LAMPARD NA GIGGS HAWANA MENO SIO? WATABWEKA SANA, ILA KUHUSU NYAMA WASAHAU
Na PrivaLDINHO
Uvunguni...
Ni miaka Takribani 25 imepita tokea ligi kuu England iundwe upya mnamo mwaka 1992. Lakini miaka 7 nyuma yake, kunako mwaka 1985 pale Liverpool palitokea Maafa. Uwanja wa Heysel ulianguka na Kocha Joe Fagan aliamua kujiuzulu. Wakati Fagan akijuzulu kama kocha wa Liverpool, kule chile Manuel Pellegrine nae aliamua kustaafu soka mwaka ule ule. Mtaalamu huyu mwenye Degree ya uinjinia wa Ujenzi Alipoulizwa kwanini aliamua kustaafu soka alisema kuwa "kitendo cha mtoto wa miaka 17 kuruka juu zaidi yangu na kufunga goli la kichwa ni fedheha kubwa kwangu". Niposikia kauli ile kwa haraka haraka nilikumbuka goli la kichwa la Messi Mbele ya Vidic na Rio. Aliyesababisha Pellegrin kuvua viatu si mwingine ni Ivan zamorano mfungaji bora wa Real Madrid 1995.
Fagan alipoamua kujiuzulu mwaka ule ule, Kenny Dalglish legend wa kukumbukwa milele pale liverpool alichukua mikoba yake akiwa kama kocha mchezaji. Alipata mafanikio mengi tu akiwa kama kocha na mchezaji ndani ya liverpool.
Ukiitazama vizuri ligi kuu ye England utagundua ni moja ya ligi kubwa na bora duniani. Kwanini nasema hivi. Hakuna nchi yoyote ndani ya miaka 12 iliyopita imeweza kupeleka timu zaidi ya tatu katika fainali za kombe la ulaya. Rekodi hazidanganyi, mnamo mwaka 2005 Arsenal vs Barca, 2007 Liverpool vs Ac milan, 2008 Man Utd Vs Chelsea, 2010 Man utd Vs Barca, 2012 Man utd Vs Barca, 2013 Chelsea Vs Buyern. England imeweza kupeleka timu 4, huku hispania zikiwa tatu tu.
Ligi kuu England kuna kitu nmekiona. Ukiitazama ligi kuu Hispania, inazalisha matunda mengi mno. Wakati England ikitoa Wachambuzi wazuri wa soka, kama akina Gary Leeniker, Garry Neville, Owen, Henry, Scholes na wengineo, Hispania wao wanazalisha makocha wenye mafanikio makubwa mno, ingawa Hispania pia wachambuzi wapo kama Kocha na mchezaji wa zaman wa Klabu ya Real zaragoza Babu Jorge Valdano anayefanya kazi Bein Sport. Kwa Mfano tu tokea mwaka 1992 England ni Makocha 9 tu walioshinda kombe la ligi kuu ( Ferguson, Ancellot, Deliglish, Wenger, Pellegrin, Mancinni, Ranieri Mourinho na Conte) na hao wote waliocheza ligi kuu England ni Keny Daliglish tu, huwezi simuhesabu Mancinni kwa sababu kwanza alikuja Leicester City akiwa na miaka 36, hakucheza hata mechi moja dakika 90, pili alicheza michezo mitano tu kisha akaenda Kuwa kocha Fiorentina. Hivyo takwimu zipo wazi hakuna mchezaji aliyewahi kucheza England zaidi ya (Dalglish alitwaa kombe hilo akiwa kama kocha wa Blackburn rovers mwaka 1993, tuseme hata na Mancini isiwe kesi) ambaye ametwaa kombe hilo akiwa kama kocha.
Kwa maana hiyo ligi kuu ya England inaonekana kuzalisha waandishi wa habari zaidi. Tukiiangalia upande wa Laliga, tokea mwaka 1992 ( Johan Cruyjff kocha na mchezaji wa Barca alitwaa la liga mwaka 1992, huku Jorge Valdano aliyeicheza Real zaragoza na Real Madrid, alikuwa kocha wa Madrid alitwaa laliga 1994, Radomir Antic Alicheza Zaragoza na alikuwa kocha wa Madrid na Barca nae alitwaa laliga, pia yupo babu Del Bosque mzaliwa wa Salamanca, kocha na mchezaji Madrid, Rafael Benitez huyu hakucheza sana Daraja la juu ingawa alicheza ndani ya Hispania katika klabu za Real Madrid C, Castila n.k nae alitwaa ubingwa wa La liga akiwa na Valencia, Rijkaard nae aliwahi kuichezea Real Zaragoza kwa mkopo na kutwaa la liga akiwa na Barca, Nadhani sina haja ya kuwazungumzia Guardiola, Zidane, Enrique na Simeoni pamoja na Marehemu Tito Villanova hawa wanafahamika kuwa wote wamechezea klabu walichobebea nazo makombe ispokuwa Tito licha ha kucheza a liga, kabla sijafunga hili listi mniwie radhi kwa kumsahau Bern Schuster babu kutoka Ujeruman aliyekipiga Barca, Madrid na Atletico na kutwaa ubingwa akiwa kama kocha wa Madrid.)
Makocha 11 waliowahi kucheza laliga tayari wametwaa la liga nimemtoa Benitez kwakuwa hakucheza ligi kuu ila alicheza daraja la pili na la tatu. Kwa Upande wa England ni Keny Dalglish tu ndiye mwenge medal akiwa kama mchezaji na pia kama kocha. Makocha wengi mno wamejaribu kama akina Mark Hughes, allardyce na wengine wengi wameshindwa. Wachezaji wengi waliocheza England kwa muda mrefu wamekuwa wapondaji tu kwenye vituo vya Tv. Garry Neville alijaribu lakini yaliyomkuta hayana tofauti na yale yaliyomkuta baba yetu mzee Kitwanga.
England kuna porojo nyingi licha ya ligi kuwa bora, huwa siku zote naamini mama akiwa mcheza vigodoro usitegemee mwanae akawa mwimba kwaya. Tazama akina Gerrad na Rio, wamejificha nyuma ya kioo cha BT sports Tv, ili kuponda wenzao kila kukicha. Lampard juzi nae kakimbilia huko huko. Sijajua hasa kwanini hawafuati nyayo za akina Zidane, Guardiola na Enrique , sijui hawaajiriki wale??, sijui ni waoga au ni nini. Msishangae hadi Thiery Henry wa watu nae kawa mzaramo. Naombeni mwenye namba ya mbwiga Mbwiguke amuulize kwanini Waingereza wanapenda kuongea sana je wana undugu na wazaramo??
Kama vipi naona haya ya uvunguni tuachane nayo maana ni kuchafu ......
Leave a Comment