PEREZ HATOJALI MAKOFI YA CAMP NOU

TUBONGE KIDOGO KISOKA

Na Privaldinho

Mesut Ozil aliondoka Real Madrid, kila mtu alisikitika kwa maamuzi yale. Sababu za kuuzwa kwake zilikuwa na figisu Figisu. Naweza kusema yalikuwa mamuzi ya Florentino Perez. Hakujali ufundi wa Ozil ila kuna kitu alikihitaji zaidi.

Alihitaji kilichofanyika Stamford Bridge kwa Steven Gerrard kijifanyike kwake. Aliumia sana 2005, pale Ronaldinho alipoibuka Chipsi pale pale Bernabeu. Mwaka 2005 pale pale bernabeu wahispania waligeuka kuwa wabunge wa chama fulani ambao wao kazi yako ni kupiga makofi na kusema ndio walishindwa kuvumilia alichofanya Ronaldinho, chuki ziliwajaa lakini mikono yao iliwasha. Ilibidi tu wampigie dinho makofi

Wachezaji watano wamekwisha ondoka na heshima Bernabeu, 2005 Ronaldinho, hata hasimu wao mkubwa mwaka 2009 messi nae aliibuka Mfalme bernabeu, Del Piero pia hakuwaacha salama. 2015 unafiki ulikuwa unga, maji yalizidiwa, Ilibidi wamwage mboga wapike uji. Walipata kichapo, na bado walisimama na kumpigia Iniesta Makofi.

Hayupo, na simjui aliyewah kupigiwa makofi Camp Nou kutoka Madrid. Lakini wakati Stefano Relando anaandika kwa herufi kubwa kwenye gazeti la mjini Madrid, alisema Isco ni lulu ya baadae kwa Wahispania. Huenda Perez aliposoma hiki kichwa cha habari alitabasamu na alijiamini kuwa kuondoka kwa Ozil sio pengo.

Kwa bahati mbaya Matarajio ya Perez kwa Isco yalianza kukauka. Isco alikuwa na misimu mibovu, alianza vibaya mno. Kila mtu alianza kumtukana. Lakini Mara ghafla amekuja Zinedine zidane, amekuja na petrol, amechoma kichaka alichopo Isco. Kabla sijaendelea nataka tujikumbushe kidogo. Takwimu zinasema Kwa miaka kadhaa Madrid imecheza bila kuwa na kiungo wa kihispania mwenye uhakika wa namba klabuni hapo baada ya kuondoka akina guti na xabi.

Huenda Isco akazina pengo. Kubali ukate urithi wa Iniesta timu ya taifa kwa sasa upo kwenye umbo la Isco. Isco ni mchoyo sana, ni mgumu sana kumnyang'anya mpira mguuni mwake. Ana mguu kama kijiko. Alichonyimwa ni jicho la tatu ambalo Iniesta analimiliki (kutoa pasi muhimu na kwa wakati). Kwa misimu miwili Zinedine ametuonesha kichaka walichojificha wanafiki wa Isco na amekwisha kukichoma. Isco ambaye aliandikwa na Relando na kumfukuza Ozil Madrid hatimaye ameonekana.

Mechi ya Mwisho  mashabiki wa barca walijifanya hawakuona alichofanywa Rakitic na Modric. Ila kama angekuwa mhispania mwenzao naamin Modric angepigiwa makofi. Huenda wasimpigie Assensio kwa kigezo cha Umri na huenda pia wasimpigie makofi Isco kwa kuwa alisema barca ni wabaguzi lakini kubali ukatae kama Mashabiki wa Liverpool walishindwa kumpigia Ronaldo Makofi akiwa na Man utd lakini roho ziliwasuta wakampigia makofi akiwa na madrid pale pale anfield. Hivyo huenda mashabiki barca watampigia Isco makofi akiwa na timu ya taifa.

Huenda Furaha aliyo nayo Perez kuona kiwango cha Isco kinavyokua hata leo tukimfuata tukimwambia atulipie deni la bombadier anatulipia na anatuongezea nyingine. Isco alitukanwa sana mwacheni perez acheke, msipompigia makofi tabasami la Perez linamtosha isco....


No comments

Powered by Blogger.