R.I.P BRADLEY ROWERY. UMEFANYA DUNIA IYAONE MACHOZI YA JARMIEN DOFOE


Vita ya kuupigania uhai wako imefika tamati. Umeamua kuiweka nukta ktk ukurasa wa mwisho, kwenye kitabu kilichobeba simulizi ya huzuni juu ya maisha yako..Baada ya pumzi kugoma kuendelea kuishi kwenye matundu ya pua ulizonazo.. Na moyo kusitisha huduma ya kukusambazia damu kwenye mishipa. Umeamua kuipungia mkono wa kwaheri dunia. Kwasasa inatulazima kabla ya kulitamka jina lako tuanze na neno marehemu..

Marehemu Bradley Rowery. Wewe ni binadamu uliyeishi kwa miaka 6 tu chini ya mbingu.. Ila ni miaka 6 ya machozi jasho na damu.. Miaka 6 iliyobeba mateso huzuni na simanzi.. Miaka 6 iliyoufunga moyo wako pingu za huzuni kwenye jela ya majonzi..

Mara zote ulipokuwa kwenye vita ya kuupigania uhai wako.. Hospital uliigeuza ngao ili kuyadhibiti makombora ya maumivu.. Maumivu ambayo yalijigeuza fisi nakuishambulia mifupa yote ndani ya mwili wako.. Ikiwa ni matokeo ya saratani iliyoanza kukushambulia tangu ukiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi 6..

Ulikuwa shabiki mkubwa wa timu ya Sunderland. Timu ambayo a.k.a yake ni paka weusi. Naamini hata nawewe ulikuwa na moyo wa paka..Ndio maana hukukubali kuzifunika mboni za macho yako kwa usingizi wa milele..Mpaka nyakati ziliposimama nakukushuhudia kuwa kweli.. Sunderland imepoteza kibali cha kuishi ndani ya ligi kuu ya England..

Bradley Rowery. Ulikuwa ni mtoto wa kizungu uliyebeba moyo wa upendo wa kweli kwa mtu mweusi.. Ktk ligi kuu ya England yenye wachezaji zaidi ya 500..Wewe uliamua kuchagua kuishabikia miguu ya Jamernie Defoe..Naye hakukuangusha.. Kila alipozitendea ukatili nyavu za timu pinzani.. Magoal yake aliyatoa kama zawadi kwako..

Bradley habari za kifo chako zimeondoka na tabasamu la rafiki yako. Defoe ameshindwa kuyazuia machozi mbele ya TV uku dunia nzima ikimtazama.. Kila alipo jaribu kukuelezea kwiki za majonzi ziliishia Kuweka kizuizi kwenye koo lake..Moyo wake ukafunikwa na theruji ya huzuni.. Namboni za macho yake zakaishia kuitiririsha mvua ya machozi..

R. I. P BRADLEY. Wewe mbele sisi nyuma. Binafsi naamini umekufa mwili. Ila ki nafsi uhai. Na utaendelea kuishi nasisi ktk ulimwengu wa roho.

Written by Green Osward
0715 035 836

No comments

Powered by Blogger.