NYOTA INAYO ANDAMWA NA WINGU
Na San Andy
Usiku wa september ishirini kuamkia ishirini na moja klabu ya Borussia Dortmund inaandika rekodi ya kufunga magoli 3000 katika ligi kuu ujerumani. Maelfu ya mashabiki waliopo ndani ya dimba la Signal Iduna park wana washudia nyota wao kama Kagawa, Aubemeyang na Pulisic waking'aa
Anga hili hili la ulimwengu wa soka linalo ruhusu nyota za vijana wale zing'ae ndilo ambalo wingu lake limegoma kuacha nyota ya Marco Reus ing'ae badala yake wingu jeusi la majeraha limeendelea kuandama nyota ya kijana huyu
Licha ya mng'ao mkubwa wa kipaji na uwezo alionao Marco bado majeraha yame endelea kuwa sehemu ya maisha yake. Sio mara ya kwanza kwa wingu hili la majeraha kumnyima Reus nafasi ya kuacha alama katika anga la sokka. Ni wingu hili ndilo lili mfanya asiwe mmoja ya wachezajj wa kijerumani walioweka historia duniani baada ya kutwaa kombe la dunia mwaka 2014 katika dimba maarufu la Marracana ndani ya ardhi ya Brazil.
Bila ya chembe ya huruma wingu la majeraha lilienda sambamba na nyota ya Marco Reus hadi kumpelekea kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya ulaya kwa ngazi ya taifa yaani EURO 2016. Haikuishia hapo bado wingu hili limegubika nyota ya Marco Reus wakati yeye mwenyewe akiwa kitandani anauguza jeraha la goti litalo mfanya aendelee kuwa nje ya uwanja hadi mwaka 2018
Kwa wale wachache wenye macho makali nina hakika wamewahi shuhudia uwezo mkubwa alionao Marco Reus hili huonekana pindi nyota ya Reus inapofanikiwa kutoroka wingu kwa muda fulani hakika ni kati ya nyota zenye nuru ang'avu zaidi ndani ya ulimwengu wa soka
Inauma sana unapo maliza kusoma majina hamsini na tano ya wachezaji wanaowania kuwepo kwenye kikosi bora cha mwaka FIFA Pro XI na kugundua hakuna jina la Marco Reus huku kukiwa na wachezaji ambao baadhi uwezo wao ni nusu ya Reus. Hakuna wa kumlaumu juu ya uwepo wao na kutokuwepo kwa Reus ni kwasababu tu lile wingu la majeraha limeonekana kupenda zaidi kuishi na nyota Reus kwa hali hii unafikiri ni muda gani ulimwengu utaweza kuona vizuri uwezo wa Marco? Jibu ni jepesi tu ni siku ambayo wingu hili litaamua kuacha nyota ya Reus. Lakini inawezekana wingu likatoka kwenye nyota hii wakati mwanga wake umeanza kufifia maana kwasasa Marco Reus ana umri wa miaka Ishirini na minane na hatufahamu ni lini wingu lita jitenga nae
Wingu la majeraha limezuia baadhi ya nyota nyingi kumulika anga la soka ni kwasababu hii hata wale waishio chini yake imepelekea kutojua kiasi cha ubora na ung'aavu wa nyota hizo. Wenye macho makali wanaweza kuona baadhi ya nyota hizo zilizo nyuma ya wingu la majeraha.
Utapokuwa umetuliza macho yako angani kutafuta kuuona mwanga na ubora wa Marco Reus tafadhali usisahau kuangalia na nyota nyingine kama ile ya Jack Wilshere, Daniel Sturridge na Ilkay Gundogan kama ilivyo kwa Reus hawa pia kuna wakati huwa wanatoroka nyuma ya wingu.
Leave a Comment