ANACHOTAKA WENGER KINAPOTEZA ALICHO NACHO

.

Na San Andy

Arsene Wenger sidhani kama kuna mpenzi wa sokka la ulaya kwa karne hii ya ishirini na moja ambae halifafahamu jina hilo,Ndio una shindwa vipi kufahamu jina la kocha mkubwa kama Wenger? Mmoja kati ya makocha wawili pekee waliowahi kutwaa kombe la dhahabu pale Uingereza kwa kushinda ubingwa wa ligi bila ya kufungwa


Kitakwimu huyu ndie kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Arsenal ametwaa kombe la ligi mara tatu na FA cup mara saba,Hivi ni kati ya vitu vingi vilivyompatia "Heshima" Arsene Wenger,Nakumbuka niliwahi kuambiwa "Unaweza kutumia muda mrefu sana labda hata maisha yako yote tokea uwepo juu ya uso wa dunia kutengeneza heshima uliyonayo hii leo,Lakini inaweza chukua siku moja tu au chini ya hapo kupoteza heshima hiyo"

Wenger alianza kujitengenezea heshima yake ndani ya Arsene mwaka 1996 pale alipo ajiriwa kama kocha mkuu wa klabu hiyo,Ndani ya miaka hii ishirini na mmoja kuna vipindi viwili vimetokea kwa Wenger,Kwanza ni kuanzia 1996 - 2004 huu ndio wakati alio jijengea heshima,2005 - 2017 huu ndio wakati alioanza kupoteza heshima na mapenzi ya mashabiki wa klabu hiyo

Ndani ya miaka hii kumi na miwili Wenger amefanikiwa kutwa makombe makubwa manne tu ambayo ni kombe la FA mara akitwaa mara nne,Kwa ukubwa wa timu ya Arsenal mashabiki walihitaji ndani ya hiyo miaka kumi na miwili angalau wawe wameshinda klabu bingwa dunia,Klabu bingwa ulaya,Europa league ama kombe la ligi kuu Uingereza lakini swala hili kwa linaonekana kama ni ndoto katika utawala wa Wenger wanachotaka ni kumuondoa tu mzee huyo

Hivi unadhani Wenger hataki kuondoka Arsenal? Kama unafikiri hivyo unakosea sana,Wenger yupo tayari kuondoka ndani ya Arsenal ila anahitaji  kuondoka kwa heshima kama ilivyokuwa kwa wazee wenzake Heynckes na  Sir Alex Ferguson,SAF alitangaza kuachana na timu akiwa na medali ya Barclays Premier League shingoni na kombe likiwa uwanjani

Najua una kumbuka vizuri sana kuwa Heynckes wakati anasema anastaafu watu wa store walikuwa wakipanga makombe matatu mapya na ndani ya chumba cha kuhifadhia makombe ya Bayern Munchen,Bado unataka Wenger armstaafu akiwa na FA cup mkononi?

Hiki ndicho ambacho Wenger ana kitaka kurudisha heshima iliyopotea lakini bahati mbaya sana naona anaendelea kuipoteza hata ile heshima ndogo aliyobaki nayo,Mfano mdogo kama Wenger ange achana na Arsenal kabla ya msimu wa 2016/17 leo hii tungesema "kwa kipindi chote ambacho Arsene Wenger ameifundisha Arsenal hajawahi kukosa kufuzu klabu bingwa ulaya" sio heshima hii?

Wenger aliongeza miaka miwili  ya kuendelea kuinoa Arsenal kwa lengo la kurudisha heshima lakini alisahau kabisa kuwa alisha haribu sana,Sio siri hata kidogo kuwa Arsenal sio timu inayovutia sana wachezaji wakubwa,Nasema hivi kwakua hivi sasa Wenger hawezi fanya michezo yake ya kununua mchezaji mdogo na kumkuza kwasabu ana muda mfupi sana kwahiyo anachohitaji ni kununua wachezaji bora ili wampe anachotaka,Tatizo ni je mchezaji gani mkubwa atakubali kwenda sehemu ambayo wengine wanakimbia? Sina maana kuwa hakuna wataoenda kabisa ila watakuwa wachache

Ozil na Sanchez nao sio tu wata msababishia heshima kushuka ila kwasasa tu wanamtesa na mawazo,Ifikikapo dirisha kubwa la usajili mwakani hawa wote watakuwa wachezaji huru kwenda wanapotaka inamaana Arsene na Arsenal yake hawatopata kitu,Lakini kama anataka kukwepa hasara hii itambidi awauze kwenye dirisha la usajili la january ambapo Sanchez anataka kwenda Manchestet City na Ozil inasemekana anataka  kwenda Manchester United hii maana yake ni kumpa silaha adui unayetaka kumshinda

Shabiki gani wa Arsenal atafurahi na kuendwlea kumuheshimu Arsenal Wenger huku anafahamu wachezaji wao bora kabisa waliuzwa au waliachwa hadi wakaondoka bure chini ya utawala wa Wenger,Kumbuka hawa watu bado wana kumbuka RVP kwenda Man Utd,Cole to Chelsea na Nasri kwenda Etihad,Tatizo soo kuwauza ila kumuuzia mtu ambae unawania nae ubingwa wa ligi hapa ndipo mashabiki wake wanapozidi kumshushia heshima

Alichoamua kufanya Wenger ni sawa kabisa na Sepp Blater,Blater baada ya kuona watu wamemchoka na wanahitaji mtu mpya hakujiuzulu alienda kwenye uchaguzi na akamshinda Prince Alii baadae akatangaza kujiuzulu,Alichotaka kukionyesha ni kuwa bado ana uwezo na watu wanamkubali ndiomana walimchagua tena

Wenger anataka kuonyesha kuwa bado ana uwezo wa kufanya makubwa ndani ya Arsenal na kurudusha heshima yake lakini bahati mbaya sana nahisi hii geshima anayoitaka inawndelea kumfanya apoteze heshima aliyonayo


No comments

Powered by Blogger.