MAFARAO NA VISIMA VYAO MAFUTA, WABRAZILI WAPO KWENYE FOLENI YA ESCROW
Na Priva ABIUD.
Miaka kadhaa iliyopita, kuna kauli Sir alex ferguson aliitoa, watu wengi wakasisitiza kuwa fergie ameona wivu na kuna watu walifika mbali wakasema uzee unampoteza. Ferguson alisema kuwa “fedha hainunui mafanikio” moja kwa moja aliilenga klabu ya Manchester City. Kwa kipindi cha miaka kadhaa, Man Utd na Liverpool zimetumia zaid ya million 700 kwenye usajili kwa lengo la kupata mafanikio na kuzidi kuimarisha hadhi zao n.k. lakini tunaona ni jinsi gani Man Utd, Liverpool, na Man city zinateseka masokoni (usajili) pamoja na viwanjani. Hii kauli mbali na kwamba Fergie alilenga klabu mimi nadhani kuna kila sababu ya kuliangalia hili katika timu za taifana kwa wachezaji pia.
****************************************************************************************
Mataifa Fulani kipindi cha nyuma yalionekana kuwa na uwezo mkubwa sana, kwa sasa mataifa hayo yanaonekana kupotea kwenye ramani ya soka. Juzi juzi zimepatikana taarifa kuwa Mohamed Aboutrika anatafutwa na serikali ya Misri kwa kujihusisha na masuala ya ugaidi, inasemakane jamaa anadhamini vikundi vya kigaidi huko misri. Hii yote ni kwa sababu ya utajiri wa fedha alizojichotea huko kwao. Ulishwahi kujiuliza mchezaji bora wa Africa kwa mara 4 na hajawahi kucheza moja ya ligi kubwa barani ulaya? Jamaa ametumia muda mwingi kucheza zaid soka la Africa ,lakini ana utajiri wa dola million 12 ikiwa jamaa anaizid utajiri klabu ya zamalek ambayo ina utajiri wa dola million 10>> ukiachana Aboutrika Kuna jamaa mwingine anajulikana kama Ahmed Hassan anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola million 11, pia nadhan wengi tunamkumbuka Hossam Hassan aliyeichezea timu yake ya taifa ya misri michezo 177 na kufunga magoli 79, huyu nae ana utajiri wa dola million 9 ingawa hajui legue kuu England ni nini lakin tayari ni tajiri mkubwa tu kuliko hata wachezaji wengi wakubwa wanaocheza ulaya, mfano mzuri pepe anayepokea dola millon 7 kwa mwaka. Kuna mchezaji bwana mdogo anayekipiga Al ahly, jamaa amecheza michezo 55 tu timu ya taifa lakini tayari ameshaweka kibindoni dola million 7. Achana na akina hosny Abdi Rabou mwenye million sita yupo pia goli kipa wao ambaye nae ana utajiri wa dola million 4, kuna kijana mmoja alikuwa fundi sana ambaye mpaka kesho namfananisha na Verrati Marco, mbali na jamaa kuwa kiungo mkabaji ila anaujua mpira vizuri, nae hapajui Uingereza lakini tayari ana dolla million 4.
*******************************************************************************************
Ukijaribu kuangalia vizuri timu ya taifa ya misri iliporomoka sana kwenye ubora wao kwa kipindi kirefu mno. Ukitazama kwa makini katika orodha ya wachezaji matajiri huwezi kuwaona akina Mohamed elneny, wala Mohamed sallah akiwa anapokea million 3 pale AS roma ikiwa huo ni mshahara wa Aboutrika ukitupilia mbali utajiri wake. Kiuhalia ligi za magharibi mwa Africa, ligi kuu Algeria inathamani ya million 87 sawa kiasi anachopewa mshindi ligi kuu England, ligi kuu Tunisia nayo ni million 81 huku morocco ikikadiriwa kufikia million 70, hii ndyo sababu inayowafanya wachezaji wengi wa kiarabu wasiwe na mchecheto wa kwenda ulaya lakini kwa upande wa Misri ni zaidi million 107.
***************************************************************************************************
Wakati kisima cha mafuta kinaingamiza misri kizazi cha wabrazil kinaangamizwa na Renmimbi (hela ya china). Kwa haraka haraka tokea mwaka 2014 kufikia leo tarehe moja mwezi huu wa pili tayari wachezaji 33 kutoka brazili wamelekea ligi kuu china ikiwa ni pamoja na wachezaji bora pamoja na wale tegemezi kabisa kwenye kikosi cha timu ya taifa. Kwangu mimi ni kama brazili inageuza mpira wetu kutoka kwenye uhalisia wake, yaani inabid mpira wao kwa sasa tuuite uchumi na sio soka, hakuna soka la aina hiyo. Vijana waliokuwa safi kabisa kama Renato Augusto, alex texeira, Geuvanio pamoja ana Ralf, ukiachana na hao Ramirez nae alitimkia huko kwa thaman ya paundi 37, taarifa pia zinasema kutoka mwaka 2001 kufikia 2010 tayari wachezaji 137 kutoka brazili tayari wameshasjiliwa ligi china. Wachezaji wengi wakubwa waliotimkia brazili wanasahau kuwa wanategemewa na taifa lao kwa kias kikubwa.
Vijana wengi wa kibrazili wamehamisha ndoto zao za kucheza soka ulaya na kuzielekezea nguvu zao zaidi kwenye fedha. Vijana hawa brazil hawafuati nyayo za waliowatangulia. Hwajifunzi kutoka kwa Lucas moura aliyekimbilia fedha za Warabu wa PSG, wamemsahau kaka yao kaka aliyekimbilia fedha za Madrid, wamesahau kuwa tama zilipoteza kiwango cha Robinho. Wanachowaza kuwa ni kuwa fedha nyingi, wanunue boti za kifahari kama ya Neymar, wanatafuta pesa nyingi ili wakirudi Copa Cabana wazungukwe na watoto wazuri mbele na nyuma, huku akiangalia maghorofa yake. Yaani wao wameweka mawazo yao kwenye utajiri zaidi. Ni kweli watapata utajiri mkubwa, hata ukifuatilia kwa makini utagundua Oscar Emboaba anapokea kiasi cha takriban billion 70 za kitanzania, lakini je timu yao ya taifa itakuwa na aina ya wachezaji gani? Kwanza tatizo la ligi kuu china haina ushindan,? na maisha ya brazili ni ya shida, kuna umasikini mkubwa tu kama bongo, kwa hiki walichoonesha, texeira, augusto, paulinho, hulk, Ramirez na Oscar ambao wote ni wachezaji ambao wana uhakika wanamba ya kudumu timu ya taifa wamekimbilia fedha. Mwisho wa siku wabrazili watakimbilia fedha china maanazipo zakumwaga, hawatajali kuwa watapata namba timu ya taifa au lah. Wakati moura kabla hajaelekea PSG alionekana moja kizazi cha kutisha sana kwa hapo baadae, tama zimemponza, Robinho nae tama zilimponza.
**************************************************************************************************
Timu ya taifa ya brazil kama wachezaji watakuwa na tama kiasi hiki, basi wanpotea njia, kwanza timu yao itajazwa na wachezaji ambao wengi wao hawana uzoefu wa michuano mikubwa, wakati England wakizilazimisha klabu kubwa kuwapa nafasi zaid wazawa kwenye vikosi vya kwanza, brazil wao wapo wamejazana viwanja vya shanghai na wengine wakiwa Zhongguo guangda yinhang ( moja ya benki maarufu kule uchina) wakipokea mabilion yao kama yale ya ESCROW. Brazil itakuwa na wachezaji wengi matajiri ila wasio kuwa na tija kwa taifa lao. Timu nyingi za taifa za ulaya zinfanya vizuri kwa sabau wachezaji wao wapo kwenye ligi kubwa na bora duniani ambako wanakutaa na ushindani mkubwa, waalimu wazuri pamoja na mazingir mazuri ya kisoka.
Leave a Comment