ACHAGUE MOJA, AKOMAE KAMA TOTTI, AU ASALIMU KAMA OWEN



Na PrivaLDINHO

Ogopa hili swali kutoka kwa mwanao "baba kwanini huendi kazini" ? Ushawahi kujiuliza Carzola anajisikiaje pale India Ursula akimuuliza baba mbona huchezi tena mpira? Wakati Carzola 2012 Carzola anajiunga Arsenal Mji wa Llanera, Asturias wenye zaidi ya wakazi 13,000 walijaa kwenye kumbi za Video kumtazama Carzola. Ubora na Ufalme wa Michael Oweni ulinasa kwenye misuli ya nyuma ya goti lake tokea akiwa na miaka 19.

Michael owen aliteseka na Majeruhi maisha yake yote. Alipofika mwaka 2013 aliona bora Dr leakey wa England ili acheze mpira wa mdomoni kwenye vituo vya Tv baada ya Mateso ya misuli kwa kipindi kirefu. Kipindi cha nyuma kidogo nadhan ilikuwa mwaka 2007 Dr Richard Steadman alimweleza Ji sung Park kuwa opereshen yake ya goti itamweka benchi mwaka mmoja, haikuwa taarifa nzuri kwake kabisa. Huyu Dr maarufu aliwahi kuwatibu akina Ronaldo, Ruud van Nistelrooy, Michael Owen na Alan Sheare na kuwaeleza wazi kuwa matatizo yao ya misuli haiwezi kuwaacha salama. Wakati Park akiwa nje mwaka mmoja Carzola nae tokea mwezi wa 10 mwaka jana hayupo uwanjani. Dr wake ndugu Roman Cugat huenda ndiye mwenye majibu sahihi kwa mtoto wa Carzola ambaye anamuuliza baba kwanini huendi kazini. Jibu la Cugat kwa mtoto wa Carzola ni moja tu. Amweke wazi kama Steadman alivyofanya kwa Delima. Amweleze ukweli kuwa baba hawezi kurudi uwanjani hivyo atarudi Lugo de Llanera in Oviedo (nyumbani kwao).


Michael Owen aliumia mnamo tar 12 mwezi wa 4 mwaka 1992 akiwa na Liverpool kule leeds. Hakuwahi kuishi kwa amani uwanjani. Mwaka 2007 alikaa nje ya uwanja takriban siku 315. Achana na 2012 ambapo alikaa nje kwa siki 129. Maisha haya ya Owen kushindwa kuishi kwa amani ndiyo yanampeleka Carzola llanera. Wakazi wa Asturias walizoea kumuona Carzola akikatiza mitaa ya Oviedo na mchumba wake Ursula baadae wakawa wanamwona akikatiza misitu akina Vidic, Terry na Cahil baada ya muda hawamuoni tena. Wamemisi kumuona Carzola akimpa Furaha Wenger. Mashabiki wa Arsenal kote duniani wanapaswa wawe wavumilivu mpaka hapo mwezi wa 10. Lakini bado Dr wake Roman Cugat ameshauri Carzola aachane na soka. Tokea mwezi wa 10 mwaka jana Carzola atatumia siku 346 akiwa benchi. Ana umri wa miaka 32 kwa sasa, unategemea nini?

Ingawa Carzola Bado anaamini kuwa pilipili ni tamu kuliko sukari, ana Imani na misuli yake kuwa ina uwezo wakupambana majira yote, lakini imani yake hii bado kwangu ni kama Imani ya wayahudi wanaomsubiri masia au Imani ya kusubiri Tanzania ya Viwanda. Katika miaka 8, Carzola amelitumikia benchi siku 608. Takribani miaka miwili amekuwa akitembea na magongo. katika kipindi hiki Arsenal imejengwa chini ya Alexis Sanchezi, akiwa kama Mshambuliaji. Lakini pia ameletwa Alexandre laccazete. Bila shaka Sanchez atatokea pembeni kumpisha laccazete. Huku Ozil nae atacheza pembeni. Namba nane kwa Carzola itakuwa uwongo, misuli ya Carzola itaanza ushindani na Granit Xhaka. Nje yupo Ramsey, pia yupo Elneny. Usisahau kuwa Ozil atasimama kama namba 10, Walcot nae anapigania namba, na usisahau kijana wa Mwendokasi Bwana Alex Chamberlain. Chumba cha Carzola ni kama kimeshanunuliwa. Mashabiki wa Arsenal watatamani kunirushia mawe, lakini niwaambieni tu ukweli, tafuteni video za Falcao aliyetokea benchi baada ya kukaa miezi 8 alikuwa na hali gani.


Labda tu tujiulize unafikiri swali la Enzo (mtoto wa Carzola) kwa baba yake linaweza kujibiwa kirahisi kwa hali hii? Kwenye umri huu wa Carzola na hali aliyo nayo atamjibu nini mwanaye? Kama sio kumwambia naenda kesho kwa tabasamu lenye sura ya kikwete huku ndani  yake huku tunafaha ndani yake ana huzuni sawa na aliyo nayo lipumba?


Lakini kwa upande wangu huu ni wakati wa yeye kupunguza ruti za hospitali kila siku. Kiasi cha pesa alichokitumia kwenye upasuaji nadhani ni vyema arudi Cimavilla na fukwe za Abba Kaya kule Gijon akapunge upepo na mke wake Ursula. Aliyoyafanya ni makubwa. Asijikute Fransesco Totti. Misuli yake na akili yake ina mgogoro kama wa CCM na UKAWA haviwezi kupatana kamwe.

Carzola amewekeza sehemu nyingi mno. Mwaka 2014 aliwekeza kwenye kampuni ya ardhi na makazi yenye ofisi zake Liverpool na Man United ijulikanayo kama Capital Centric Investments LLP. Ambapo yeye na Luis Suarez, Mikel Arteta na Jose Henrique waliwekeza zaidi ya Euro milioni 50 na wanategemea kupata faida ya sio chini ya Euro 250 milioni kwa mwaka. Wote walikuwa wakurugenzi kwenye kampuni moja licha ya uhasama wao wa kitimu wakiwa pamoja na akina Higgins. Nadhani huu ni wakati wa yeye kusimamia mambo yake Mengine ya kibiashara pamoja na wa ubavu wake. Amebarikiwa kuwa na mwanamke msomi waliyetokea nae kijiji kimoja. Hajamjua kwa sababu ya Umarufu kama Diamond na Zari. Walipendana tokea kwenye dhiki. Tena mkewe akiwa na miaka 9 tu, alikuwa anaenda na baba yake kumwangalia Carzola kulee Oviedo. Mke wake huyu ni msomi mkubwa tu. Ana Degree ya   sayansi ya elimu ya viungo. Ni muda muafaka wa yeye kuwekeza zaidi na kufanya mambo mengine.. ni ngumu kukubali lakini sijui kama kuna namna ya Carzola ambaye muda sio mrefu atafikisha miaka 33 kurudi katika ubora wake. Kila la kheri kwake na nampa pole pia...

ila APAMBANE NA HALI YAKE



No comments

Powered by Blogger.