BENITEZ HAJAMJUA MCHAWI WAKE

UVUNGUNI



Rafael Benitez ni Kocha mkubwa sana duniani. Hilo lipo wazi. Ni kocha aliyebeba laliga mara mbili akiwa na Valencia, Uropa akiwa na Chelsea, Copa Italia na Napoli, na Ubingwa wa Uefa akiwa na Liverpool. Kiuhalisia sio kocha wa Level za Newcastle ya sasa. Msimu uliopita alikuwa championship, kwa uvumilivu alipambana nayo na hatimaye ameirudisha Newcastle EPL. Juzi juzi Jammie Caragher alisema anaamini kuwa Benitez atabaki Newcastle misimu mingine zaidi. Lakini tetesi zishaanza kuwa mkurugenzi mkuu wa Newcastle bwana Lee Charnley ameshindwa kabisa kushughulikia suala la usajili


Kwa miezi y 16 ya Benitez Pale Tyneside kumekuwa na mvutano mkubwa na Mwenyekiti wa bodi ya ufundi bwana Graham Carr. Inaonekana kuwa hawakuwa na mahusiano mazuri. Benitez alihitaji majina makubwa lakini kikwazo ni bwana Carr na Charnley. Klabu hiyo imepata mapato makubwa lakini kufikia sasa wamesajiliwa wachezaji ambayo yeye hajawataka hiyo ikiwa ni kazi ya Bwana carr


Mwishowe Bwana Carr ameondoka St James Park huku akikumbukwa kwa kuleta vipaji Murua kama Cheick Tiote, Yohan Cabaye na Moussa Sissoko. Carr ameondoka takriban mwezi umeisha lakini Bado Charnley hajafanya yale anayotaka Benitez. Benitez baso anataka kuendelea kupambana ila alichodhan kikwazo kwake kimeondoka lakin mkurugenzi mkuu bado hafanyi matakwa yake, Benitez alitaka awe mhusika namba mmoja kwenye usajili, kufikia mpaka sasa anga sio shwari kwake. Kufikia hapo siamin kama anaweza kuendelea kupambana na kikosi kile


Mnamo mwezi wa tano Paul Merson alisema kama Newcastle haitofanya usajili wowote wajiandae kumaliza ya 16, 17, au 15 wakijitahidi sana hivyo wajiandae kisaikolojia. Kwa mawazo yangu niliona ni kama ana wivu. Ni wazi sasa kikosi hicho ni dhaifu maana hata benitez mwenyewe amekiri licha ya kutaka kubaki klabuni hapo

Mbali na tetesi hizo Benitez amekiri kuwa wana hali ngumu kwa muda huu uliobaki kupata wachezaji muhimu. Hawezi kusema lolote kwa sababu dhamira yake ni kubaki kwenye jiji kubwa na lenye upendo kwake.... Lolote kaweza kutokea

#dinho


Graham Carr


No comments

Powered by Blogger.