PAMBANA NA HALI YAKO
NATAKA TUBONGE KIDOGO KISOKA...
Kwanza tuwekane sawa... Kwa daraja la Neymar Jr mpaka anafikia maamuzi fulani kwenye maisha yake ya soka... Kuna kundi kubwa la binadamu wenye akili nyingi limechangia mawazo... Kuanzia kwenye kulinda kipaji chake, jina lake, biashara na kesho yake...
Nimeiona akili ya Neymar Jr niliposoma ile statment ya Yohan Cruyjf...
Alisema hivi "Epukeni kutengeneza zizi ili kuweka mafahari wawili"
Neymar amebet...
Kwanza ametazama kuwa Barca inaenda kupotea kabisa... ubora wao kimwili uko karibu na jeneza kuliko mikono ya madaktari... wazo hili huenda lipo sahihi kwake...
Kwanini...
Wakati Pirlo anaenda Juventus aligundua kuwa Serdoff, Inzagh na Maldin umri umeenda... Ufalme wao ulikuwa jirani na mauti kando ya kaburi....
Kabla ya kumuwaza huyu fundi wa Kibrazil mwenye miguu yenye nta iliyofunga ndoa ya Kikristu na mpira... angalia umri wa Pique, Messi, Iniesta na Suarez?
Ricardo Kaka naye alipoona Ac Milan inapotea, naye hakususua kupokea kile kilichotoka kwenye mfuko wa Perez... Uchizi siyo kupokea ila kutopokea angekuwa mwendawazimu kamili...
Neymar amegundua kizazi cha Catalunya kinakwenda Kenya kwenye uchaguzi, hana uhakika kama Mungiki watakiacha salama...
Pengo la Puyol mpaka sasa halijazibika... Ndicho kilichopo kwenye pengo la Xavi... Hata kivuli cha Alves holaaa... Hakipo kwenye unyunyu wa mashambulizi kutoka mbavu za kiumeni kulia....
Iniesta huyooo anasepaa umri hauna urafiki na mapafu na miguu yake tena...
Messi anavunja ndoa ya kwenye ubora wake muda sio mrefuu... Mpaka sasa anaendelea kutawala kwa nguvu ya dola na siyo matakwa ya sanduku la wapiga kura....
Neymar hapo amegundua anahitaji miaka miwili mpaka mitatu tu magazeti yataanza kuita Messi flop na Ronaldo veterani... Wakati huo atakuwa ana umri wa miaka 27, ni kipindi na nyakati muafaka kabisa wa kiwango cha mchezaji bora wa dunia...
Mpaka hapo washindani wake ni Hazard, Griezman, Delle Ali, Pogba na Dybala kama siyo Mbappe...
Hana cha kupoteza hapo... labda Sepp Blatter arudi tena kuwa rais wa Fifa hiyo tuzo ampe Messi kama ile ya 2010 ambayo hata mtoto wangu aliyekuwa tumboni wakati huo aliamini Xaiv na Iniesta mmoja wapo alistahili... Hata ile ya 2014 mikono salama ya mlinda milingoti mitatu ya Ujerumani na Bayern alistahili... Lakini Fifa ya Blatter ikapeleka kwa Messi.
Hivyo anaamini katika kipindi cha miaka miwili ijayo atasifiwa kwa kuwa mbeba timu ya PSG na anafahamu fika kuwa La Liga inabebwa na Messi na Ronaldo, anataka na yeye asemwe Ligue One ni ya Neymar Jr tu... anajua hata Barcelona ikibeba kombe la Fly Emirates sifa ni kwa Messi... sasa kwanini asiende mahala ambako ana uhakika wa vikombe ambavyo magazeti ya El Quip yatapambwa na picha zake?
Kama Barcelona itashindwa kuziba pengo la Xavi, Puyol na Iniesta msishangae kuona muda sio mrefu Messi naye huyoo kasepa...
Neymar Jr ameona mifuko miwili...
Mfuko wa lawama za Barcelona mbovu atakayoachiwa na Messi... au mfuko wa Billion 40 kwa mwaka kutoka kwenye vikoi na kanzu za Kiarabu...
PAMBANA NA HALI YAKO...
Leave a Comment