RANIERI NENDA SOFAPAKA, KISHA RUDI KING STREE NA QUEEN STREE UANGALIE ILE SANAMU
RANIERI NENDA SOFAPAKA, KISHA
RUDI KING STREE NA QUEEN STREE UANGALIE ILE SANAMU
MIWANI YANGU.
Mnamo mwaka 2009 sofa paka
walitwaa ubingwa wa KPL yaan ligi kuu ya Kenya. Hakuna aliyedhani klabu ndogo
kama ile ingeweza kufurukuta mbele ya timu kama Gor mahia, tusker na klabu
nyingine kubwa Kenya kama FC leopard kama wanavyojiita wenyewe INGWE. Mwaka uliopita
pale England nako palitokea maajabu kama haya haya ya Kenya Leicester city
anatwaa ubingwa mbele ya timu kubwa nne za England. Msimu wa England umeanza
tena, kila mtu ana neno lake la kuongea, wakati EPL inaanza Kenya jadithi nayo
ni tofauti kidogo, wale mabingwa wa 2009 sofapaka wanapambana na Ushuru FC
pamoja na Nairobi city star kutokusuka daraja. Sofa paka kwa sasa
wamejikusanyia alama 15 tu huku nairob city ambao wao wana alama 14. Ushuru fc
wao tayari wameweka kibindoni alama 22 huku wote wakiwa wamecheza michezo 23. Nairobi
city star wao wanashikilia mkia wakiwa wako nafasi ya 15, sofa paka 14 kisha
ushuru 13. Wote hao wanapambana kutokushuka daraja. Anaeongoza ligi kwa sasa ni
tusker FC ikiwa na alama 44 huku wakifuatwa kwa karibu sana na Gor mahia wakiwa
na alama 37 na mchezo mmoja mkononi.
Mlinzi wa zamani wa Mathare
United Noah abich ambaye kwa sasa anakipiga sofapaka juzi nilimnukuu maneno
yake akisema kuwa ni ngumu kwa sofa paka kushuka daraja, watapambana mpaka
jasho lao la mwisho kuhakikisha kuwa wanabaki ligi kuu nchi Kenya. Sofa paka
ambao wanajulikana kama Batoto Ba Mungu msimu huu walikumbwa na matatizo lukuki
ya kifedha yaliyopelekea klabu hii kupoteza takribani wachezaji 21 ingawa
ilisajili wachezaji wapya 25 ambao wote walikuwa wakiwango cha kawaida. Klabu ya
sofapaka ilipoteza wachezaji wake wa kikosi cha kwanza wote. Mchezaji wao
hatari John Barry ama kwa jina lake kamili John baraza alistaafu kucheza soka
na akaamua kujiunga na benchi la ufundi la klabu hiyo. Mnamo mwezi wa kwanza
Mwenyekiti wa klabu hiyo Bwana Elly Kalekwa alipitia katika wakati mgumu
kifedha kitu ambacho kilimfanya kocha mkuu wa klabu hiyo David Ouma kutangaza
kuwa klabu hiyo haina uwezo wa kuwanunua wachezaji wenye majina makubwa.
John barasa akiwa na tuzo ya mchezaji bora mwaka 2010 |
Tukirudi Pale England Jamie Vardy
ana miaka 29, muda sio mrefu nae ataanza pensheni hasa kutokana na mfumo wa
ligi kuu, Leicester city tayari wameshampoteza mchezaji wao mahiri kabisa N’golo
kante, amekuja Mussa ambaye binafsi yangu namwona ni mwoga sana, bado ana roho
ya kiafrika ya kuogopa kukosea mbele ya rangi nyeupe, bwana mdogo grey bado ni
mzito nae ana akili inayoendana na rangi yake mzito kufikiri na kutoa maamuz ya
haraka. Leicester city uliyoanzishwa miaka 132 iliyopita wanarudi EPL tena
sijajua wanatetea ubingwa au wanapambana na hali yao. Tukirudi takribani miaka
40 hivi, Nottingham forest walipanda ligi kuu England mwaka 1978 na wakatwaa
ubingwa sawa tu na sofapaka na Leicester city. Msimu uliofuata Nottingham walimaliza
ligi wakiwa chini ya Liverpool kwa alama 60 liverpool wakiwa na alama 68 huku
mshambuliaji hatari wa kiingireza Garry Birtles akifunga magoli 14 na kuwa
mfungaji bora wa klabu hiyo. Kwa upande wa pili huku Kenya msimu wa pili wa
sofa paka wao walitwaa kombe la shirikisho huku ulinzi stars wakitwaa ubingwa,
walishinda pia kombe la Rais. John baraza aliibuka kidedea kama mfungaji bora
kwa jumla ya goli 15.
jarmie vardy akiwa na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi msimu wa 2015 |
trevor francis akiwa na kombe la UEFA 1979 |
Leicester wana kazi nzito msimu
huu, Jarmie Vardy alivunja rekodi ya Ruud Van Nestelrooy kwa kufunga magoli 13
kwenye michezo 11. Msimu huu wameuza ghali na wamenunua ghali, kante ameondoka
kwa Ada ya E30 na wamemnunua Islam Sliman kutoka sporting CP kwa ada ya E29
ikiwa ni rekodi kwa klabu hiyo. Nottingham nao msimu wa 1978 hawakuwa nyuma
kwenye usajili Ingawa walisajili wachezaji wawili tu, Garry milly aliyetokea
klabu ya watoto na Trevor fransic aliyetokea Birmingham city kwa ada ta
1,000,000 aliyweka rekodi ya usajil, lakini walimuuza Peter white kwa ada ya
200,000 kwenye Newcastle. Msimu huo wa 1979 nottingham forest ikiwa ni kwa mara
yao ya kwanza kushiriki kombe la Yuropa ambalo kwa sasa ni UEFA ilitwaa ubingwa
ule. Narudia tena. Msimu huo wa 1979 nottingham forest ikiwa ni kwa mara yao ya
kwanza kushiriki kombe la Yuropa ambalo kwa sasa ni UEFA ilitwaa ubingwa ule. Mwaka
huo huo walitwaa charity shield, na kombe la ligi ambao wengi wanaliita Carling
Cup kwa sasa likijulikana kama fly emirates Fa cup. Fainali ya YUropa walicheza
na malmo Fc na Francis aliwainua waingereza kidedea katika ardhi ya Ujeruman
kwenye uwanja wa Olympiastadion ulikuwa ukibeba takriban ya mashabiki 57,000.
Sofapaka na Nottingham
wanaonekana kutoa somo kwa Leicester city. Ranieri hapaswi tu kuangalia Man united
wamemsajili pogba kwa gharama kubwa, gharama kubwa waati Fulani sio tija. Itakuwa
aibu kubwa sana kama tutaona Leicester wanapambana kutokushuka daraja. Nottingham
wao msimu wa pili hawakuhangaika kushuka daraja, ule msimu Chelsea na
Birmingham wao ndo walioshuka daraja. Tusitegemee vipigo vya haja kwao maana
ule msimu tottenham ndiye aliyepewa visago vya maana Liverpool 7 0 tottenham,
tottenham 0 5 arsenal. Nadhani ni wakati wa Leicester city kuonesha kuwa wao
hawajabahatisha. Imechukua takriban miaka 7 ndipo sofapaka anaelekea kushuka
daraja.
Brian Clough alikuwa kocha wa Nottingham kwa miaka takriban 18 na ndiye
kocha mwenye mafanikio makubwa zaid ndani ya klabu hii,
Brian Clough
ametengenezewa sanamu kubwa maeneo ya King street kwa mafanikio makubwa
aliyoyapata, je ranieri anaweza kuwekewa sanamu ndani ya nchi ya watu? Kwa lipi?
Labda Leicester city wakutengeneze, ila je utatengenezewa sana kwa heshima kama
ya Clough? Kama ranieri anahitaji heshima ya clough kwanza inambidi afanye
makubwa ambayo waingereza watamthamin.
Huenda Ranieri nae akaonekana kocha
mwenye mafanikio ya kipekee, lakini Ranier atathaminika kama clough endapo tu
atafanya mambo makubwa msimu huu. Yaani asitoke kapa kabisa. Nottingham walitwaa
tena kombe la UEFA mwaka uliofuata. Je Leicester nao watwae uefa? Daah ni kama
nawaonea Leicester city hasa katika kizazi hiki cha Messi na Ronaldo.
Labda tuipe Leicester city
mtihani mrahisi tu, msimu huu wapambane kubaki nafasi tano za juu, au afike
hatua ya robo fainali ya UEFA kama huko kugumu basi tumwone Uropa akifika nusu
fainali. Vipi huu mtihani utamfaa Ranieri? Kama Ranieri hakubahatisha basi afanye
hayo maswali niliyompa hapo juu. Vipi bado ni mgumu?
claudio ranieri akiwa na ubingwa wa ligi |
Mtihani wa clough ulikuwa
mgumu sana. Yaani timu imepanda daraja na inachukua ubingwa wa ligi na kutwaa
UEFA kwa miaka miwili mfululizo? Sasa ugumu wa Ranieri uko wapi? unadhani miaka
ile hakukuwa na mafundi?
brian Clough akiwa na kombe la UEFA |
Walikuwepo akina Bryan Robson aliyenunuliwa million
1.7 na Manchester united mwaka 1980. Hawa Nottingham wenyewe walikuwa tayari
kutoa Million 1 ikiwa na mchezaji wa kwanza kutoka England kununuliwa ghali
mno, je Leicester mmesajili nani? Je mtashinda huu mtihani kweli? Kuna mwanaume
mwingine alielekea wolverhampton akitokea aston villa kwa million 1.4 bwana andy grey. Kuna
mwingereza mmoja alikuwa fundi sana kevin Keegan miaka ile alikua hamburg, kuna
kijana mwingine alikuwa hatari sana kwa kunyumbulika wazee wazamani walivyokuwa
wanamwita ndugu Laurie cunnigham alipokuwa pale Madrid, aisee huku werder
Bremen wazee wa vunja vunja alikuwepo bwana David Watson, sasa tukienda
ufundini walikuwepo akina zico, Socrates, edinho, na mwanaume falcao. Sio kwamba
hakukuwa na mastaa kama sasa, walikuwepo. Ranieri nenda Kenya ukishagundua
kwanini sofa paka waanazingua Rudi sasa mpaka West Bridgford kisham mtafute
fawaz Al hasawi mwombe ruhusa ya kuongea na bwana Philippe Montainier, mwambie
Montanier kuwa umeongea na bosi wake ustazi hasawi akakuruhusu uongee nae ili
akuoneshe makabrasha aliyoacha huyo kocha wa zamani wa Nottingham brian Clough
ili ujue alifanikiwa vipi miaka ile ya 70 Plz ranieri no excus do the exams. Wish
you luck.
clough alikuwa anapigisha pindi hata wakiwa safarini |
Leave a Comment