WEST HAM MNACHOKITAKA MTAKIPATA

PrivaLDINHO

Nawaza tu...

Ligi kuu imeanza..

West Ham kuna kitu nmekiona kwao. Ni kama wanakunywa mkojo kwa kisingizio cha kiu. Wamefanya usajili wa wachezaji wengi kwa kigezo cha ufinyu wa kikosi.

Usajili wao wa fujo umenikumbusha yale ya akina Mark Hughes na Harry Redknapp miaka ile walipokuwa na QPR. Ilisajili wachezaji wengi kwa fujo na wengi wao walikuwa wazee. Kuanzia Julai mosi 2012 kocha Mark Hughes aliwasajili akina : Ryan Nelsen (Tottenham) bure; Andy Johnson (Fulham), bure; Robert Green (West Ham), bure; Samba Diakité (Nancy), £4m*; Park Ji-Sung (Man United), £2.5m; Junior Hoilett (Blackburn), £4m; José Bosingwa (Chelsea) bure; Júlio César (Inter Milan), haikuwekwa wazi; Esteban Granero (Real Madrid), £9m*; Sam Magri (Portsmouth), bure; Stéphane Mbia (Marseille), £5m*.Harry Redknapp aliwasajili akina Tal Ben Haim bure; Loïc Rémy (Marseille), £8m*; Yun Suk-Young (Chunnam Dragons), £1m*; Christopher Samba (Anzhi Makhachkala), £12.5m; Jermaine Jenas (Tottenham) bure.

West Ham wao wamekua kivingine...

Hawajanunua bure ila ni kama wanakula maganda ya miwa kwa kigezo kuwa jungu kuu halikosi ukoko. Wao wamesajili wazee kwa gharama kubwa. Wametumia kiasi kikubwa kufanya walichokifanya QPR.
Wamemsajili Chicharito miaka 29, zabaleta miaka 32, Arnautovic miaka 28, Joe Hart miaka 30.

Wachezaji tegemezi katika kikosi hiki wengi wao umri umeenda kidogo, Makipa, Hart 30, Adrien 30, mabeki Reid 29, Ogbona 29, zabaleta 32, Jose Fonte 33, J collins 33, Koyoute na Ayew 27 sio mbaya, Mark Noble 30, Andy Carrol 28,

Wastani wa Umri wa kikosi chao ni kama miaka 27. Kimahesabu hii timu inatarajiwa kutengenezwa upya mwakan maana wengi wao hapa umri umeenda sana, na wengine wanalotafuta jua la jioni kuanikia nguo. Sisemi kama West Ham watakuwa na msimu mmbaya, lakini kwa nionavyo mimi hawatakuwa na msimu mzuri. Yaliyowakuta mwaka jana yanaweza yakajirudia na mwaka huu

Msimu huu tayari ameshakunywa 4 kutoka kwa Mashetani Wekundu, msimu uliopita walitwangwa na Chelsea 2 1, kisha wakashinda kwa bournemouth 1 bila, kisha wakabatizwa goli 3 kwa moja kutoka kwa City, Watford nao wakatoa karamu ya magoli manne kwa mbili nyumba kwa West Ham, ndipo West Bromwich nae akajipigia 4 2. Southampton nao walijipia vitatu kwa Nunge.

Watabiri wengi wameitabiria Huddersfield vibaya msimu huu. Lakini kwangu mimi nina mashaka na utume wa Bilic. Huenda akawa kundi moja na Conte. conte ameonesha waziwazi kupanic baada ya kuonekana akihaha kwenye mchezo dhidi ya Burnley huku akionekana kuzuzana hata na makocha wenzie. Kama Conte ataandoshwa Klabuni hapo basi naona Bilic akipanda mlima kilimanjaro na vile viatu vya kike virefu.


No comments

Powered by Blogger.