FIRMINO NI BORA ASIPOKUWA NA MPIRA
FIRMINO:MCHEZAJI MZURI ASIPOKUWA NA MPIRA.
A good player without the ball ndio kauli tunayoweza kuitumia kwa lugha iliyokuja na meli.Ukiangalia kwa jicho la juujuu unaweza usielewe kwa nini Klopp hafikirii wala hakuwa na mpango wa kusajili striker,Unaweza usielewe kwa nini wakati wenzake wako busy na Aubemeyang,Morata,Lukaku na Lacazette Klopp alishaamua Roberto Firmino kuwa striker wake msimu huu yeye akawa yuko busy kuwaza atampataje KEITA na VVD.Aliona vitu kwa Firmino ambavyo wengi hawawezi kuviona.
Firmino anavitu ambavyo ma striker wa asili wa nafasi hiyo hawana,firmino anaweza Ku press kuanzia mbele,firmino anaweza kushuka chini na kukaba timu inaposhambuliwa,firmino yuko dynamic sana kuna kipindi mchezo ukiwa unaendelea unaweza kumuona kama namba 10 wakati mwingine kama namba8 au ukamuona wings au kama kiungo mzuiaji,huu uwezo si wa kawaida lazima uwe na mapafu ya duma ufanye haya yote hii kitu huwezi kuipata kwa Lukaku,morata au Lewandosky.Vasatility yake inafanya Liverpool ionekane hatari sana kila inaposhambulia lango la adui kwani mabeki wanashindwa kumkaba firmino kama nani.
Kuna kipindi waandishi waliwahi kumuuliza KLOPP "umeamua kumfanya firmino kama mshambuliaji wako wa kati lakini si mfungaji mzuri kama ungekuwa na striker halisi,"Klopp akawajibu firmino ni mchezaji mzuri akiwa hana mpira hata asipofunga kwake haoni tatizo.Huyo ndo Roberto firmino hafungi lkn anachokifanya pale mbele ni cha maana kuliko kufunga Wakati mabeki watimu pinzani wanahangaika na firmino magoli ya Liverpool yanafungwa kutoka ktk kila angle za ushambuliaji.
Bayern 0 Liverpool 3:
Hatuhitaji kujisifu na kujikweza saana tukaona ndo tumemaliza la hasha hizi ni mechi chache tu za kirafiki za pre season ingawa wanachofanya Liverpool mpaka sasa ni kizuri kinacholeta matumaini.Mambo yanakwenda vizuri ingawa kwa mtazamo wangu bado tunahitaji zile sajili mbili alizotuahidi klopp zile sajili mbili zilizobaki zitakazongatia ubora kuliko wingi(quality than quantity),bado tunahitaji yule beki wa kati mmoja(CB) na yule kiungo wa kati mmoja(CM) then tufunge hesabu tuanze kupiga miluzi taratibu huku tunatafuna bisi na tende shake maziwa taratibu kabisa.
Kwa nini??
Kwa upande wa beki wa kati iko hivi kama matip na Lovren wataanza basi huyo awe back up yao coz bado Lovren anamakosa flani hivi anayafanya au kama huyo beki ataanza na matip basi Lovren awe back up yao.Ukija kwenye Kiungo wa kati naye bado anahitajika kama atasimama kama regular starter au back up,Kama no yeye na Hendo basi CAN awe back up au kama ni CAN na HENDO basi yeye awe back up.Tukifanikiwa maeneo haya mawili tukutane Final UCL.
Blog hii haina haki zozote za makala hii imepatikana whatsapp
Leave a Comment