PIIRLO ALITENGENEZA HESHIMA, DONNARUMA HATAKI HESHIMA AMECHOKA KULA DONA
Na
Priva ABIUD.
Kijiweni......
Ni
miaka 6 imepita tokea mkurugenzi wa zaman wa Ac Milan bwana Adriano Galliani
afanye kosa aliloliita kosa lake la maisha. Ni pale alipomruhusu kiungo bora
kabisa Andrea Pirlo kujiunga na mahasimu wao wakubwa Juventus. Kosa alilolifanya Gallian kwa sasa linamtesa
mkurugenzi mkuu wa Millan kwa sasa Marco Fassone ambaye ameingia mgogoro mkubwa
na Wakala wa Golikipa wa klabu hiyo Gianluigi Donnarumma kwa kila kinachoitwa
vita ya pesa. Donnaruma amedai kuwa
anashindwa kuongeza mkataba kwa sababu ametishiwa sana na mashabiki wa klabu
hiyo na hata taifa kwa ujumla.

Donnarumma mlinda mlango kwa Ac Milan kwa sasa anaishi kama mkimbizi ndani ya taifa
lake. Hivi majuzi tu kwenye mchezo wa
timu taifa ya vijana ya Italia donnarumma alitupiwa hela feki na
mashabiki kwa kile walichodai kuwa bwana mdogo amegomea mshahara wa E80,000 kwa
wiki akiwa na miaka 18 tu. Mino
Raiola aliyekuwa dalali wa dili la Paul Pogba, ndiye wakala wa Donnarumma, na
amekanusha kuwa mteja wake kuwa hajasaini wa sababu za kifedha ila anahofia
usalama wake klabuni hapo. Donnaruma alijiunga Ac milan akiwa na miaka 16 akiwa
anapata mshahara wa E100,000 kwa mwaka.

Walio
wengi wanamtukana Donnaruma wanasema kuwa anapenda hela kuliko klabu ya Ac
Milan.
Kwa akili ya kawaida ni nani hapendi pesa? Yuda Iskarioti mwenywe
alimuuza Mwana wa Mungu kisa pesa. Makanisa mengi duniani yanahimiza matoleo ya
sadaka, wewe ni nani asiyependa pesa kama viongoz wa dini wanatuhubiria kuhusu
sadaka? Hivi unajua kazi anayoifanya Donnaruma pale golini? Yaani mtu anajitupa
kufuata mashuti ya watu mnasema anapenda hela? Mlitaka apende nini?Cha
muhimu katika maisha ya mchezaji kwanza ni maslahi yake. Huwezi kutegemea kazi
ya mchezaji bila kutimiza maslahi yake. Wapo
watu wanaodai kuwa wachezaji wa siku hizi wanataka fedha nyingi ukilinganisha na
wa zamani.Naamini watu watakuja na mfano wa Messi kugomea waraabu wa Man city
na PSG kuwa hapendi hela. Kuna tofauti kubwa sana hapa, fahamu kuwa kuna
tofauti ya mchezaji aliyeridhika na pesa anazopata na yule ambaye yeye anaona
alizo nazo bado ni kidogo.Mshahara wa Messi pamoja na mafanikio yake yanamtosha
Willie Groves |
kabisa kususia fedha za klabu ambazo haziwezi kumpa mafanikio hayo. Donnarumma
yupo kwenye timu ambayo haina mbele wala nyuma kwa sasa na bado mshahara ni
mdogo je aendelee kubaki kisa anaogopa ataambiawa anapenda fedha nyingi? Hivi
fedha nyingi ndo nini? Kipi ni kipimo cha fedha nyingi? Dunia imebadilika sana.
Ulitegemea mchezaji ambaye ana kipaji kizuri apatikane kwa ada ya million 20?
Kwani tupo mwaka 2000? Hivi hao wazungu wanaotoa hizo fedha kwan wao hawaoni
kama ni nyingi? Ni kweli kiasi ambacho Moratta anahitajika nacho Man Utd ni
nyingi sawa, ila ni nyingi kwa wakati gani? Ngoja
leo niongee kiuchumi kidogo ili kidogo nieleweke, kwanza nataka nikwambie kila
baada ya miaka 7 mpaka 10 kuna uwezekano mkubwa
thamani ya kitu ikawa mara mbili zaidi ya kilivyo kuwa kiuchumi.
Usiniulize ni nani kasema, nimesema mimi mwenyewe. Nikukumbushe tu, mwaka 2000
dola 1 ya Marekani ilikuwa sawa na shilingi 800 ya Tanzania, leo hii dola 1 ni
sawa na 2300, hii inaashiria nini? Uchumi umebadilika sana. Nikurudishe mbali
sana, mchezaji wa kwanza kabisa duniani kuuzwa
alikuwa Willie Grove aliuzwa E100 kutokea West Bromwich albion na kwenda Aston
Villa mwaka 1893, ilipita takribani miaka 12 ile rekodi kuvunjwa na mchezaji
aliyefuata aliuzwa takribani E1000 ambapo mshambuliaji hatari wa Sunderland kwa
wakati ule Bwana Alf Common alipouzwa kwa Middlesbrough. Ukiangaliahiyo bei ni
sawa na takribani mara 10 ya bei ya hapo awali.
Hivi
hata nyie mashabiki wa Arsenal mnaosema Arsene Wenger ni mbahili hamjui kuwa kocha
wenu wa zaman Bwana Herbert Chapman aliweka rekodi ya kumnunua mchezaji wa gharama
kubwa mwaka 1928, walitoa kitita cha E10,000 ili kumpata David Jack kutoka
Bolton Wanderers hapo ilikuwa takriban miaka 10 baadae.
![]() |
katikati Bwana David Jack |
Nadhani mpaka hapo
unaelewa nini nachomaanisha. Bei za wachezaji zinapanda kutokana na hali halisi
ya uchumi kwa wakati huo. Au nikupe mfano rahisi tu, mwaka 2008 gari la kifahari
aina ya Buggati Veyron 16.4 liliuzwa
dola million 1 na ushee, lakini gari lile lile kwa mwaka 2015 linauzwa
takribani dola milion 2.5, hii ni mara mbili ya bei ya hapo awali. Maisha
yanabadilika, uchumi unapanda, bei ya maisha inaongezeka kwa kiasi kikubwa. Bei
ya Pirlo akiwa na miaka 22 ilikuwa E18 mnamo mwaka 2001, lakini huwezi kumpata
kiungo mkabaji mzuri kama Pirlo kwa wakati kwa bei hiyo hata kidogo.

Nmeuliza
tokea awali pesa nyingi ndo nini? Kipi ndio kiwango cha pesa nyingi? Je tutumie
kigezo gani kusema pesa ni nyingi? Twende taratibu tu utanielewa. Najua
unamfaham Juan Veron? Bila shaka unamfahamu. Huyu aliweka rekodi ya kununuliwa
ghali zaid mwaka 2000 kiasi cha E28, katika ligi kuu ya England alipojiunga na
Man Utd. Je unafahamu ilichukua muda gani ili mchezaji apatikane kwa mara mbili
zaid ya bei ile? Naam mwaka 2014 Angel Di maria aliweka rekodi hiyo kwa kitita
cha E58 akijiunga Man Utd ile ile iliyoweka rekodi ya awali. Nataka niwaambie
kitu ndugu zangu, nadhani ni vyema bei zikalinganishwa kwa miaka ili kupata
uwiano mzuri na sio tu kisa namba zikionekana nyingi basi hiyo pesa n nyingi
sana. Mfano mwingine mrahisi, tujikumbushe hapo awali, miaka ya 2000 soda
tulinunua shilingi ngapi? Sio 200 kweli? Je leo hii 200 unapata nini? Je miaka
ya nyuma unakumbuka thaman ya senti tano? Je bei ya soda kwa sasa na kwa wakati
ule sio mara mbili?
Kwanini
tunawalaumu akina Mbappe wakitakwa kwa E130? Unadhani wazungu wamewehuka?
Maisha yamebadilika mno. Thamani ya pesa inapanda sana. Unategemea Donnarumma
hapendi maisha mazuri? Hivi ni kweli kwamba hapendi kutembelea gari ya lakshari kama Buggati Veryon? Unadhani
yeye hapendi kupumzika hoteli za kifahari kama Pallazo Parigi kule milano? tena kwenye vyumba
vya gharama kabisa? Unafikiri hapendi kwenda fukwe za Puglia na San Vitolo Capo
kule sicily kula bata wakati wa mapumziko na familia yake? Yaani kwa akili yao
wanafikiri Donnarumma anapopigiwa mashuti golini na kudaka kama mtu asiye na
akili kwamba hawazi maisha mazuri?
Twendeni
mbele turudi nyuma, ukisikia E100 usidhani kwa wenzetu ni nyingi sana kama
tunavyowaza hapa kwetu bongo. Ukweli ni kwamba klabu kama Man Utd na Madrdi
zina takribani utajiri wa Dola billion 3 na ushee kila moja. Sasa kama timu ina
utajiri huo kumnunua mchezaji ghali sie kinatuuma nini? Yaani leo hii Bakhresa
amenunua andazi la 100 kwa 1000 unalalamika?
Mimi
sioni kama ni matumizi mabaya ya fedha nachokiona ni mabadiliko yametokea
kwenye uchumi wa dunia. Siku hizi wametokea mawakala virambasi sana, na wenyewe
wanataka cha juu kwenye kila dilia wanalo piga, je unategemea utampata mchezaji
kwa bei za mbuzi? Huna pesa kaa kimya. Usiseme kama Man Utd inaharibu soka kwa
kununua wachezaji ghali kwamba timu ndogo zitashindwa kufanya usajili, kwani
timu gani ndogo imenunua mchezaji ghali? Kama hazijawahi shida iko wapi Man Utd
na liverpool zikimwaga hela? Msinielewe vibaya, hapa sizungumzii soka la
biashara la wachina. Wale wanajielewa wao wenyewe, nao wana mipango yao. Hao si
wazungumzii kabisa.
Kiuhalisia
milion 100 kwa sasa ni sawa na Million 40 ya miaka 10 iliyopita wala hilo
halipingiki kabisa. Labda tu nikukumbushe rekodi zilitolewa na Delloite kuhusu
mapato ya Real Madrid na Man Utd kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2001 hadi 2011,
mwaka 2001 zote kwa pamoja ziliikusanyia zaid ya million 350, lakini kufikia
mwaka 2011 zote zilijikusanyia mapato ya takribani million 800, sasa unategema
nini? Kama timu inapata mafanikio makubwa kiasi hiki kama tunavyoona kwanini
wachezaji nao bei zao zisipande? Sasa kama Ac Millan imenunuliwa kwa mkataba wa
zaid ya billion 1, lakini bado Donnarumma analipwa 100, 000 kwa mwaka
unategemea nini? Kwanza Donnarumma anataka zaid ya million 10 kwa mwaka.
Ashafahamu kuwa ana kipaji ambacho kinauzika kwa gharama yoyote kwa sasa duniani.
Sasa ya nini masikini kumpangia tajiri namna ya kutumia hela? Umri wa mchezaji
sio tatizo kabisa, kwani Henry alinunuliwa bei gani na alikuwa na Umri gani? Je
kuna mtu alitegemea balaa la henry hapo baadae? Maana henry alinunuliwa E16 akitokea
Juve akiwa na miaka 20 tu, lakini kila
mtu alimnyooshea kidole Wenger. Lakini Rekodi ya Henry inakuja kuvunjwa baada
ya miaka 13 na Mesut Ozil aliponunuliwa kwa ada ya E47 akiwa na miaka 24. Je ulitegemea
kumpata ozil kwa bei ya Henry ya mwaka 2000 kweli? Labda nikuulize swali la
kizushi tu, si unafahama Coutinho wa liverpool? alinunuliwa Million 7 akitoke
Inter mwaka 2013? Je ingekuwa ndio sasa hivi yupo Inter angeuzwa bei hiyo hiyo
kweli? Narudia tena heshima zipo jeshini kwenye soka cha kwanza maslahi. Siku njema.
Leave a Comment