…..MNAWACHOSHA MAGOLIKIPA, NA LAANA HII ITAWATAFUNA…….
Priva, ABIUD
Kijiweni kwetu…
Kuna baadhi ya mambo huwa
yananitatiza sana, jambo la kwanza ni vita kati ya washambualiaji na makipa na
mara nyingi mshindi anaibuka kuwa mshambualiaji. Kuna wakati nawaza marefa wanapenda kuona magoli sana yakifungwa bila kujali uhalali wake? Waamuzi wengi duniani wameonekana kuwa wauwaji zaidi
kuliko kuokoa. Marefa hawa wamekuwa wakirahisisha michezo ili kuwaondolea
ugumu. Mwamuzi anaweza akafanya kwa makusudi kabisa maamuzi yatakayoibeba timu Fulani,
sio kwamba anaipenda la hasha, lengo lake ni kuharibu timu moja ili kupunguza
kasi ya mchezo na kufanya iwe rahisi kwake. Mchezo unapokuwa wa kasi au
unapokuwa mgumu waamuzi huwa wanatafuta mlango wa nyuma. Kwa mfano rudia
kuangalia magoli ya mchezo kati ya Barcelona dhidi ya PSG na mchezo kati ya
Madrid dhidi ya Buyern Munichen. Kisha angalia mchezo wa Man Utd dhidi ya West
ham, pia jikukumbushe mchezo wa Man city dhidi ya Middlesbrough na mchezo wa
Man utd dhidi ya Swansea. Maamuzi ya waamuzi yamekuwa mzigo mkubwa kwa walinda
mlango.

Magolikipa wamekosa thamani kubwa
uwanjani. Kipa wa Real Madrid anaweza akaokoa mpira mmoja ambao kama ungeingia
golini basi ingeitoa Madrid mchezoni, lakini dunia isimtazame hata kidogo, ila
goli atakalo funga Cristiano Ronaldo dakika ya 88 hata kama ni la kusawazisha
litamweka kwenye ukurasa wa mwanzo wa kila gazeti. Magolikipa mara nyingi
wamekuwa ndiyo wanashikilia matokeo ya timu, lakini hata afanye jambo gani
hakuna anayemkumbuka kama mshambuliaji atafunga goli la muhimu. Nataka nijaribu
kusema kitu Fulani, kuwa kosa moja la goli kipa linaweza kuigharimu timu nzima na
likaharibu mipango yote ya timu hata ile mipango iliyopangwa kwa mwaka mzima. kwa hiyo kipa ni mtu muhimu sana na anapaswa kuangaliwa kwa kina.

Pia
jitihada kidogo tu ya goli kipa inaweza ikaleta furaha ya mashabiki na timu
kwa ujumla, lakini jitihada ile itaondolewa na goli la kichwa ambalo litafungwa
hata na beki ilimradi tu liwe goli la ushindi au kusawazisha. Magolikipa wamekuwa
na kazi ngumu sana magolini lakini marefa wanatumia silaha ya namna ya
kuwalinda kuwachinjia mbali. Oliver Khan aliwahi kusema kuwa golikipa ni kujitia uchizi, yaani ni kuruhusu watu wakupigie mashuti makali kwa nguvu zao zote na kuanza kujisifia kuwa wamefanya jambo kubwa. usidhani kama kupigiwa mashuti kama yale na kuyapangua ni jambo la kawaida, tena magolikipa huwa hata hawapewi nafasi kwenye tuzo mbalimbali kwa kuwa mchango wao unaonekana wa kawaida
FIFA inaamiini kuwa madhara ya
mikono ya golikipa kumgusa mshambuliaji hata kwa bahati mbaya ni makubwa mno
kiasi kwamba anastahiki kadi nyekundu. Je madhara ya mshambualiaji anayedanganya
ili kipa apewe kadi nyekundu na apate penati hili nalo limekaaje? Je ni kwamba
FIFA haithamini umuhimu wa magolikipa uwanjani?
Mimi sikatai kama waamuzi ni
wanadamu, wanafanya makosa sawa, kuwa mwamuzi ni sawa na mwanadamu kuingia kwenye
kundi la mbwa wanaopigania nyama, shida inakuja kuwa wanadamu hawa nao wanashikwa
na tama wanapigania nyama ile ile. Unapokuwa mwamuzi mimi naamin kuwa ule
mchezo unapaswa uuchukulie kama mchezo wa fainali hata kama ni mechi ya
ufunguzi. Waamuzi wengi wanasahau majukumu yao na wanaweka hisia mbele.
Ushauri wa wangu ni nini?
Beki akimgusa mtu kwa bahati mbaya
hata kama ni mtu wa mwisho kadi nyekundu isitumike kwa sababu hata kipa ana
nafasi yake kubwa tu uwanjan. Naamini adhabu ya penati au kadi ya manjano ni sahihi kabisa hasa
pale beki anapocheza faulo ndani ya boksi ikiwa faulo ile haikuwa na dhamira mbaya na ikiwezekana kama faulo ile ni ya kawaida au ya bahati mbaya na aliyecheza faulo ile tayari ana kadi njano basi hekima ya Pelluge Colina itumike. Kwanini nasema kadi nyekundu
isihusike? Kwanza kama Yule mchezaji alikuwa na nafasi ya kufunga basi kuna
mawili? Akose au afunge. Kitendo cha yeye kupewa penati basi ni nafasi tosha ya yeye kufunga kwa sababu anakuwa yeye mwenyewe na golikipa tena akiwa na uhuru mkubwa
zaidi tofauti na hapo awali. Tunaamini kuwa penati ni asilimia 80 kwa mpigaji kufunga kukosa ni bahati mbaya au uzembe. mara nyingi magolikipa hawana chakupoteza kwenye penati ni maamuzi ya mpigaji tu.
Mpigaji wa penati huwa anapewa nafasi ya pili tena akiwa huru, tena akiwa na golikipa mwenyewe. Akiwa na nafasi ya kuchagua wapi pakupiga na apige vipi tofauti na awali alipokuwa
akikabwa na beki tena akiwa katika kasi ambayo ingemnyima uhuru wa kupiga
atakavyo. Mzigo huu wa kadi nyekundu na penati unamwendea
golikipa na anakuwa na wakati mgumu kwa makosa ya beki wake au makosa ya refa
au kwa bahati mbaya au udanganyifu wa mshambuliaji. Hivyo basi FIFA wajifunze
kupitia uongo wa neymar na wa Suarez kwenye mchezo dhidi ya PSG ambako mizigo
ya udanganyifu ilimwelekea golikipa bila kujali uongo wa mshambuliaji.Je kadi nyekundu iondolewe kwa mtu wa Mwisho?
Mimi siamini kama kadi nyekundu
inahusiana sana kumzuia mtu kufunga au la. Mimi naamini kuwa kadi nyekundu ipo
kwa ajili ya dhamira mbaya ya mchezaji ambayo husababisha madhara makubwa kwa
mchezaji aliyechezewa.
Kwa mtazamo wangu kadi nyekundu haipo kwa mchezaji tu
anayezuia goli ila dhamira mbaya. Hivyo kadi nyekundu itolewe tu pale dhamira
ya mchezaji inapokuwa mbaya. Kadi nyekundu itolewe bila kujali kama ni mtu wa
mwisho au lah, yaani itolewe tu kama kawaida. Kama faulo ya mtu wa mwisho itakuwa
na dhamira mbaya au kama itakuwa rafu mbaga basi itolewe lakini kama alikuwa katika harakati za kumzuia kufunga asipewe kadi nyekundu kwa sababu ndiyo kazi yake. ikumbukwe mpira wa miguu sio pulitebo useme watu wasigusane, mfano tu kumbuka mchezo wa Buyern Dhidi ya Arsenal? nilishangazwa sana na maamuzi ya refa kwa kumtoa Coshienly kwa kadi ya pili ya njano. Kazi ya beki ni kuzuia magoli, yaani ni kama mpira wa miguu haipaswa watu kukabana yaan hawapaswi kugusana kabisa. kadi nyekundu isitolewe tu eti kisa ni mtu
wa mwisho, ila itolewe kwa sababu faulo ni mbaya na alidhamiria kwa makusudi kabisa. kadi isitolewe eti kisa yule beki ni wa mwisho kwa sababu tayari kuna mtu
mwingine golini ambaye anaweza kuzuia hivyo beki asihesabiwe kama ni mtu wa
mwisho ila wapewe kadi nyekundu kwa makosa yao na sio sheria ya mtu wa mwisho.
Kingine kama faulo amecheza goli kipa kwa bahati mbaya basi itolewe
penati tu, ila kama amecheza faulo ya kawaida nje ya boksi la penati itolewe kadi
ya nyekundu kwa sababu hiyo ni dhamira mbaya na golini hamna mtu hivyo tunaweza
kusema Yule ni mtu wa mwisho na golini hakukuwa na mtu hivyo ni rahisi kwa mfungaji
kufunga. Ila kama ni ndani ya boksi penati na ni faulo ya kawaida ukiachilia ule upuuz wa mtu kujitega kwenye miguu ya kipa itolewe kadi ya njano kwa goli kipa
na penati kwa kuwa lile ni eneo sahihi la goli kipa. Kwanini nasema hivyo? Lengo langu tafsiri ya mtu wa mwisho, ni
kwamba lazima golini asiwepo mtu kabisa ili uwezekano mkubwa wa mshambuliaji kufunga
uwe asilimia 88 na sio 50 kwa 50, tofauti na hapo tafsiri ya mtu wa mwisho itakuwa na mkanganyiko mkubwa.
Kingine kama faulo amecheza goli kipa kwa bahati mbaya basi itolewe
penati tu, ila kama amecheza faulo ya kawaida nje ya boksi la penati itolewe kadi
ya nyekundu kwa sababu hiyo ni dhamira mbaya na golini hamna mtu hivyo tunaweza
kusema Yule ni mtu wa mwisho na golini hakukuwa na mtu hivyo ni rahisi kwa mfungaji
kufunga. Ila kama ni ndani ya boksi penati na ni faulo ya kawaida ukiachilia ule upuuz wa mtu kujitega kwenye miguu ya kipa itolewe kadi ya njano kwa goli kipa
na penati kwa kuwa lile ni eneo sahihi la goli kipa. Kwanini nasema hivyo? Lengo langu tafsiri ya mtu wa mwisho, ni
kwamba lazima golini asiwepo mtu kabisa ili uwezekano mkubwa wa mshambuliaji kufunga
uwe asilimia 88 na sio 50 kwa 50, tofauti na hapo tafsiri ya mtu wa mwisho itakuwa na mkanganyiko mkubwa.

Leave a Comment