye bingwa mtetezi.
-Hata hivyo serengeti inahitaji kuongeza jitihada kwani Angola Níger pia zilimaliza 2-2, zikiwa na faida ya sare ya magoli.

2. Mara Paap Zacharia Hanspope arejea Simba.
-asema wameyajenga na kwamba mpasuko kwasasa hauwajengi bali utasababisha Simba kukosa kila kitu. Wapanga kuonana na Mo Dewji. Simba itaikabili Mbao kunako fainali ya FA.

3. TFF yasisitiza uchaguzi Agosti 12, sifa zaanikwa. Kwa nafasi ya Uraisi TFF mgombea sharti awe na Degree na uzoefu ktk Uongozi. Imedokezwa kuna uwezekano mkubwa Raisi wa sasa Jamali malinzi akagombea tena.

4. Samata na Genk yake wakaribia kurejea Michuano ya Europa.

-Genk imeshinda Mechi 7 na sare 1 na hivyo kuongoza kundi lake kule Ubelgiji.

-Imefunga goli 22 na kuruhusu 2 tu.

-ingawa imebakiza mechi 2 Genk tayari imefuzu ikingoja kuvaana na mshind wa kundi A. Kisha endapo itashinda itamva mshindi baina ya namba nne na tano kwny msimamo wa sita bora kupata tiketi ya Europa.

5. Yanga kusaka taji mbele ya Toto leo. Wakishinda ni wazi watakuwa wametwaa taji la ligi kuu.

6. Mengineyo
-kadi nyekundu ya Mbaraka yafutwa.

-Mwamuzi Ngole Mwangole aondolewa kunako orodha ya waamuzi ligi kuu.

-naodha wa Serenget boys Issa Abdi Makumba aliumia kabla ya serengeti kuanza kukipiga Afcon na sasa ataikosa Michuano hiyo. Na

-imedokezwa Simba huenda wasiende tena FIFA. Ni endapo Yanga atashinda leo.

Kiafrika
-Afcon ngazi ya vijana leo mapumziko.

-Kesho Guinea Cameroon, Ghana Gabon. Guinea wanaongoza waliibamiza Gabon 5-1, Ghana iliizodoa Cameroon 4-0.

Kimataifa
1. Chelsea yadhihirisha haikubahatisha kutwaa EPL. Yaibongeza Watford 4-3
(Goli za Terry, Azipilicueta, Batshuayi, Cesc).

2. Reading kuialika Fulham sa 3:45 hii leo, ni kusaka tiketi ya kucheza EPL. Mechi ya awali walitoka 1-1. Mechi nyingine baina ya Sheffield Wednesday na Huddersfield itapigwa kesho.

3. Mechi za leo EPL
-Manchester City na West Bromwich sa nne usiku.
-Arsenal na Sunderland sa 3:45 usiku.

4. Mechi ya kesho EPL
-Southampton kuivaa man United sa 3:45.

5. Mechi Nyingine za kesho ulaya
-Juventus kuivaa Lazio fainali ya Coppa Italia.

-Celta Vigo kuikaribisha Real Madrid, ni ile mechi ya kiporo.

-nao mabingwa wa ligi kuu ufaransa Monaco watawaalika St Étienne.

6. Zinazohusu Usajili.
-Ryan Giggs asema manchestee United inahitaji nyota wanne mpk watano. Adokeza Alexis Sanchez atawafaa.

-Edison Cavan asema Sanchez, Aubameyang waje tu PSG nitawakaribisha.

-Arsenal yahusishwa na mlinzi wa kati wa Middlesborough aitwaye Gibson. Pia yatajwa kuliamsha kwa Mahrez wa Leicester.

-Kinda anayetabiriwa makubwa siku za usoni, Vicinius wa Flamengo kasain tena klabuni kwake mpk 2019. Hata hivyo imedaiwa Real Madrid italipa pauni milion 45 atapotimiza miaka 18, June 2018.

-klabu ya Grémio ya nchinj Brazil yakana nyota wake Luan kuafikiana na Liverpool. Luan anatabiriwa kuwa Ronaldinho mpya.

-imedaiwa Real Madrid itahitaji pauni milion 75 Kwa klabu itayomhitaji James Rodrigues.

-Everton yamgeukia Lanzini wa West Ham United.

-imedaiwa endapo Bale akitimka Real Madrid klabu hiyo itafanya kila italoweza imnase Griezman.

-Imedaiwa Schalke haina pingamizi na itamruhusu Kolasinic kutua Arsenal HAPO julai mosi.

7. Nyinginezo
-Chelsea yafikia rekodi yake ya kushinda Mechi 29 za ligi kuu ndani ya msimu.

-Neymar asema huu ulikuwa ni msm wake bora kabisa Barcelona.

-Kasper Schmeichel atwaa uchezaji bora wa msimu Leicester City.

-Tuzo ufaransa: Mbappe atwaa mshambuliaji bora. Kante mchezaji bora anayecheza nje ya ufaransa na kocha
Jardim wa Monaco atunukiwa ukocha bora wa msimu.


SOURCE MICHEZO NA BURUDANI GROUP WHATSAPP


No comments

Powered by Blogger.