..,,,HIVI UNAFAHAMU KWAMBA KATI YAO YUPO MGANDA ALIYEMTOA KIJASHO MOURINHO..?
Na Priva ABIUD.
Kijiweni kwetu
Wakati
Man Utd ikiumana na Celta Vigo na Midjytland kuna kijana mmoja mweusi alikuwa
amekamata dimba la kati kwa jina anaitwa Pione Sisto. Huyu kijana alionekana
kung’aa alipokuwa Midjytlan na hata kwenye mchezo wa hivi majuzi akiwa na Celta
Vigo. Huyu ntamuongelea baadae ngoja niwazunguzmie kaka zake kwanza;
*****************************************************************************
Peter Schmeichel |
Wakati
nazaliwa mnamo mwaka 1992 kikosi cha bwana Richard Moller Nielsen kiliishangaza
dunia, kwa kuichabanga Ujeruman waliokuwa mabingwa wa kombe la dunia kwenye
michuano ya Euro. Kichapo kile Denmark ilichokitoa kilimfanya nguli wan Nchi hiyo Michael
Luadrup kustaafu soka. Denmark walikuwa wakiongozwa na mlinda mlango
anayeaminika kuwa mlinda mlango bora kuwahi kutokea Bwana Peter Schmeichel.
Hicho ndicho kilikuwa kizazi bora kwa Denmark kwa wakati ule na katika Historia
ya nchi hiyo.
Katika historia ya taifa ile hatuwezi kuacha kumzungumzia Brian
Laudrup ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Denmark kwa mara nne na
pia aliwahi kutajwa na FIFA mwaka 1992 kuwa mchezaji wa tano kwa ubora duniani
kwa mwaka ule. Ni mchezaji ambaye sima wa soka kutoka Brazil Pele alimtaja
katika orodha yake kuwa ni mmoja kati ya wachezaji bora dunian kuwahi kutokea
duniani akimweka nafasi ya 125.
![]() |
Michael Laudrup akimpa mdogo wake kitambaa cha unaholdha |
Michael laudrupp ni kaka yake na Brian Laudrup ni mmoja kati ya
wachezaji bora kukumbukwa katika ardhi ya Denmark akikukumbukwa kwa mafanikio
yake aliyopata ndani ya Barcelona Ajax Real Madrid na Juventus. Ni mmoja kati
ya viungo waliong’ara kipindi cha Johan Cruyff alipokuwa kocha mkuu wa
Barceolna, walipotwaa vikombe tisa ndani ya klabu ya Barcelona. Mwaka 1999 alitajwa
kuwa mchezaji bora wa kigeni bora wa ligi kuu Hispania kwa kipindi cha miaka
25. Mwaka 2006 alitajwa na chama cha soka cha nchini humo kuwa mchezaji bora wa
Muda wote kutoka Denmark. Wakati
Laudrup mkubwa akitajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji bora kuwahi kutokea katika
nchi za Scandinavia {Sweden, Norway, Denmark n.k} akimpiku mtu kama Zlatan
Ibrahmovic pia ni moja kati ya wachezaji waliochezea mahasimu wawili Barcelona
Na Madrid na kupata mafanikio katika vipindi vyote. Anatajwa pia kuwa kati ya
wachezaji 11 bora kigeni katika historia ya Real Madrid. Kizazi cha akina
Laudrup kimeshaondoka Denmark. Kimekuja kizazi kingine kabisa. Kizazi hiki
kilianza mizizi yake kwenye michuano ya UEFA ya wachezaji wenye chini ya miaka 21 mwaka 2014. Kikosi kile
kilicheza michuano yote ya kufuzu michuano ile bila kufungwa mchezo hata mmoja
kwa kushinda michezo nane na kutoa sare michezo miwili.
![]() |
Pierre Emile Hojbjerg |
Katika kikosi kile
kilikuwa na kijana mmoja anaitwa Pierre Emile Hojbjerg ambaye akiwa na miaka 14
tayari wanadenmark washamwita Zidane wao. Akiwa na miaka 17 alisajiliwa pale
Buyern Munichen. Mwandishi maarufu kwa jina la Jonathan Fadugba mnamo mwaka
2016 alisema kuwa Kijana huyu aliyeanzia maisha kule FC Copenhagen ambaye kwa
sasa anakipiga Southampton anaweza akawa na balaa kuliko Staa wa taifa hilo kwa
sasa Christian Eriksen anayekipiga Tottenham Hotspur. Kijana huyu akiwa na
miaka 17 na siku 251, aliweka rekodi ya mchezaji mdogo kuwahi kucheza kwenye
mchezo wa mashindano ndan ya klabu ya Buyern Munichen mnamo mwaka 2013. Mbali na
baba yake kukutwa na matatizo ya kansa kocha mkuu wa Buyern bwana Pep Guardiola
alimsaidia baba yake na Hojbjerg kuhakikisha anapata matatibu. Hojbjerg anasema
siku ya kwanza Pep kukutana na baba yake, Pep alitoa machozi kutokana na hali
ile.
*****************************************************************************
Tukiachana
na huyo kuna fundi mwingine aliyemtoa kijasho Jose Mourinho. Anajulikana kama
Pione Sisto. Mashabiki wa Man Utd watamkumbuka vyema kwenye mchezo wao dhidi ya
Celta Vigo. Ni kiungo wa katikati hivi, mweusi, anakata mbuga kama N’golo Kante
vile. Huenda wadernmark wasimsahau Michael Laudrup lakini huyu nae atakuwa moja
ya lulu walizobarikiwa kwa miaka ya hivi karibuni ukiachana na Christian
Ericksen. Akiwa na miaka 18 alikipiga katika klabu ya Midjylland na alitwaa
tuzo ya mchezaji bora wa mwaka akiwa na miaka 18 tu. Aliifungia klabu ile magoli 20 katika michezo
90, kwa idadi hiyo ya magoli mengi huku akiwa kiungo wa kati tu. Barcelona Juventus
Milan na Porto zilimmendea kwa miaka kadhaa kabla ya Arsen wenger nae kupeleka
ofa yake. Wakati Man Utd ilipotwangwa na Midjytlland 2-1 yeye alifunga goli
moja na alikuwa balaa mbele ya ulinzi wa Man Utd.
huyu ndiye Mganda Pione Sisto |
***********************************************************************************
Pia
kuna kijana mwingine anaitwa Andreas Christensen, nadhani mashabiki wa Chelsea wanaweza
kumwelezea vizuri maana alijunga na academy ya klabu hiyo akitokea kwenye klabu
ya nchini kwao iitwayo Brondby. Cheslea alicheza mchezo mmoja kabla ya kuelekea
Ujeruman. Conte alitaka kumrudisha kikosini mwaka huu mwezi wa kwanza. Amekuwa ndiyo
kiongozi wa klabu ya Borussia Monchengladbach akiwa na wastani wa 4.5 kati ya
5, akiwa amejikusanyia alama 624 kutokana na kituo maarufu cha kutoa takwimu za
wachezaji kijulikanacho kama Squawka. Kwa msimu huu amezuia mipira ya juu kwa
asilimia 64, amekuwa na wastani mzuri wa pasi kwa asilimia 90 amemzidi hata
Paul Pogba. Ana uwezo mkubwa wa kuzuia
mipira, umakini katika kupiga pasi na utulivu wa kipekee uwanjan, yaani ni kama
Michael Laudrupp amerudi tena uwanjani.
***********************************************************************************
Ajax
nao wana mdenmark mmoja anajulikana kama Kasper Dolberg ukimwona akiwa amevaa
jezi ya Ajax unaweza ukadhani Yule dogo ni mholanzi lakini sio.
Kasper Dolberg |
Aliyeibua kipaji
cha kijana huyu ni Yule Yule skauti aliyewaleta zlatan, Ericken, nad Fischer
sokoni. Msimu huu ndani ya Ajax ana magoli 18 na ametengeneza magoli 6 katika
michezo 38. Kwa takwimu hizo huyu nae ana balaa nan do kwanza ana miaka 18. Huu
ndio kwanza msimu wake wa kwanza kuwa kikosi cha kwanza ndani ya Ajax na tayari
ana balaa. Kwenye mchezo wa Mwisho dhidi ya Ajax ndo nilianza kumwelewa huyu
kijana baada ya kuipatia klabu yake goli la pili dhidi ya Olympic lyon. Ndani ya
Ligi kuu uholanzi tayari ameshafunga magoli 15 latika michezo 25 huku michuano
ya ulaya akiwa na magoli 3 kwenye michezo 6 huku michuano ya UEFA akiwa na goli
moja katika mchezo 1 tu. Mpaka kufikia sasa yeye ndiye mchezaji bora ndani ya
ligi kuu uholanzi akiwa na wastani wa 3.5 [squawka] Nataka pia nikumegee tena
na motto mmoja mchafu sana anajulikana kama Jens Odegaard, achana na Martin
Odergaad Yule wa Madrid, huyu ana miaka 17 tu, na kwenye michuano ya UEFA ya
miaka 17 tayari ameshakuwa gumzo huko. Wadernmark wanamwita Marco Van Bastern
wao, ni mshambuliaji wa mwisho. Wapo wachezaji wengi kama kipa wao Peter
schmeicel anayekipiga Leicester City, pia yupo Ericksen anayekipiga Tottenham.
![]() |
Viktor Fischer |
Pia
yupo kiungo wa zaman wa Ajax ajulikanae kama Viktor Fischer mwenye miaka 22
ambaye aliichezea Ajax Michezo 80 na kufunga magoli 25 huku akiwa na magoli
matatu timu ya taifa kwenye michezo 13 alitajwa kuwa mchezaji chipukizi mara
mbili akiwa Denmark na baadae akiwa Ajax, pia akiwa kwenye michuano ya wachezaji
wa chini ya miaka 17 aliweza kuifungia timu yake ya taifa magoli 20 katika
michezo 30 na waliweza kufika nusu fainali ya kombe hilo kabla ya kufungwa na
Ujeruman. Babu yake fischer pia alikuwa mcheza soka wa zaman wa taifa hilo
bwana Poul Pedersen ambaye alikuwa akisakata kabumbu kama winga teleza miaka
hiyo.
*******************************************
Nini hasa lengo langu
kuwazungumzia hawa,? Kwanza ukiangalia taifa la Ubelgiji lilikuja kwenye raman
za soka baada ya wachezaji wake wadogo kutambulishwa katika ligi kubwa barani
ulaya huku pia wakiwa wachezaji tegemezi ndani ya klabu hizo. Kwa kuangalia
namna Ubelgiji walivyovuma, ni kama naoana Denmark wakipitia njia ile ile. Kwa mfano
ukiangalia vijana hao wote, wapo chini ya miaka 23, maana yake miaka 6 ijayo
Denmark itakuwa na vijana zaid ya 8 ambao tayari ni wachezaji wakubwa na
tegemezi katika kikosi chao. Vijana hao wameshaonesha viwango vikubwa kiasi kwamba
tayari ni chachu kwa vijana wengine walibakia. Sisto Pione ambaye ni mzaliwa wa
Uganda tayari ameshaonesha kiwango cha aina yake. Sisto ameikataa Uganda na
kwenda Denmark kwa sababu tayari ameshaona mwanga mbele. Tayari academy za
Lyseng IF, academy ya Lyngby BK, Aalborg bila kusahau academy ya Midjytlland
ambayo imekuwa gumzo kwasasa. Hizo shule za soka zote tayari zitapata mwamko wa
kuzidi kuendelea kuinua vipaji zaid. Natoa angalizo ni mapema sana kufananisha
kizazi hiki na kile cha mwaka 1992 kwa upande wa mafanikio lakini tayari
wameshaonesha cheche.
Leave a Comment